Gwajima wa kanisa la Ufufuo na ving'ora barabarani

Jamani kwani Gwajima ana jeshi la polisi? ebu msilete za kuleta hapa. Mnamlaumu Gwajima kana kwamba aliamrisha aje apokelewe airport na kupewa escort ya police. Shida mnakurupuka tu bila kujua ilikuwaje. Na mkitaka details kwa nini Gwajima alipewa escort si mkamwone IGP Mwema au kamanda Kova.

Hakuna mtu anayeweza kujiamulia tu kuwa police wampe escort. Kama jambo hili halijawafurahisha basi msimlaumu Gwajima. Yeye alikuwa Japan akihubiri injili, karudi kafika airport kakuta washirika wake (watoto wake wa kiroho) wamekuja kumpokea. Sasa ni kipi kinachowakera? Hebu leteni mada za maana hapa na si mambo ya majungu yasiyo na maana. Tabia za udaku usio na maana hautusaidii chochote.

Na kwa taarifa yenu bado muda kidogo sana Gwajima atakuwa anatembea na escort ya police kama mwana wa mfalme. Mbona Yesu siku moja aliingia Yerusalemu akiwa juu ya mwanapunda na tena mwanapunda akatandikiwa kanga (kwa mara ya kwanza). Gwajima ni mtumishi wa Mungu na anastahili heshima yake. Maandiko yanasema mtu akimtumikia Mungu, Mungu atamweshimu. Na sasa kam Mungu anamweshimu wewe ni nani umdharau.

Hongera sana IGP Mwema kwa kumpa huyu mtumishi wa Mungu escort ili awahi kufika kanisani ambako maelefu ya washirika walikuwa wanamsubiri. Keep it up and God bless you.
 
Siku hizi wahubiri wengi wanafanya biashara na waumini, Wanauza injili kwa sadaka. Wanawakamua kondoo (washirika) bila aibu. Hata Benny Hinn ana kashfa kubwa ya kuwa nabii wa uongo. Kwa maoni yangu, watu wasome maandiko yanavyosema na kuyafuata na sio kuwafuata wahubiri matapeli. Ni maoni tu.

We Sabra acha kuongea mambo usiyoyajua. Unawafahamu wahubiri wangapi wanaofanya biashara na washirika? Ni wajibu wa washirika kutoa sadaka na hili ni agizo la Mungu. We unafikiri watumishi wa Mungu hawahitaji pesa za kujikimu wao na familia zao. Mnajitafutia laana za bure kufanya generalization zisizo na ukweli wala maana yeyote. Kazi ya Mungu ili iende mbele LAZIMA washirika watoe pesa zao kama sadaka. Na mimi nashangaa sana watu wanaolalamika kuwa washirika wanakamuliwa wala sio washirika wa kanisa lolote ni watu wa vijiweni tu. Hata kama ni kweli washirika wanakamuliwa wewe kinakuuma nini kama pesa si za kwako. Unajifanya una huruma sana. Je hao wanaokamuliwa wao hawaoni kama wanakamuliwa mpaka waendelee kukubali kukamuliwa. Usiwafanye watu wanaotoa pesa zao kwa kazi ya Mungu kuwa hawana akili. They know what they are doing and you can stop them by your malicious words.
 
ni kitu kibaya sana kuongea jambo usilolijuwa kwa kujifanya unalijua sana, unakuwa unampaka mtu matope pasipo hata na sababu. kitu cha muhimu kuelewa ni kwamba, ukimgusa mtumishi wa Mungu kama ninyi wengine mnavyofanya hivi, unagusa mboni ya jicho la Mungu...ni rehema za Mungu tu lakini Mungu anachukia mnachofanya......Mungu awasaidie.
 
wafuasi wa ibilisi huwa hawapendi maendeleo ya mtumishi wa Mungu maana INJILI kama kawaida ni moto
kwa watoto na wana wa pepo, sasa shetani ameuvaa mwili na kuanza kazi lasimi, lakini wapiganaji wa neno hatuko nyuma kuhakikisha tunapiga majeshi mpaka shetani na vimalaika vyake vikome, kazi ya Mungu haitosimama kwa sababu ya nani kasema nini, ama yupi kafanya nini
 
Kama kweli mhubiri huyo alipewa escort ya Polisi na vin'gora ili kumuwahisha tu anakokwenda basi kuna mushkeli katika jeshi la Polisi. Na hii haina uhusiano kabisa na hoja ya kwamba ni mtumishi wa Mungu. Huko nako ni kwingine kabisa; labda ianzishwe thread yake nyingine. Kama itabidi wahubiri wote wapatiwe huduma ya aina hiyo basi huo mtafaruku katika barabara zetu sijui utakuwaje. Anayefahamu kadhia ya ma-VIP wa Lagos na Abuja na ving'ora barabarani anaweza kuipata picha kidogo. Sidhani kama sisi tunataka kuwa namna hiyo. Aidha, ni dalili ya kukwama kimaendeleo.
 
wafuasi wa ibilisi huwa hawapendi maendeleo ya mtumishi wa Mungu maana INJILI kama kawaida ni moto
kwa watoto na wana wa pepo, sasa shetani ameuvaa mwili na kuanza kazi lasimi, lakini wapiganaji wa neno hatuko nyuma kuhakikisha tunapiga majeshi mpaka shetani na vimalaika vyake vikome, kazi ya Mungu haitosimama kwa sababu ya nani kasema nini, ama yupi kafanya nini

Utukufu. Nadhani wewe ni shepherd au potential shepherd. Hahahahaaaaaaa. Piga majeshi na usonge mbele.
 
