GTV: Ndio tumekula hasara au?

hivi siwezi kutumia the same facilities (dish n receiver) kupunguza costs za kuunganisha DSTV? utapeli huu

Sidhani kama itawezekana kwa receiver ya GTV kutumika kwa DSTV...Kimsing imekula kwako mkulu,ingia tu gharama upya kuunganisha DSTV
 
Tuko wengi. Mimi niliitelekeza DSTV kwa sababu ya bei zao kubwa. Kumbe vitu rahisi mara nyingi ni ghali sana! Naikumbuka Greenland Bank, Meridian Bank,...
TCRA mtatusaidiaje? Kuna Advocate yeyote yuko tayari kulisimamia hili?

Mhh Mkuu,

Nadhani advocate wa kwanza ni wewe mwenyewe. Kwanza angalia mkataba uliotia saini unaseamje. Je,kuna kipengele cha kukusaidia kupata fidia andapo GTV watavunja mkataba? Kama hakipo, hapo sina hakika endapo una pa kukimbilia. Lakini kwa kuwa waliopata hasara ni wengi, basi kwa kutumia nguvu ya umma labda mnaweza kujaribu kunusuru angalau vijisenti kidogo!
 
Wanajamii,
Mimi nina ushauri ambao labda utasaidia. Kampuni kisheria ina "utu", hivyo hata ikifilisika bado mnaweza kuidai. Kwa standards za kihasibu, unapolipa pesa GTV hawatakiwi kurecognize income mpaka utakapotumia huduma zao kwa muda ulionunua. Hivyo wewe kwenye vitabu vyao unaonekana kama creditor mpaka utakapotumia huduma yao kwa muda ulionunua.

For that case, wale waliolipia wanaweza kurecover part of the money paid, although cost/benefit analysis ya kufuatilia inatakiwa ifanyike.Isiwe mtu anadai 20,000/= akatumia more than 20,000/= kupata pesa yake.

Kampuni ikitangaza kufilisika,huwa anateuliwa mfilisi ambaye anakusanya mali na madeni yote ya kampuni husika. Baada ya hapo,anafungua daftari la wanaoidai kampuni(creditors), so you can use that chance to register yourself so that you can recover your money.

Kuhusu receiver na satelite dish,sijajua contract inasemaje. Kama ulinunua moja kwa moja then itakuwa ngumu kurecover,labda tupate ushauri zaidi kwa wanasheria waliopo ndani ya JF.
Tunaomba lawyers na Accountants waliopo humu ndani watusaidie kwa hili kiushauri.
 
Mimi nafikiri ipo haja ya Mammlaka ya TCRA kuwa na muundo kama wa BOT kwa wanaowekeza kwenye Mabenki ambayo sharti lake wawe na 5billion, sambamba na hii mamlaka ya TCRA waweke masharti kwa wanaotaka kuwekeza kwenye biashara ya TV wawekewe kima cha pesa kama deposit ili wakifilisika watu ambao wanawadai waweze kulipwa. Hivi sasa sina uhakika kama hawa watu wapo nchini kwani ofisi zimefungwa muda mrefu wamewaachia watu decorders na ma dish ambayo hayana kazi ni hasara kwa kweli.
 
ndugu zangu,


sasa zile mechi mechi za mpira za madaraja kule UK du! ITAKUWAJE hivi DSTV hawawezi kufanya mpango jamani mbona tumeumia.
 
kweli bure ya ghali
Wakunyuti,

Sidhani kama ilikuwa bure.

Serikali inatakiwa kutoa tamko nadhani. Hii ni mbaya sana kwa watanzania walio wengi nahisi imewaathiri wote wapenzi wa soka la Uingereza.

Hawa jamaa waliingia kwa mkwara mzito sana na wakapewa leseni ya kuonesha nasikia 80% ya mechi za ligi kuu ya Uingereza.

Nami ni muathirika mmojawapo wa hawa jamaa. Nilikuwa na tabia ya kulipia miezi 3 kwa mkupuo na nilikuwa nimelipia mpaka March mwaka huu.

Ninachoamini ni kuwa serikali inaweza kuhakikisha watanzania wote waliokuwa wamelipa wanarejeshewa pesa zao (zaidi ya Januari) na ikiwezekana na gharama za usumbufu.

Binafsi siamini kama njia waliyoitumia ya kukata ghafla (ndani ya siku mbili tu bila kuwaeleza wateja wao hatma yao) ni njia sahihi.

Watanzania, ni wakati wa kutofumbia macho wizi wa namna hii.

Nafurahi kuwa DSTV wanaendelea kunipa huduma nzuri japo mechi wanaonyesha chache na nafaidi UEFA tu kwao. Hawa GTV nasikia walikuwa na mpango wa kuchukua hata leseni ya UEFA, nadhani wangetuumiza zaidi ya hivi.

DSTV nao wapunguze gharama, $75 kila mwezi ni wachache tunaoweza kumudu ilhali wanaibadilisha kwa Tshs 1,450/=.

Inasikitisha lakini ndiyo hali halisi. Nini kinafuatia? Au ndio tuamini kuwa Tanzania ni shamba la bibi? Wamekuja wamechuma na wanaondoka kiulaini tu?
 
Max
Siamini kabisa kama hawa jamaa wamepata hasara,jamaa wamechuma hela wakafanya analysis wakaona huko mbele watapata hasara wakatafuta kisingizio cha "Global Financial Crisis" ili watu wasipige kelele but ukweli jamaa wametuibia
 
DSTV wapunguze bei watakusanya wale wateja wote wa G Sport
 
DSTV kwa sasa bei zao za installation zilikuwa chini kuliko GTV. Kuna offer walitoa last year na nadhani hawajapandisha bei mpaka sasa. Gharama kwa upande wa DSTV ni kwenye hizi monthly charges. Gharama ziko juu, na kibaya zaidi wanacharge kwa USD.
 
DSTV kwa sasa bei zao za installation zilikuwa chini kuliko GTV. Kuna offer walitoa last year na nadhani hawajapandisha bei mpaka sasa. Gharama kwa upande wa DSTV ni kwenye hizi monthly charges. Gharama ziko juu, na kibaya zaidi wanacharge kwa USD.

mkuu unaweza ukanipa amount (bei) ya kuinstall?
 
Max
Siamini kabisa kama hawa jamaa wamepata hasara,jamaa wamechuma hela wakafanya analysis wakaona huko mbele watapata hasara wakatafuta kisingizio cha "Global Financial Crisis" ili watu wasipige kelele but ukweli jamaa wametuibia

Nakubaliana na wewe na ndiyo taaluma ya biashara inavyotakiwa usisubiri ufe kifo cah mende bora nusu shari. Hii ndiyo press release iliyokuwepo kwenye wesite yao:

LONDON – 30 January 2009

Gateway Broadcast Services announced today that its Board of Directors has unanimously approved a plan to liquidate the Company.

The current financial and global crisis has severely interrupted the company’s ability to secure further funding for the continued operation of the business.

The company has worked extensively with external advisors and all internal resources to investigate, evaluate and analyze strategic alternatives for the Company to further continue to operate. In determining to approve the Company's plan of Liquidation, the board and management carefully reviewed the advice and findings.

Gateway Broadcast Services, suppliers of the GTV service to subscribers across Africa has over the last 2 years invested a total of US$200 million and created jobs and competition in the 22 markets. The economic crisis that has emerged globally over the last few months has caused excessive demands on the business.

With immediate effect the service will be withdrawn.

“Increased instability in global markets interrupted our ability to secure funding on an acceptable timescale and have left us no choice but to cease operations,” said a company spokesman.

“We realise the negative impact this has had on our loyal customers, creditors and staff, all of who have believed in GTV and the revolution in pay TV it had created. We have tried every possible step to keep the company going but we are all the unfortunate victims of the current global economic crisis.”

Thank you.
 
Tuko wengi. Mimi niliitelekeza DSTV kwa sababu ya bei zao kubwa. Kumbe vitu rahisi mara nyingi ni ghali sana! Naikumbuka Greenland Bank, Meridian Bank,...
TCRA mtatusaidiaje? Kuna Advocate yeyote yuko tayari kulisimamia hili?
...Mwanangu usinikumbushe mambo ya Greenland bank wamezama na mapene yangu wale!! Na huwezi kuamini hata mimi nilipanga nikipata kaji-salary kangu end of January nijiunge huko GTV...salama yangu nilipata safari ya kikazi Ntwara huko nadhani ndicho kilichoniponyesha.
 
