Gwiji wa Sheria na Katiba, Prof. Issa Shivji, Agoma Kuzungumzia Dhana ya Udikiteta/Uvunjifu Katiba!

Wanabodi,

Nikiwa mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, leo nimehudhuria Mhandara wa Wazi wa Kongamano la Kavazi la Mwalimu Nyerere katika Ukumbi wa Costech hapa jijini Dar es Salaam.

Baada ya kumalizika kwa kongamano nilimtafuta Mkurugenzi wa Kavazi ya Mwalimu Nyerere, Prof Issa Gulamhussein Shivji ambaye ni mwanasheria nguli na mbobezi wa sheria ya katiba, yaani Constitution Law.

Baada ya kumpata kwanza nilimpongeza kwa kazi kubwa na kazi nzuri anayoifanya kwenye Kavazi hapo Costec na kabla ya hapo alipokuwa na Mwenyeki wa Kigoda cha Mwalimu.

Ndipo nikamtupia swali kuwa hizi kelele tunazozisikia kuhusu madai ya kuwepo kwa udikiteta nchini Tanzania unaodaiwa kufanywa na rais wa Jamhuri ya Muungano ambao pia unahusishwa na madai ya kuvunjwa kwa katiba ya JMT.

"Jee tuhuma au madai haya yana ukweli wowote au ni dhana tuu?, wewe kama mbobezi wa sheria na katiba, kauli yako ina nguvu sana katika hoja hii, jee una nini la kusema as an authority kwenye sheria na katiba?" .

Prof. Shivji kwanza alinyamaza kama anawaza kitu huku akinitazama tuu as if anajiuliza ajibu au asijibu....kisha akanyoosha mikono yake miwili na kupunga ishara ya kukataa kuwa hataki kusema kitu huku akitingisha kichwa ishara ya kukataa!.

Mimi sikuridhika na jibu lile, nikamuomba basi japo anieleze tuu "off the record " na sitaripoti na sitaandika chochote kuhusu atakachoniambia kama huu udikiteta Tanzania upo kweli na kama ni kweli kwenye udikiteta huo pia kuna ukiukwaji wowote wa katiba au ni dhana tuu?!.

Prof. Shivji aliirudia tena ishara ile ile bila kutamka neno lolote!.

Nilipoona hivyo, mimi kama mwandishi mkongwe, nilimwelewa Prof. Shivji na kukitafsiri vyema kimya chake.

Sisi waandishi tunatakiwa kuwa very assertive na persistent, yaani unakuwa king'ang'anizi kulazimisha majibu and not to give in kirahisi rahisi, lakini hapa kwa Prof. Shivji, mara moja nilimuelewa na nili give in kirahisi kabisa! .

Mtu anapokataa kwa ushara kujibu swali, anamaanisha hataki kabisa kuwa quotated hata neno moja ili usije ukam miss quote!.

Unapouliza swali na kutojibiwa kuna ukimya wa aina tatu.

1. Ukimya wa Kutojua. Huu ni ukimya ambao yule aliyemuuliza hajui chochote kuhusu unachouliza hivyo ili kuepuka kujibu kitu ambacho sicho na kulinda heshima yake kwa kutokusema hajui, anaamua kunyamaza bila kujibu chochote.

2. Ukimya wa pili ni pale unapouliza swali gumu linalotaka jibu la uhakika, na jibu unalo ila ungependa kujiridhisha kwanza to be sure, hivyo unamua kunyamaza ili usije kujibu kitu halafu kikatsfsiriwa vibaya, hivyo unaamua kunyamaza kimya.

3. Ukimya wa tatu ni ule ambao unaulizwa swali, jibu la uhakika unalo ila kwa sababu fulani (ambayo naijua), anaamua usijibu chochote ili usije kuwa mis quoted kwa sababu hiyo!. Huu ndio ukimya wa Prof. Shivji.

Kwa wale tuoamfahamu Prof. Shivji alivyo bold kwenye issues za utetezi wa katiba, kama ni kweli Tanzania kuna udikiteta na katiba imekiukwa, watu wote Tanzania nzima wanaweza wasilizungumzie hili lakini sio Prof Issa Shivji! , sasa kama tumefika mahali hadi Prof. Shivji hawezi kuzungumza, au ameepuka kulizungumzia hili, then, tukubali tukatea, nyakati sasa zimebadilika! .

Jee unaweza kuhisi ni nini kilichomfanya gwiji huyu wa Sheria na Katiba, Prof. Shivji asijibu chochote kuhusu hoja ya udikiteta na uvunjifu wa katiba nchini Tanzania unaodaiwa kufanywa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye amekula kiapo cha kuilinda hiyo Katiba?!.

And by the, huu udikiteta unaolalamikiwa upo kweli au ni dhana tuu? ,na kwenye udikiteta huo jee ni kweli katiba imekiukwa au ni watu tuu wasiojua katiba ndio wanaopiga kelele za kukiukwa kwa katiba lakini mabingwa wa katiba wamenyamaza kimya kwa sababu katiba haijavunjwa? !.
Pasco
Alijua akijibu lolote lazima utaandika na kuongeza na yako pia. Prof. is very smart he didn't buy the idea of confidentiality you assured him. All in all hayo maswali unayotuuliza sisi kwa nini wewe usiyajibu kwanza kwa jinsi uonavyo wewe? Maana wewe unauliza maswali kwa kuhisi tu tuambie we unaamini nini tutakujibu kama upo sawa au umekosea. The word dictator is a relative term and very wide people can perceive differently and argue for or against, so tell us your preception we will tell you our preception.
 
Wala usiseme rangi bali hata kimakaratasi Mzee issa Shivji (PhD) ni Mtanzani zaidi ya Watanzania wenye asili ya kiafrika wengi tu pmj na huyo anayemuita Muhindi, kwa maana ukisema atoe ushahidi wa Utanzania wake atakutolea Cheti chake cha kuzaliwa na cha familia yake yote, sasa muulize huyo anayemuita Muhindi athibisthishe Utanzania wake wa vizazi viwili tu kwa documents kama ataweza, zaidi ya kukwambia nimezaliwa kijiji fulani kamuulize babu fulani anatujua!
Wewe mwenye kama Prof Shivji angejibu tofauti na unavyotamani angejibu, ungekuwa wa kwanza kuandika hapa kuwa Shivji sio raia na atimuliwe haraka.........!
 
Bw.Pasco
Hukupata nafasi ya kumuhoji Professor Tundu Lissu upatae mawazo yake?
Mkuu Lanca, Tundu ndio mwanzilishi wa dhana ya udikiteta uchwara, ukimhoji Lisu unakuwa umempa leading questions kama vile kuuliza majibu badala ya kuuliza maswali. Lisu ni partisan kwenye active politics japo ni mwanasheria by professional lakini huwezi kumuuliza swali la kisheria ukategemea an objective answer! . Hawezi kuwa objective kwa sababu objectivity yake ameisha I compromise kwenye politics, Prof Issa Shivji is and has never been a politician hivyo bado ni very reliable professional you can rely on getting honest opinions.
Pasco
 
Shida watu hawaelewi pia kukaa kimya nalo ni jibu,shivji ana Busara sana siyo mpayukaji kama hao mnaowasifia,,tatizo la vijana wq Leo tumezoeshwa MTU sahihi ni Yule mwenye domo pana anaongea popote,,,naomba tumpe heshima yake mzee shivji,katumia Busara kukaa kimya,muda wa kuzungumza ukifika anaongea,ndo kwanza hata mwaka bado,
Prof Shivji hawezi kuongea tena hususani mambo mazito ya Kitaifa yanayoweza kutoa mwelekeo fulani, naomba turejee toka swala la katiba mpya maarufu kama katiba ya Warioba lilivyoanza na changamoto zake hajaonekana kuwa ni yule Prof Shivji tunayemjua au tuliyemzoea ktk mambo mazito ya Kitaifa!.
 
Pasco et al., rejea:

Issa Shivji ‏@IssaShivji Sep 23
"I'm tired at the hypocrisy,the stupidity,&the brutality of the authorities&of our submissiveness,pliancy, evasiveness" Marx agst censorship

Issa Shivji ‏@IssaShivji Sep 17

State control through the Board of both journalists and media should be scrutinized carefully b4 celebrating.

Issa Shivji ‏@IssaShivji Sep 12
A thought provoking EID gift. I just uploaded 'Good governance' by Mwalimu Nyerere to @academia!

Issa Shivji ‏@IssaShivji Sep 12

And which country has leaders with a moral conscience?

