Great Thinker, Sugua Kichwa kama Unaweza

Mabel

JF-Expert Member
Sep 1, 2010
1,273
678
Uko gerezani umefungwa kifungo kisicho na mwisho, unapewa nafasi moja ya kutoka gerezani iwapo utapita mtihani ulio mbele yako.

Mtihani wenyewewe
.

Unaonywesha milango miwili, kila mlango unamlinzi mmoja, mlango mmoja unaelekea kunyongwa na mlango mwingine unakurudisha uraiani kula maisha na jamaa zako. Hujui mlango upi kati ya miwili unakwenda uraiani na upi utakupeleka kwenye kifo, katika kukusaidia kutambua mlango sahihi wa kuelekea uraiani umepewa nafasi ya kumuuliza mlinzi mmoja wapo kati ya hao wawili swali moja TU ilikutambua ni mlango upi utokee/ufungue na upate kupona.

Katika hao walinzi wawili, mmoja anasema uongo tu na mwingine anasema kweli tu, na hawa wawili wanajuana tabia zao na wewe hujui yupi ni mkweli na yupi ni muongo.

JE,
Utauliza swali gani kwa mlinzi yupi NA utafanya nini ili ujue mlango utakao kupeleka uraiani kufurahia maisha na si kwenda kunyongwa?

Karibuni
 
Nitasimama katkat ya hao walizi wawili then nitauliza: huu mlango wa kwenda kunyongewa? Watajibu wote kwa 7bu kilammoja atadhani nimemuuliza yeye. Nadhani nitapata jibu la ndio na hapana. Yule askari mongo si atakua a vise vesa? nitakua nimepata jibu
 
Hah hah, mkuu umenifurahisha sana. Masharti ni kumuuliza mlinzi mmoja wapo na huwezi kuwauliza kwa pamoja na unapomuuliza huyu mwenzake hajui unamuuliza swali gani.

Umechemka mkuu.
 
aah hili swali linaitaji kalam na karatasi yaani (x+y)x=xy/x-y findi x , given y=8

aagrr
tukupe mji..
 
Mkuu wa mahesabu unatisha na milinganyo yako,

Kama silaha yako pekee ni nyundo, basi kila kitu/tatizo utaona linafanana na msumari!
Haha hah, umechemka kaka.
 
Tupe jibu basi maana siwezi kwenda nyumbani sina jibu, nikipata jibu nikamchemshe na shemeji/wifi yako
 
Ntamuuliza swali la kizushi askari kama "nackia mnanyonga kwa kutumia sumu?" najua askari mwongo atakataa wakat askari mkwel anaweza jibu "sio mimi ninayenyonga" afu bada apo ntajua tuu.
 
Utauliza swali ambalo wote mnajua jibu lake mfano, Je hapa ni gerezani?
kama yule uliyemuuliza atasema ndiyo basi unajua ndiye msema kweli.
Kama atasema hapana basi huyo ndiyo msema uongo.
 
Mkuu sijakuelewa,
Kumbuka unanafasi ya kuuliza swali moja tu ili ujue mlango sahihi wa kutokea, na unamuuliza mlinzi mmoja wapo kati ya wawili pasipo kujua ni mkweli au muongo unayemuuliza.
 
Ntamuuliza swali la kizushi askari kama "nackia mnanyonga kwa kutumia sumu?" najua askari mwongo atakataa wakat askari mkwel anaweza jibu "sio mimi ninayenyonga" afu bada apo ntajua tuu.
Mkuu umenifurahisha,
Sasa kwa swali lako hilo utajuaje utokee mlango upi ambao utakupeleka kupona?
Umechemka mkuu.
 
Utauliza swali ambalo wote mnajua jibu lake mfano, Je hapa ni gerezani?
kama yule uliyemuuliza atasema ndiyo basi unajua ndiye msema kweli.
Kama atasema hapana basi huyo ndiyo msema uongo.
Hili swali litakusaidia vipi kujua mlango wa kutokea?
 
Kwasababu umesema kila mlinzi analinda mlango mmoja na unaruhusiwa kuuliza swali moja, utamchagua yeyote umuulize swali hilo kujua msemakweli ni yupi ili uchangue mlango wa kutokea.

Ila kama mlinzi utakaye muuliza lazima uchague mlango wake basi hilo halitakuwa swali zuri
 
Mkuu unaruhusiwa kumuuliza mlinzi huyu na ukatokea mlango wa mlinzi mwingine. Unaruhusiwa kutokea mlango wowote unaotaka wewe baada ya kuulinza swali moja tu kwa mlinzi yeyote.
 
Sasa jibu langu lina kosa gani? kwasababu walinzi na mfungwa wanajua kuwa pale ni gerezani sasa atakayesema hapana basi huyo atakuwa mwongo na mfungwa atajua mlango wa uraiani ni upi as long as walinzi watakuwa kwenye milango yao.
 
Mkuu umesema hivi
Chamoto said:
Utauliza swali ambalo wote mnajua jibu lake mfano, Je hapa ni gerezani?
kama yule uliyemuuliza atasema ndiyo basi unajua ndiye msema kweli.
Kama atasema hapana basi huyo ndiyo msema uongo.

Sidhani kama hapa utatoka maana wewe unataka kujua muongo yupi na mkweli ni yupi. Lengo ni kudodosa ujue mlango sahihi wa kutokea.
 
Bwana mabel mbona umeanzisha hii topic wakati huu ambao vichwa vimeshachoka na pilika pilika za siku nzima!
Ungeuliza asubuhi hakyanani mimi ningetoa jibu sahihi lakini sasa hivi nipo hoi hapa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom