Grain milling

majiyashingo

Member
Feb 2, 2011
44
2
HabarI za jioni wana JF
kutokana na ongezo la watu na umuhimu wa chakula nilikuwa nataka kuanzisha Grain milling ambayo itakuwa ikisaga unga wa mahindi na kufanya packaging kwenye mifuko ya kilo moja moja na kilo 10 na hamsini.Je kwa watalamu wa mambo haya hii biashaa mnaionaje ambapo ukilinganisha tayari kuna Giant wa kuuza unga Bakhresa?je ni rahisi kuingia kwenye soko kweli au niachane na hili wazo au ni wapo naweza kupata soko zaidi.Nategemea kusaga kwa kufuata standards zote na technologia ya juu pia.Msaada wa mawazo jamani
 
Riz1 nae ameshawekeza kwenye biashara hii pale kibaha tena kwa scale kubwa kuliko bakhresa
 
Bwana huyu Riz 1 ndo nani unaweza kunipa dondoo hata website kama wanayo ili niangalie hiyo production yao
 
haa haaaaaa haaaaaaaa .... humjui Riz1 ..... mtoto wa mkulu

ningekushauri ujikite kwenye value addition ya grains products ... whether packaging or the likes .... wapo wazalishaji wengi sana katika vitongoji wana mashine ndogo ndogo na wao pia wanapack kwenye vironba 5kg, 10kg 25kg
 
ala kumbe hiyu mtoto wa kigogo))du sasa naona ushindani mkubwa vipi nikiwekeza kwenye Rice milling au napo ushindani wa vigogo mkubwa?
 
mkuu ... rice milling pia kuna utitiri ... kinachotokea ni kwamba wakulima wenyewe huenda kufanya milling na kuuza rice grain, sijui utaifanyaje na ni lazima uwekeze sehemu zenye source ya mpunga
 
Waweza kuwekeza kwenye rice milling(if it is the correct word) ama hata maize milling, do not wory about the competition watu wananunua mabasi mapya yakwenda mikoani pamoja na utitiri wa mabasi mengi na bado wanapata wateja. Population inaongezeza na opportunity za biashara zinaongozeka pia. My only ushauri is that SEEK A STRATEGIC LOCATION. Location is very important as well as the lay out. One problem of people who have gone to school, we analyse alot and do alot of some risk calculations and we end up with FEAR( False Evidence Appearing Real). Don't fear man, just go into business consider location of the business, carefully select the people to be involved, and do it. I am encouraging you go for it.
 
Hiyo ni biashara nzuri sana. Nimefanya utafiti na kugundua watanzania wengi wanatumia mapato mengi zaidi katika chakula. Mvua nazo huwa siyo za kutegemea. Mwaka huu kwa mfano, chakula kinategemewa kupanda bei kwani kulikuwa na ukame na mvua hazijanyesha kwa wakati katika baadhi ya mikoa. Bakresa anauza sana nje ya nchi na hana uwezo wa kulisha watanzania wote.

Angalia sana gharama kwani kuweka katika vufungashio vizuri, gharama za kununua mahindi, uwezo wa mashine yako nk ni bora ukafanya upembuzi yakinifu. Angalia uwezo wa mashine yako kwa siku, kwa mwezi, kwa mwaka. Unahitaji tani ngapi za mahindi? ni sawa na eka ngapi? utanunua wapi na una uwezo wa kuweka ghala la tani ngapi? Kwa gharama gani?

Ki msingi hiyo ni biashara nzuri ukizingatia mambo muhimu hususani gharama za uendeshaji ili ujivunie bei nzuri.
 
wazo zuri
unga wa mahindi una faida ndogo kwa kilo,ila una nunuliwa sana,jiandae kuwa na network ya usafirishaji wa bidhaa zako,uwe na msingi wa kukopesha wholesalers ,unaacha mzigo unakuja kuchukua pesa after a week or two.tarajia kuibiwa na wafanyakazi wako,unatakiwa kuweka supervisor makini na asiye na tamaa,ideally awe mwanamke.
kuongeza faida,unakuwa na side business ya chakula cha mifugo,unapotoa pumba unatengeneza chakula cha mifugo
 
Back
Top Bottom