Grand Theft: Vodacom, Airtel, Tigo, Zantel na Sasatel - Wanachochea ufisadi?

wangekuwa wanalipa kodi zao kiukweli wangepata wapi jeuri ya kugawa magari mia moja na mamilioni kila baada ya muda mfupi, sijui tunaelekea wapi lakini its the right step kushtuka kwanza then tutakuwa na maswali mengi na majibu yatakuja tu...kudos mzee mwanakijiji,

Kwa maswali yako majibu yangu haya;
a. How many phone lines do you currently own? 3
b. What major phone companies do you use? vodacom
c. What would you consider to be your monthly average bills for all the phone services? 300,000
d. How do you afford to pay for all phone services - your phone bill is what percent of your expenditure? -company pays 75% me 25%
e. What percent of your income is the the amount of money you spend on phone services? 14%
f. If you were given an option to have a phone service with an unlimited service for a flat rate for standard services would you continue to have more than one line? no
 
Halafu kitu kingine watanzania hatuna utamaduni wa kuchunguza whether hizi tsh 3 kwa sekunde au 1 tsh kwa sekunde ni kweli
<br />
<br />

Hapa kaka watu wengi huwa hatufatilii kama Tarrifs wanazozitangaza ni kweli, watanzania tumelala ila TCRA ndio imepewa dhamana ya kudeal na tarrifs zote ili watumiaji wa simu tusiibiwe sidhani kama wamejaribu kufanya japo reaserch japo ya kawaida, kilichobaki wanapeana mishahara mikubwa tu.
 
Jambo jingine linaloniuma sana ni hili la zantel kwa upande wa internet katika special tarrifs ya high life, high life gharama yake kwa week ilikuwa shilingi elfu kumi kwa week ili uweze kupata 2gb za high life kuitumia katika moderm ya zantel, jamaa wakaona watu wamenunua line za zantel kwa ajili ya kujiunga then wanaitoa pembeni ikabidi waintroduce inshu ambayo itakufanya uitumie ile line yao, sasa hivi high life huwezi jiunga mpaka uwe umetumia shilingi elfu tano kwa week na si chini ya hapo katika matumizi ya kawaida ya simu, kwahiyo basi unatakiwa kuweka elfu kumi ya awali katika moderm na shilingi elfu tano katika line na uitumie utakavyojua wewe iishe ili uweze jiunga na high life sasa ukiangalia mie si mtumiaji wa zantel imenishinda maana siwezi weka elfu tano halafu nipigie watu wakati sina inshu nao ili nipate high life katika moderm, kwa sasa high life jumla imekuwa elfu 15 wakati huo ni ya siku 7 uwe umetumia au hujatumia hizo 2gb zikitikimia siku 7 hakuna kujazia unaanza upya utumie elfu 5 katika simu na elfu kumi uweke kwenye moderm, kweli bongo ni keki ya birthday kila mhudhuriaji atakatiwa kipande kwa uwezo wake. TCRA wajaribu kudeal na watumiaji wajue tunaumiaje maana ndio wamebeba haki zetu zote katika mawasiliano bongo
 
Kinachonisumbua mimi ni hizi KAMARI wanazobuni kila mara za kuwaibia WATANZANIA mbumbumbu. Mara magari 100, mara nyumba ya milioni 100, mara shinda milioni 10, milioni 100, mara shinda muda wa maongezi kwa dakika kadhaa,......., ni wizi wizi wizi kwa kwenda mbele. Vyombo vyetu vya dola vipo. Kodi hazikusanywi kutokana na mapato haya. Jiulizeni tu VODACOM wanawezaje kukodi majengo yote yale pale MlimaniCity kisha wakatengeneza faida na kutoa gawio kwa wanahisa wake mbali na gharama zingine za kujitangaza kila mahali, kila Tv na kila barabara za mji huu?
 
Mwanakijiji
Hapa si inawahusu wale wanaojua kidhungu(english) tu. Nadhani sisi waswahili haituhusu. Sawa bwana kwa ubaguzi wenu. Mkimaliza kufanya huo sijui ni utafiti wenu kwa wale tu wanaojua kidhungu basi mtufikirie na sisi wana wa tanganyika na pia wana wazanzibar ambao lugha yetu halisi ni kiswahili ambacho kinafanya tuchangie kwa uelewa zaidi.

SWALI
Hivi ndugu mwanakijiji je tukikuita wewe ni kaburu tutakuwa tumekosea? Kwa mtazamo wangu mimi nakuona kama una ubaguzi. Mwanakijiji narudia tene wewe ni kaburu vinginevyo nakuomba uwashawishi wana JF hasa wale wanaopenda sana lugha yetu ya taifa kuwa wewe si kaburu ila umepitiwa tu katika jambo hili.

Nimesikitishwa sana na ubaguzi uliotutenda ndugu mwanakijiji.
 
Ndugu yangu mmoja kanitumia namba zake za simu; amenipa namba tatu za mkononi!!! huu ni wizi tu!

Ndugu MM huyo ndugu yako anajaribu kuepuka wizi wa makampuni ya simu kwa watanzania. Angalau kwa kuwa na namba tatu atapunguza matumizi yake ya simu. Ukitaka kujua niyasemayo jaribu kuweka 5000/= kwenye simu tigo/voda/airtel n.k alaf upige mtandao mwingine (yaani voda - tigo/ Airtel - vod/ tigo - zantel n.k) hata kabla hujamaliza maongezi utasikia simu imekatika!

Gharama ya mawasiliano hapa kwetu ni kubwa mno. Ikumbukwe siku za nyuma walikuwa wanaituibia sana manake angalau kwa sasa gharama zimeshuka sana hasa za simu ndani ya mtandao mmoja!

Sielewi vyema TCRA kwanini haiwezi kuwa kama EWURA ikapanga bei reasonable kwa mawasiliano???
 
<br />
<br />

Hapa kaka watu wengi huwa hatufatilii kama Tarrifs wanazozitangaza ni kweli, watanzania tumelala ila TCRA ndio imepewa dhamana ya kudeal na tarrifs zote ili watumiaji wa simu tusiibiwe sidhani kama wamejaribu kufanya japo reaserch japo ya kawaida, kilichobaki wanapeana mishahara mikubwa tu.

kila kitu mkuu tunageuza kama mapokeo no argument
We don't ask tunapokea kila kitu kinavyokuja
 
Ndugu MM huyo ndugu yako anajaribu kuepuka wizi wa makampuni ya simu kwa watanzania. Angalau kwa kuwa na namba tatu atapunguza matumizi yake ya simu. Ukitaka kujua niyasemayo jaribu kuweka 5000/= kwenye simu tigo/voda/airtel n.k alaf upige mtandao mwingine (yaani voda - tigo/ Airtel - vod/ tigo - zantel n.k) hata kabla hujamaliza maongezi utasikia simu imekatika!

Gharama ya mawasiliano hapa kwetu ni kubwa mno. Ikumbukwe siku za nyuma walikuwa wanaituibia sana manake angalau kwa sasa gharama zimeshuka sana hasa za simu ndani ya mtandao mmoja!

Sielewi vyema TCRA kwanini haiwezi kuwa kama EWURA ikapanga bei reasonable kwa mawasiliano???
TCRA ni wadau wakubwa kwenye wizi huu wa simu. Watanzania tunaibiwa sehemu nyingi tu. Kama unamiliki king'amuzi cha DSTV utashangaa zaidi kwa nini TCRA hawasemi lolote juu ya hawa makaburu kutuchaji kwa dola ndani ya nchi yetu! Akina Ami Mpungwe tuliwapeleka kule Afrika Kusini na wamekuwa mabalozi kweli si mchezo.
 
