Graduation ya mzumbe secondary yaahilishwa kwa sababu ya chadema

Nyamemba

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
845
446
Katika kile kinachoonyesha kuwa mabadiliko ndani ya jamii hayaepukiki,wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya wavulana ya mzumbe iliyopo hapa morogoro wameendelea na msimamo wao wa kuushinikiza uongozi wa shule hii kongwe na mahili katika taaluma hapa nchini uwaalike viongozi wa CHADEMA katika mahafari yao ambayo yalikuwa yafanyike alhamisi hii na kuahilishwa mpaka hapo itakapo tangazwa tena.Wanafunzi hao wameendelea kumnyima usingizi mkuu wa shule huyo kwani amebainisha wazi kuwa hawezi kutimiza matakwa ya wanafunzi hao kwa kuwa anahisi atapoteza kibarua chake,yeye ameendelea kuwashinikiza walete viongozi wa serikali mfano mh SITTA/MWAKYEMBE au yeyote ilimradi atoke ndani ya serikali lakini wamekataa na kuahidi kufanya kituko iwapo ataenda kinyume na matakwa yao,wanamtaka either mh MBOWE/ZITTO/dr SLAA au MNYIKA.
 
Mhh lazima aogope kibarua kuota nyasi hapo
Na akiwaita tuu hao ajue kesho yake anapokea barua ya kustaafihsw akwa manufaa ya umma
 
Dah?! Dotcom hii!! wangekuwa wanafunzi wa darasa la saba, ningeelewa...lakini form four???! come on guys kuna tofauti kati ya uongozi wa chama na serikali, fine hamwapendi CCM but not to that extent, ...it's one of Special school, doing that itashusha hata hadhi yenu... hapa nawashauri tumieni hekima ya wakubwa wenu si ushabiki!!
 
there is no way out,cha msingi wasifanye hiyo gradu kwani wanaweza kuzomea kitu ambacho si kizuri pia
 
Mkuu mgeni wa heshima kwenye mahafali hana uhusiano na kushusha heshima ya kitu
Maana anachokuja kufanya sio kupiga siasa ila kufanya kile kilichompeleka pale ambacho ni kuwapa vyeti vyao vya Leaving
NA vile vile vijana wana uwezo wa kumtaka mgeni wao wa heshima sio wa kulazimishwa
 
Ikitokea mkuu akalazimisha basi watakaoalikwa wajiandae na zomeazomea ya ajabu. Bora kinga iwe tahadhari mapema.

hiyo zomea zomea jana imemkuta mtoto wa mkulima,mh.mizengwe , na kumfanya akose amani na kushindwa kuhutubia alichokuwa amelenga.
 
Dah?! Dotcom hii!! wangekuwa wanafunzi wa darasa la saba, ningeelewa...lakini form four???! come on guys kuna tofauti kati ya uongozi wa chama na serikali, fine hamwapendi CCM but not to that extent, ...it's one of Special school, doing that itashusha hata hadhi yenu... hapa nawashauri tumieni hekima ya wakubwa wenu si ushabiki!!

acha uzuzu hio serikali wameshaona porojo zao muda mrefu ivo ni bora waaachanene nao mm naona washikilie msimamo wao huo huo mpka kieleweke kama vip bora wapige chin hi sherehe kama wanachotaka mkuu wao ataamua kutumia ubabe wa kumleta huyo 6 mnafiki na ndumilakuwili
 
kazi ndo imeanza na mtoto wa mkulima keshaonja joto la jiwe mwanza,nani atakubali kuuvaa mkenge wa mzumbe.
 
Headmaster Mzumbe secondary.............NJAWA
Secondmaster Mzumbe secondary...........MTELESI

>>>>>jitahidini kuukabiri huo upepo!!!!!
 
Hawa wa2 ni wanoko nomaa.. njawa na mtelesi.. acheni 2.. nakumbuka kitambo icho kabla hawajakamatia izo posts
 
headmaster mzumbe secondary.............njawa
secondmaster mzumbe secondary...........mtelesi

>>>>>jitahidini kuukabiri huo upepo!!!!!


maskini shule yangu,,!!
Enzi zetu zile huwez skia malumbano kama hayo thubutuu af msuli tumwachie nani??

Nawakumbuka sana mzee mwasha,bitwale,mtesigwa na wibonelee..!!

Vijana pigeni shulee
wanasiasa hawatawasaidia chochote kile...!!
 
True story..mwaka 2010 wakati wa uchaguzi mkuu wanafunzi wa shule ya sekondari Bwiru boys iliyoko mwanza nikiwa miongoni mwao tuliongoza zomea zomea kwa aliyekuwa anagombea ubunge ndg Antony Dialo na diwani wake katika kampeini za uchaguzi zilizokuwa zikifanyika katika viwanja vya Bwiru zikijumuishwa shule mbili yani bwiru boys na Bwiru girls..zilizo sababisha mkutano kuvunjika na baadae kabineti hyo ikajipanga lasmi siku nyingine na kuja shuleni kuongea na wanafunzi lakini hali ilizidi kuwa ile ile na kumfanya ndugu Dialo kukata tamaa na diwani wake wa eneo hilo.
Siku ya uchaguzi baadhi ya wanafunzi walijitolea kwenda kusimamia vituo maeneo ya vijijini yaliyokuwa nje ya mji kidogo wakiwakirisha CHADEMA...Hatimaye matoke yakatangazwa na diwani wetu wa Chadema mwana mama kunyakuwa udiwani na mbunge wa chadema kushinda wilaya ya Ilemala.
Shamlashamla zilitanda shuleni kuanzia saa mbili baada ya matokeo ya udiwani ktk eneo letu kutangazwa..

kinachoendelea Mzumbe sishangai ni mabadiliko.. Tumeichoka SISIEMU.
 
Back
Top Bottom