Kikolo Anyisile,kulalamikia ving'ora sio ushetani ,bali mimi nafikiri ufahari anaonyesha huyo mchungaji ,sijui mfufuaji ndio ushetani,kwa kutaka yeye tu ndie apite kwanza barabarani na wengine wakae pembeni huo ni ubinafsi na ubinafsi ni dhambi ,angekuwa ni kiongozi wa kiserikali isingekuwa nongwa kwa maana naamini analindwa na sheria na utaratibu wa nchi .Ndugu zanguni tusipofushwa na manabii wa uongo na tusitumie dini kuwaona wengine ni outcast!
 
watu wanahangaika kupigana na watumishi wa Mungu...hawajui kama hao ndo wanawaweka mjini kwa maombi hadi tunapata amani ya kuweza kufanya kazi zetu bila matatizo...wakinyamaza kimya hao tz hapa patakuwa pamoto.
 
Utukufu. Nadhani wewe ni shepherd au potential shepherd. Hahahahaaaaaaa. Piga majeshi na usonge mbele.

umenikumbusha mbali na huu usemi wa "utukufu" bila shaka anyisile ni more than a sherphard au potential sherphad....nimesikia mmehamia kawe, nikirudi tu bongo nitashinda church mwezi mzima nipigwe msasa wa Bible school, nimemiss hakika mashambulizi niliyokuwa nayafanya.....

Piga majeshi..hahaha, majeshi majeshiiii, Majeshi ya Bwana, wamepigwa wamepigwaaaaaaaaaa, wamekoma kabisaaaa...

wameshindwa vita vya rohoni, wamehamia vita vya mwilini,ukiona adui anaanza kuonekana kupiga vita vya mwilini, ujue alishashindwa muda mrefu kwenye vita vya rohoni na hapo imebaki tu udhihirisho kimwili wa adui kuaibishwa na kusurrender kabisa...Tanzania nzima imetekwa kwa nguvu ya Jina la Yesu, wachawi waganga, washirikina wasoma nyota, wakuu wa anga, wakuu wa giza falme na mamlaka za nchi mkoa wilaya hadi kijiji zinahangaika...ukombozi wa wengi umekaribia, na siku ya kuaibishwa kwa shetani na wafuasi wake imewadia....
 
Jani Jioni nilikutana na hiki kipindi katika luninga ya SIBUKA, ' Saa ya ufufuo na uzima' cha Pastor Josephat Gwajima [http://www.ufufuonauzimaministries.org/]. Suala lililonishangaza ni ulinzi aliyokuwa akipewa na walinzi wake waliovalia kama walinzi wa maraisi (walkie talkie radio et cetera). Je hawa 'wachungaji' wa kileo hawana imani na mazingira yao ya kazi? Naomba kueleweshwa katika hili.
 
Biblia inatueleza kuwa amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye kuwa ngao na kinga ya maisha yake.
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
Bwana asipoulinda mji waulindao wakesha bure.
 
Biblia inatueleza kuwa amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye kuwa ngao na kinga ya maisha yake.
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
Bwana asipoulinda mji waulindao wakesha bure.

Wala usishangae, haya yote Yesu aliyasema, ni dalili za mwisho wa nyakati. People have turned Jesus to big profitable businesses.
 
Wala usishangae, haya yote Yesu aliyasema, ni dalili za mwisho wa nyakati. People have turned Jesus to big profitable businesses.

Kweli tena, nilishangaa sana jamaa kama 'presidaa' na jamaa wanaonekana wamebeba 'miguu ya kuku'
 
Buji jamani duh!mbn wknd yangu inaanza kwa mibaraka?ubarikiwe sana uncle chelulute
Biblia inatueleza kuwa amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye kuwa ngao na kinga ya maisha yake.
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
Bwana asipoulinda mji waulindao wakesha bure.
 
Muache alindwe,yule mchungaji anamtegemea Mungu sana ukisikiliza mahubiri yake utajua hivyo.Ana vita yake anayopigana na Ibilisi,watabiri na wanasiasa anaowapinga kila siku........usisahau pia ana Hummer yake .....lol na mara nyingi watu ni wengi wanaotaka kumuona wale walinzi ni wakuweka taratibu tu za kuonana nae na kuhakikisha yu salama na anatupiga injili kama kawaida as well as kutoa mapepo yanayotutesa.Basi we usiweke geti kwa kuwa Mungu atakulinda kwako???wala kule benki ulikoweka hela zako,ziombee tu lakini kusiwe na ulinzi?????
 
Kwani ni mchungaji yupi halindwi?.Kuna mambo ya rohoni,hufanywa kiroho,kuna mambo ya mwilini hufanywa kimwili.Paroko huwa na timu ya vijana kama wawili au wanne,mchungaji wa kilutheri huwa na wazee wa kanisa,hawa ndio walinzi.Kwa upande wa mchungaji Gwajima ni kutokana na huduma yake,anapambana na wazito waliochukua wenzao misukule,wengi wao ni vingozi wa siasa na wafanyabiashara.Hivyo kupewa ulinzi kama raisi ni sawa.Kwanini raisi alindwe?Hali kadhalika kiongozi yeyote anapaswa kuwa na ulinzi.Wala sio kusema amtumainie mwanadamu....hiyo sio sahihi.Ni haki yake kupewa ulinzi.
 
Uinzi dhidi ya nani?
Rais analindwa kwa sababu ana mabaya anayoyafanya kwa watu wake...huyu mchungaji kafanya mabaya gani kwa waumini wake?
 
jamani mambo ya rohoni ni ya rohoni na mambo ya mwilini yanaenda kimwili kama ww si mchungaji uwezikujua vita ya wachungaji binafsi sioni kosa kwa mtumishi wa mungu kulindwa kwani nimeona watu wenye mapepo wakiwavamia watumishi wengine wanatumwa kwakweli ulinzi ni lazima
 
Back
Top Bottom