Biashara hiyo. Kama kuna demand, kwa nini wasitoe over-priced service. Consumer protection agency Tanzania hakuna, au mimi sijawahi kuisikia. I use on average $10/month kwenye simu. Napata sms 4000, nk! Hiyo ni elfu kumi na mbili ya bongo. Nilienda bongo, nikatumia Tsh10,000 chini ya wiki. Kutuma sms tu! Kwa nini rates bongo zipo juu kiasi hichi?
Kila siku haya makampuni ya simu yanatoa mashindano. Ivi watu hamjiulizi, hiyo pesa wanatoa wapi? Msisahau jinsi hizi kampuni zilivyoingiza serikali yetu mfukoni kwake. Kila siku utasikia visherehe, na watu wa serikali wamekaribishwa. Unaweza kukuta hata wanapewa line za bure.
 
Tukiachana na hoja zote hizo, najiuliza kwanini hakuna kampuni hata moja ya simiu inayomiliki jengo lake lenyewe?makampuni yote yamepanga au yameingia ubia katika ujenzi na wenye majengo
 
Kweli tunaibiwa sana halafu washen** hawa hawalipi kodi inavyotakiwa! Mie nna line 4 voda 2, tigo na airtel
 
Trend ya utumiaji mobile phone services in TZ ipo hivi: Mobile phone subscribers are now more than 15 million. We a number three in consumption of this service in Africa. Mobile phone service in India is 11% - 15% times cheaper than here. Likewise, the United States is 9% - 11% times less, while Kenya and Uganda is 10% - 15% lower than here. (SOURCE:https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/17519-big-scandals-by-mr-r-j-sabodo.html)

Nimejaribu kupata list ya TOP 10 TAX PAYERS IN Kenya, nimepata ya 2008 click link hapa:
http://www.marsgroupkenya.org/Reports/LawsandConventions/KRA_Distinguished_Taxpayers_List_2008.pdf,

Safaricom LTD ndo iliongoza kwa kulipa kodi Kenya! then ndo inakuja Kenya Breweries Ltd (KBL).


The same in Uganda! MTN Group ndo inaongoza kwa kulipa kodi, hii ni kwa financial year 2006/07, and it has been the leading taxpayer for 3 consecutive years, na trend ilivyo wataalamu wametabiri kuwa MTN inaweza kuongoza katika 3 coming years i.e.nanukuu: "The statistics prove that Ugandans are spending more on mobile phone airtime, fuel, beer and phones. The trend of consumption is likely to remain the same in the next three years".

hali ya Uganda ni kama ya TZ tu, makampuni ya cm yapo more than 3, na competition ni kubwa.

nanukuu kwa uganda: "The top 10 of the best 1000 taxpayers paid out about Ugshs753 billion which was 28.6 per cent of the total revenue. The 10 include, MTN, Shell, Uganda Breweries, Nile Breweries, Total Uganda, Tororo cement, Century Bottling Company (Coke), and *energy producers Aggreko International.
"SOURCE cheki hapa:MTN is again Uganda's top taxpayer (MTN is again Uganda's top taxpayer),

*TZ mbona hali ni tofauti sana? makampuni yenye wateja wengi, Vodacom na tigo, hayapo hata kwenye top 15!!wakati TZ kuna watumiaji wengi na gharama za simu ni kubwa! achilia mbali wizi wao wa kwenye "bahati nasibu" zao za kienyejienyeji!

me' sio mchumi but with such "situational and comparative analysis" nashawishika kuamini kuwa kuna walakini na ukwepaji wa kodi... naomba wataalamu wa haya mambo na wanajamvi tuyajadili haya na tutafute jinsi ya kuyafikisha mbele zaidi.
 
a. How many phone lines do you currently own?
two
b. What major phone companies do you use?
Tigo, Vodacom and Airtel
c. What would you consider to be your monthly average bills for all the phone services?
10,000...but sometimes it may rise
d. How do you afford to pay for all phone services - your phone bill is what percent of your expenditure?
we need mathematician here. since, I am not mathematically inclined then I prefer to skip this question
e. What percent of your income is the the amount of money you spend on phone services?
the same applies to this (skipping)
f. If you were given an option to have a phone service with an unlimited service for a flat rate for standard services would you continue to have more than one line?
For what??? hell no...and this is what I have been telling my friends. Our government have to do something here so that we have such service
 
Back
Top Bottom