GPS inahitajika haraka

Mtazamotu

Member
Jul 29, 2011
21
10
Nawasalimu wajameni, Naomba mwenye ufahamu ni wapi ndani ya bongo (Dar) naweza kupata GPS (Global Positioning System) anielekeze ninahitaji kupata kadhaa. Natanguliza shukrani.
 
Ninayo moja mpya ya black and white kama unaihitaji tafadhali ni pm, ninaiuza Tsh 100,000/=. Napatikana Dar es salaam.
 
Mlimani City duka lipo ndani kwenye kona kama unaenda CRDB ukitokea NMB,
 
Mi naomba mnitoe ushamba!! hivi hizi gps kwetu bongo hii zinakuwa zinafanya vipi kazi wakati hata mitaa mingine haina majina na mipango miji ndio kama ilivyo!!?
 
Mi naomba mnitoe ushamba!! hivi hizi gps kwetu bongo hii zinakuwa zinafanya vipi kazi wakati hata mitaa mingine haina majina na mipango miji ndio kama ilivyo!!?
Kwenye kukusanya data mkuu ndiko kwa sasa zinatumika sana mkuu,kwa kuangalia point ni rahisi kutrace sehemu data zilipochukuliwa pia huonyesha hadi ramani alivyokuwa anatembea huyo mchukua data,pia hutuma data huku zinakohitajika badala ya kutumia dodoso a.k.a questionnaire
 
Aah Ok, kwa mtindo huo! mi nilifikiri nikiiwasha halafu nikajifanya sipajui kule mtaani kwetu ingeweza kunionyesha njia, hiyo ingekubali aisee ningeamini kwetu kumekucha!!
 
Kwenye kukusanya data mkuu ndiko kwa sasa zinatumika sana mkuu,kwa kuangalia point ni rahisi kutrace sehemu data zilipochukuliwa pia huonyesha hadi ramani alivyokuwa anatembea huyo mchukua data,pia hutuma data huku zinakohitajika badala ya kutumia dodoso a.k.a questionnaire
Aah Asante kaka, maana nilikuwa niko kizani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom