nipeni mimi hiyo nafasi ya ole naiko.
Tatizo kubwa la hizi issue ni kuwa kuna tofauti sana ya professionals view na activist view
Nikiwa kama Civil/Mining Engineer kuna nyakati ambazo siwezi kuongea na Lissu maana ideas nyingi ziko ki-activist zaidi kuliko professional point of view.
At a glance bado watu wengi hawajui mambo mengi ya madini nchi hii, tumekuwa wageni, na hatutaki kujua, wala kujishughulisha kujua, hivyo kila siku hizi issue zitakuwa za hivi hivi tu, kuongea kulaumu n.k
Kuna ya ukweli aliyoongea Naiko, nadhani challenge kubwa kuliko zote ambazo serikali ya sasa ina zi-face ni kuingia mikataba ya madini ambayo ni kichekesho, na ombi langu kwa activist kushika mpini hapo, mikataba ni mibovu saana, ambayo haiwezi kuelezeka wala kutamkika kirahisi
Tukija mambo ya mazingira they will always find justifications na ujanja wao wakiishapata justification ya mazingira basi inakuwa assumed kuwa hata mikataba ni SAHIHI!!! digressive technique!
Mikataba kwanza!!!!! kusema mazingira ni kusema mikataba iko sahihi!
Tatizo la mikataba wala siyo gumu au kitu cha ajabu kama wengi wanavyotaka watu waamini. Mikataba yetu ni mibovu kwa sababu walioiandaa hawaifahamu biashara ya madini kikamilifu, wengi wanadhani kwa kuwa ni wanasheria, basi wanaweza kuandaa mikataba ya kila aina hata kwa business ambayo hawaijui vizuri. Tunatakiwa kuwa na wataalam wa mikataba ya biashara ya madini ambao watashirikiana na wataalam wa biashara ya madini.
.
Waberoya,
..Chenge aliwahi kuulizwa kuhusu hii mikataba akasema wajibu wa Mwanasheria Mkuu si "kupatana bei."
..kuna watumishi wa serikali waliopewa hilo jukumu la kupatana bei hao nao wanapaswa kubeba mzigo wa lawama.
..haya makampuni ya nje yanapokuja hapa nchini huwa wana-hire wanasheria wa ndani, kwa hiyo hatuwezi kusema kwa uhakika kwamba tatizo ni wanasheria.
Sababu kubwa ni kwamba makampuni haya yana mitaji mikubwa, yana teknolojia na uzoefu mkubwa, lakini pia yana uwezo to absorb risks. Katika sekta ya madini kampuni inaweza kutumia $100m kufanya utafiti katika eneo fulani, na baada ya miaka kadhaa ya utafiti majibu ya mwisho ni kuwa 'the project is not viable', na kampuni ikaondoka. Tunao watanzania wangapi au kampuni ngapi hapa Tanzania ambazo zinaweza kutumia kiasi hicho cha pesa, zikawa zimepoteza na wamiliki wakaona siyo tatizo, kwa vile ndivyo biashara hii ilivyo.
Kwa mfano pale BuckReef (Biharamulo), IAM gold mpaka mwaka jana ilikuwa imetumia U$37m, wakaona mradi hauna faida, na wameondoka kurudi kwao. Haya makampuni yana uwezo wa kufanya hivyo kwa vile yana miradi mingi Duniani, wakati anapata hasara Afrika na Asia, amepata faida South America. Tusihangaikie sana umiliki wa migodi uwe wetu bali tuhangaike kupata faida kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini zinazofanyika Tanzania regardless who own those mines.
.........The Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation (ASAGBC) was being paid Sh16.4 billion every year to audit gold produced in the country while Tanzania Mineral Audit Agency (TMAA) last year was paid only Sh3.4 billion for the same work.................
http://allafrica.com/stories/201001140155.html
Mkuu napingana na wewe kwa hizo sehemu nilizotaja .
Umesema haya makampuni yana uwezomkubwa. na yanatumia teknolojia . Naamini Karne hii vifaa vya exploration usahiii wake ni mkubwa vile vile . Ukiondoa gharama exploration mwanzoni
Mpaka kampuni inaamua kuanza kuchimba inakuwa imeshafanya mahesabu na kuridhika kuwa kutokana na result z exploration yao uchimbaji utalipa
Uwezo wa kuchimba kwa faida wanakuwa wamezingatia pamoja na risks zote. Hakuna kampuni inakuja kufanya eploration au kuchimba bila cosideration ya risks . Kwa hiyo mpaka wanaamua kuweka magrader ya kuchimba ujue ni faida tuuuuuuuuuuuu
Kwa hiyo ukisema hao jamaa wa buckreef waliwekeza 37 $ millo na wakaona mradi hauna faida wakaondoka ujue kuna usanii . Mabepari hwafanyi kazi hivi. Ndio hap tunaibiwa mchana mchana.
- Ni operation costs au factors ambazo hawakujuua au kuzingatia zilizopelkea waanze kuapta hasara
Kwa sababu kwanza ukiweka pembeni kucheza na kiwango cha madini wanayochimba hawa jama pia wanacheza hata na vitabu vya mahesabu. Je serikali ina njia ya kuthibitisha au kuhakiki kma kweli waliwekeza 37$ mil na sio 15 $ Mil? Naamin Serikali inategemea Mabepari wawe Honest. Kitu ambacho ni kichekesho.
Hii imenikumbusha miaka kampuni moja ya mobile. ilifanya makadirio eti itaanza kuapta faida baadaya miaka 15. Is this realistic au ni ujanja wa kukwepa Kodi na malipo mengine. Style hii ndo inatumika kwenye madini
Ni Kweli uwezo wetu ni mdogo hatuna teknolojia na uwezo mdogo kwenye sekta ya madini lakini tunapodili na bepar tuhakikishe hawatukamui sana.
Ofisi yetu ya Auditing imeweka priority ya wa kufanya Auditing za accounting . Techincal Audit ya MAdini ndio tuliwategema Alex Stewart. Hawa nao walifanya kichekesho ile faida tuliyotakiwa kupata kutokana na kazi yao basi wao ndo wakawa wanaichukua
Nataka nikuhakikishie kuwa nipo kwenye Industry ya mineral Exploration kwa zaidi ya miaka 16, na hakuna kifaa hata kimoja kinachotumika kwenye exploration ambacho sijakiona au kukitumia labda kama kimeanza kutumika mwezi huu, ninavyozungumzia Exploration risks, nina uhakika na ninachokiongea lakini si nia yangu kuingia kiundani zaidi maana hiyo itakuwa ni long professional topic ila kwa ufupi unatakiwa ufahamu kuwa mineral or oil exploration start with 100% risk which continue decreasing as you continue exploring. Mimi mwenyewe binafsi nasimamia miradi mbalimbali ya utafiti ikiwa ni pamoja na bajeti zake. Kwa ufupi ujue kuwa kwa wastani katika duniani nzima 'in every 1000 gold exploration licenses/projects is only 1 license turns into 1 big gold mine', and this is the biggest reason why gold is expensive and will continue to be expensive. It is one of the most risk businesses. The day when the risk will much go down gold price wil not be much different from that of other metals like iron. Why precious minerals (like gold, diamond, tanzante, alexandrite, etc) are very expensive is because of their rarity and risks involved.
Tunapozungumzia IAM gold kutumia U$37m siyo hesabu zinazotokana na hisia bali ni kutokana na auditing reports. Haya mashaka mnayoonesha nayo ni kutokana na watanzania wengi kutokuielewa biashara hii kikamilifu lakini kwa anayeelewa vizuri anafahamu kuwa ni vigumu sana na wala haitegemewi kampuni kubwa ya uchimbaji madini iseme inapata hasara wakati inapata faida maana kufanya hivyo ni kujiua. Makampuni haya faida zao kubwa zipo kwenye masoko makubwa ya hisa duniani kote, na hisa zao zinapanda pale tu kampuni inapoonekana inapata faida, na ina miradi mingi mizuri in their projects potifolio.
Kusema kuwa makampuni haya hayawezi kuingiza pesa kwenye utafiti bila kujua kama kuna faida, nayo pia ni kutokufamu biashara yenyewe.Kuna tofauti kubwa kati ya Explortion na Mining. Mining huwezi kuanza kama hujui kama mradi huo una faida au hapana lakini exporation unaanza kufanya ili ujue kama mradi unaweza kuwa na faida au hapana, mpaka kufikia hatua ya kujua kama mradi una faida au hapana , tayari gharama unayokuwa umeingia ni kubwa sana. Na kampuni zinakuwa na licenses nyingi sana ili kuongeza uwezekano wa license mojawapo kugeuka kuwa mgodi huku nyingi zikiachwa kwa vile hazifai.
Mimi Sielewi mambo ya madini lakini najua kazi ya Internal Auditors ni kusadia mteja wao kukwepa kodi na malipo mbali mbali. Ndio maana nimesema serikali ikideal na hawa watu iwe na macho manne. Hii sio kwa kampuni za madini tu.Tunapozungumzia IAM gold kutumia U$37m siyo hesabu zinazotokana na hisia bali ni kutokana na auditing reports.
VANCOUVER - Tanzanian Royalty Exploration Corp. (TSX:TNX) says it has an opportunity to earn a 55 per cent interest in the Buckreef gold project in eastern Africa - formerly a holding of Iamgold Corp. (TSX:IMG).
Tanzania's state mining company, Stamico, would own the rest of the project, which is described as an advanced stage exploration project.
According to Canadian regulatory standards, the property contains about 265,000 ounces of gold on a measured basis, 83,000 ounces on an indicated basis and 507,000 ounces on an inferred basis.
Tanzanian Royalty said Tuesday that a definitive joint venture agreement is expected to be signed "in due course."
It said the Buckreef area has a long history of small-scale mining and exploration work, most of which was undertaken by the United Nations, the Tanzanian Mineral Resources Division, Williamson Diamonds and Iamgold, which brought the Buckreef property to its current stage.
source : http://www.winnipegfreepress.com/bu...anias-state-mining-corporation-112285264.html