Green star express t428blr latelekeza abiria njiani karibu na puma!

mwanamapinduko

Senior Member
Jan 24, 2011
178
41
Kuna jamaa yangu anaenda Mwanza kanipigia wametelekezwa kwenye basi hilo liloharibika huko nje ya mji wa Singida. Kondakta na dereva wamekimbia singida mjini. Wamejaribu kuomba msaada polisi bila mafanikio.
 
Kwa route ya dar to mza haya mabasi ya greenstar nimoja ya mabus bora pamoja na lucystar na murro sasa kama ni hivyo greenstar watakua wamejimaliza.
 
Kwa route ya dar to mza haya mabasi ya greenstar nimoja ya mabus bora pamoja na lucystar na murro sasa kama ni hivyo greenstar watakua wamejimaliza.

Acha uwongo, route ya Mwanza Dar gari ya uhakika ni ALLY'S SPORTS
 
Kwa route ya dar to mza haya mabasi ya greenstar nimoja ya mabus bora pamoja na lucystar na murro sasa kama ni hivyo greenstar watakua wamejimaliza.

Hayo magari ni balaa kwa kulaza watu njian, nilishalazwa manyon. Hapo wanasubiri fund atoke dar. Kama n mmoja wa abiria we nenda singida 2
 
Kwa route ya dar to mza haya mabasi ya greenstar nimoja ya mabus bora pamoja na lucystar na murro sasa kama ni hivyo greenstar watakua wamejimaliza.

lucky star hamna kitu siku hizi lazima iwe na fundi, naona itakuwa imebaki Muro njia hiyo.
 
Green star ni basi zuri sana. Tatizo nadhani ni tajiri na management. Wahudumu wake wana lugha chafu sana sijawahi ona. Kuna siku nilikuwa natoka nalo Kahama kwenda Dar, bahati mbaya pale Nzega Tumbo likaniuma. Nilimwomba Konda akaniambia subiri mpaka Igunga. Pale Igunga pamoja na mimi wakashuka wengi kujisaidia. Lakini kabla ya abiria wa mwisho kushuka konda akaanza kupiga horn. Niliporudi kwenye basi nikakuta mazungumzo kati ya driver (mwarabu) na mpiga debe. Mpiga debe akamwambia driver kuwa watu wanaumwa, subiri kwanza wajisaidie,,, driver akajibu hapa siyo hospitali mimi nitawaacha! Niliishiwa nguvu kabisa.

Tangu hapo sijagusa Green Star, hata iwe kwa shida. Nakushauri usipande hilo basi hata kidogo
 
Kweli mkuu unavyosema tarehe 19/11/2011 nilishuhudia mtoto akikojoa ndani ya gari kwa sababu mama aliwaambia makondo na dereva wakakataa kusimama. Gari ya Kahama- Dar Green Star Express.
 
Green star ni basi zuri sana. Tatizo nadhani ni tajiri na management. Wahudumu wake wana lugha chafu sana sijawahi ona. Kuna siku nilikuwa natoka nalo Kahama kwenda Dar, bahati mbaya pale Nzega Tumbo likaniuma. Nilimwomba Konda akaniambia subiri mpaka Igunga. Pale Igunga pamoja na mimi wakashuka wengi kujisaidia. Lakini kabla ya abiria wa mwisho kushuka konda akaanza kupiga horn. Niliporudi kwenye basi nikakuta mazungumzo kati ya driver (mwarabu) na mpiga debe. Mpiga debe akamwambia driver kuwa watu wanaumwa, subiri kwanza wajisaidie,,, driver akajibu hapa siyo hospitali mimi nitawaacha! Niliishiwa nguvu kabisa.
Tangu hapo sijagusa Green Star, hata iwe kwa shida. Nakushauri usipande hilo basi hata kidogo
Duuh,jamani mbona kwa route Dar-Mby hawako hivyo?
 
Jamaa amenipigia muda sio mrefu anasema wameingia Mwanza saa saba mchana. Yaani safari ya Dar Mwanza imechukua masaa 31 hrs. Bravo GREEN BUS EXPREES MMEJARIBU MUMESHINDWA MNASONGA NYUMA.
 
Jamani eeh! Green Star ana mabasi kadhaa yanayoenda Mwanza - Dar, kama mmepata bahati mbaya ya kukutana na wahudumu wakorofi haimaanishi Kampuni nzima ni mbovu. Mimi nilipanda Mohammed Trans kwenda Kahama nilijuta kwa jeuri ya wahudumu niliowakuta humo. Lkn siku niliyopanda MZA kuja DAR ningeweza kusema hamna basi lenye huduma bora kama Mohammed Trans. Kwa hiyo tunapopata matatizo ya lugha chafu na makero toka kwa wahudumu tusiishie kunung'unika kwenye JF bali tuchukue hatua.

Na nyie mnaoumwaumwa matumbo safarini punguzeni kula hovyo hovyo. Kama unajua unakwenda safari una haja gani ya kunywa chai nzito as if umeambiwa hutakula tena?! Kama haitoshi njia nzima unabukanya kama fuku fuku na baadae unaanza kutoa hewa chafu kwenye basi kuwakera wenzio.
 
Back
Top Bottom