Issa Shivji ‏@IssaShivji Sep 8

Sawa.Hakuna sk itakayotawala kwa niaba yao kama wannchi wakikosa vyombo na njia mbalimbali kushiriki ktk utawala wao

Issa Shivji ‏@IssaShivji Aug 30

No, not mellowed down. Power is incestuous. Power mates with power to reproduce power.

CHANZO: Tweets avec des réponses de Issa Shivji (@IssaShivji) | Twitter
ukita kuamini kuongea kuna nguvu, nitajie mademu wangap uliwapa kwa barua na madem wangpi uliwapta kwa kuongea..........tafakri
 
Mkuu Lanca, Tundu ndio mwanzilishi wa dhana ya udikiteta uchwara, ukimhoji Lisu unakuwa umempa leading questions kama vile kuuliza majibu badala ya kuuliza maswali. Lisu ni partisan kwenye active politics japo ni mwanasheria by professional lakini huwezi kumuuliza swali la kisheria ukategemea an objective answer! . Hawezi kuwa objective kwa sababu objectivity yake ameisha I compromise kwenye politics, Prof Issa Shivji is and has never been a politician hivyo bado ni very reliable professional you can rely on getting honest opinions.
Pasco
Asante mkuu
 
Alijua akijibu lolote lazima utaandika na kuongeza na yako pia. Prof. is very smart he didn't buy the idea of confidentiality you assured him. All in all hayo maswali unayotuuliza sisi kwa nini wewe usiyajibu kwanza kwa jinsi uonavyo wewe? Maana wewe unauliza maswali kwa kuhisi tu tuambie we unaamini nini tutakujibu kama upo sawa au umekosea. The word dictator is a relative term and very wide people can perceive differently and argue for or against, so tell us your preception we will tell you our preception.
Mkuu Higgi, kwanza naunga mkono hoja, Prof. Shivji ni very smart kukataa kujibu, ila pia ni kweli nilipouliza hilo swali kuna jibu fulani nilikuwa nalitegemea.

Tukirudi kwenye maoni yangu, sisi waandishi tutakuwa na double personality ambapo tunakuwa tukifanya kazi ya unandishi kwa weledi, utu wetu na personality zetu zote tunaziacha nyumbani, hivyo unatekeleza majukumu ya kwa kuenenda by the books and by the rules, kwa sababu hatupaswi kujumuisha our opinions. Yaani "news men are not part of the news story", hivyo siruhusiwi kuweka mawazo yangu kwenye news peaces.

Hata ukipewa tip au unajua kabisa for sure kuwa Tanzania tuna udikiteta, mimi kama mwandishi sipaswi kuandika hivyo bali natakiwa kumtafuta mtu authority kulisema hicho nilichosikia au ninachokijua.

Nakubaliana na wewe hoja ya udikiteta ni relative na inafuata principles za relativity lakini tuhuma za ukiukwaji wa Katiba ni very serious allegations hivyo hapa we have to go by the books, rules must always be obeyed! . Haiwezekani katiba ikakiukwa halafu tuna mabingwa wa katiba wamekaa kimya!. Hali hii sio bure! .

Kupata maoni yangu binafsi kuhusu dhana hii ya udikiteta, just click "udikiteta, pasco, jamiiforums " utanipata.
Pasco
 
yni na hyu jamaa jna kaongea pumba......tanzania....KUPATWA KWA MAPROFESA TANZANIA
 

Attachments

  • 14479734_211368299282321_2317720343219269278_n.jpg
    14479734_211368299282321_2317720343219269278_n.jpg
    11.1 KB · Views: 56
Mkuu Pangolin, heshima ni kitu cha bure, ila kama wewe ni mfuatiliaji wa mambo ya sheria na katiba, unaweza kuthubutu kumlinganisha Prof. Shivji na Lisu na Kibatala?!, tutake radhi! .

Hii kauli "kibabu cha Kihindi " ni kauli ya kibaguzi na ya udhalilishaji! .

Pasco
Shukran sana kwa kumchanganulia huyo nilitaka nimwambie kma wewe but shukran kwa kuwasilisha
 
Gwiji la sheria ni Tundu lissu na wakina kibatala tuu hao wengine wachumia tumbo kama hichi kibabu cha kihindi ndio hatari kabisa
Wee temea mate chini!! Tundu Lissu ni kama kanjanja tu wa sheria ukimlinganisha na gwiji Issa Shivji!!! ndio maana Shivji ni Professa mbobezi wa sheria ya katiba!
 
Back
Top Bottom