Serikali yaibana GTV

na Mobini Sarya
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

SERIKALI imeitaka Kampuni ya GTV, iliyokuwa ikihusika na huduma ya ving'amuzi nchini, kwamba hadi kufikia leo saa 4 asubuhi iwe imewasilisha taarifa ya namna itakavyorejesha gharama kwa wateja wake.

Hatua hiyo ya serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imekuja siku tatu baada ya GTV kufunga ofisi zake nchini kutokana na kuathiriwa na mtikisiko wa kuporomoka kwa uchumi wa dunia hususan kwa nchi za Marekani na Ulaya.

Akizungumza kwa njia ya simu jijini Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano wa TCRA, Mungi Innocent, alisema wameitaka GTV kutekeleza sharti hilo leo.

Alisema, GTV tayari imejulishwa kuhusu hatua hiyo ya serikali kupitia kikao baina yake na Kampuni hiyo tanzu ya GTV Tanzania Ltd, inayomilikiwa kwa asilimia 50 na Mtanzania.

"Tumeitaka GTV watuletee taarifa za wateja wao zinazoonyesha hali halisi za wateja wao zilivyokuwa kabla ya kufunga huduma zao ili TCRA iweze kuhakikisha wateja hao wanalipwa haki zao mapema," alisema Innocent.


Aidha, TCRA imesema imesikitishwa na hatua ya GTV kufunga huduma zake katika nchi mbalimbali duniani kutokana na mtikisiko wa uchumi na kuitaka iwasilishe haraka taarifa zake namna itakavyowarudishia gharama wateja wake wa hapa nchini.

Alisema, GTV wanatakiwa kuwasilisha taarifa hizo kufikia leo saa nne asubuhi, vinginevyo watachukuliwa hatua kwa sababu wana uhakika kwamba, ni kampuni inayomilikiwa na Mtanzania.

Jumamosi iliyopita, kampuni ya GTV ilifunga ofisi zake kutokana na mgogoro wa fedha uliozikumba taasisi nyingi za fedha na makampuni kadhaa hususan Marekani na Ulaya.

Hatua ya serikali ni faraja kubwa kwa wateja mbalimbali wa kampuni hiyo ambao tangu GTV ifunge huduma zake, wamekuwa wakipiga simu kuklalamikia hali iliyojitokeza.

Kikubwa kinacholalamikiwa na wateja hao, ni hatua ya GTV kuendelea kupokea malipo kupitia kwa mawakala wao hadi siku Kampuni hiyo ilifunga ofisi, Jumamosi.


Kati ya waathirika wakubwa na kufungwa kwa GTV, ni Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ambalo lilikuwa na mkataba wa miaka mitano na nusu kuanzia Desemba 2007, wenye thamani ya dola mil 3.5 za Marekani.

Kiasi hicho kilijumuisha fedha taslimu za maandalizi na nauli kwa timu 12.

Aidha, GTV ni mdhamini aliyekuwa akitoa zawadi ya fedha taslimu kwa timu zote kuanzia bingwa hadi timu ya mwisho, hivyo kuongeza ushindani.
 
Sawa sawa, hii inaitwa Kula Uliwe, Wawarudishe wateja haki yao sio kuondoka kinyeji hivyo.
 
- very trick eeh!

- mkataba kati ya GTV-TZ na mteja umekaaje?

- TCRA ina nguvu kiasi gani kuilazimisha GTV-TZ kurudisha PESA za wateja?

- remember GreenLand Bank? need I say more?
 
Nauliza hivi? lile liungo na decoder(sijui kama inaandikwa hivi) litakuwa na kazi gani tena? unaweza ukanunua receiver uakalitumia kwa kutumia ule ungo? au kwa ufupi unaweza kutumia kwa njia nyingine? je kama halina kazi tena unawza ukarudisha na wakakulipa hela zako?
 
TCRA imekumbuka shuka wakati kushakucha kama mtu/kampuni imefilisika italipaje liabilities wakati sababu ya kufilisika ni kukosa uwezo wa kulipa. Sasa unamwambie alipe atalipa kutoka wapi, kama regulatory authority iko aggressive walitakiwa kuona kabla. Saa nne ndio hii uone kama kweli TCRA wana meno yeyote ya kung'ata mtu.

Ilishawahi kutokea BOT waliingia mkenge wa Meridian Biao Bank lakini waliokoa watu na kuzama kwa Greenland Bank miaka ya tisini. Vinginevyo ya GTV imekula kwetu decoder na dish tuwapatie watoto wachezee.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom