Govt slams UN report on Arms Trafficking; demands apology

Ni vyema tu-derive history Kabila katokea bongo sasa alienda kupigana vita bila ya silaha au alikutana nazo huko, kama Kabila alipigwa tafu na bongo kwanini isiwe waasi wengine hili moja tu.

Ukweli ni kwamba Tanzania tunatambulika kwamba tunasaidia waasi katika nchi za Congo, Burundi na Rwanda manake hata vita vyao ni wabongo ndio wanamaliza juzi juzi tu wabongo walimtoa msituni mtata wa mwisho Burundi. Sasa msipende sifa nzuri tu ili muonekane watu wema siku zote wengine hawafurahii msaada mnao toa hasa wazungu ambao kwao hawana rafiki wa kudumu na maslahi yao kwanza.

Hata UN wenyewe washashutumiwa kuhusika na vita congo manake wana silaha na jeshi lakini hawachukui hatua mauaji yanapotokea zaidi ya kulinda ngome zao. Silaha hazitengenezwi Tanzania kuwaacha watengenezaji ni ubeberu wa wazungu kupitia UN kukandamiza wanyonge na kuwagawa ili waendelee kutawala. Mbona madawa ya kulevya wameenda Kabul kupiga source lakini kama kuna mwanaume aende kupiga kiwanda cha AK 47 huko kilipo na grinade zinazouzwa kama njugu au akitaje tu kuhusika aone cha mtema kuni.

Wanapolalamika wa Iran kuhusu UN na mataifa ya wazungu mnaona poa lakini mkumbuke na nyinyi sio salama. Msaada wote wa kukaa na wakimbizi miaka yote, kutuharibia mazingira na kuleta majambazi this is the price kutoka UN, watutake radhi please. Wote watushutumu lakini sio UN jamani tumefanya kazi zao sana tu.

Sio kweli kabisa kwamba mizigo yote ya huko inapitia Dar kama mchangiaji mmoja alivyosema, Mombasa inapita mizigo mingi kwenda Rwanda, Burundi na hatimaye congo kumbukeni pia congo inapakana na Sudan ya kusini.
 
Mimi nafikiri serikali inawajibika kujibu taarifa hizi ambazo kwa sasa hii inakuwa ni ya nne kama sikosei ikijumlishwa ile ya Meremeta ya Mwanakijiji.

Ya kwanza ni ile documentary ya Darwin's Nightmare ya mwaka 2004, ambayo ilitengenezwa na Hubert Sauper na ilikuwa ikielezea kwa undani jinsi silaha mbalimbali kutoka Russia zinavyopitishwa katika bandari yetu hadi nchi za maziwa makuu hususan DRC.

Ikaja taarifa ingine mwezi May mwaka huu ilioandikwa na Stockholm International Peace Research Institute (SIPRI), ambayo ilikuwa ikieleza kwamba kumeonekana ndege za kampuni ya Aviacon kwenye anga la Tanzania na kwamba ndege hizo zilikuwa zikisafirisha silaha zinazotengenezwa na kampuni za silaha za kirusi kwenda katika DRC na sehemu zingine zenye migogoro kama Burundi, Uganda na Rwanda.

Jambo la msingi na muhimu hapa ni kwamba wale woote wanaohusika katika majambo haya ni watu ambao ama wana ama hawana mahusiano na serikali ya Tanzania na kama wana uhusiano na serikali basi ni lazima serikali inafahamu.

Ikiwa hawana mahusiano na serikali basi ni lazima serikali iwajibike na mikataba ya kimataifa ambayo inazuia uingizaji, usambazaji na uuzaji wa silaha hizo kimagendo kwenye sehemu zenye migogoro au kwa kubadilisha na madini.

Tabia ya kuruka na kusema kwamba taarifa hizi ni uongo wakti watu wenye utaalam wa kuchunguza wanagundua na kuona kwamba silaha hizo zinapitishwa katika anga na ardhi ya Tanzania tunakuwa "totally irresponsible"
 
Hii nchi tunapenda uongo hii. Tumedanganya sasa tumemaliza kwa kuanza kujidaganya wenyewe. Safari yetu ya uongo bado inaendelea!!
 
Tanzania ina kiwanda cha kutengeneza silaha..au hujui nchi zenye kutengeneza silaha.
inategemea unamaanisha silaha ya namna gani, na za kiwango kipi, kwa taarifa yako Kiwanda cha mzinga Morogoro kinaunda Risasi za bunduki za Aina zote, milipuko yote ya vifaru na magari ya deraya. Elimika .
 
Wanasiasa wa Tz, Membe akiwa mmoja wao ni mahodari sana wa Kung'aka. Hata mheshimiwa huyu kwa bahati mbaya akisahau kufunga zipu ya suruali yake, halafu akatokea msamaria na kumwambia "mheshimiwa samahani, hujafunga zipu ya suruali yako" atang'aka na kusema "hapana,si kweli. Umejuaje?"

C'mon Membe, basi sema kuwa Tanzania huwa tunapitisha silaha za maziwa makuu kupitia bandari ya salama, isipokuwa mwenye silaha hatumjui! kwa maana silaha za kivita zinajulikana na zimewahi kuonekana zikikatiza mitaa kuelekea nchi jirani mchana na usiku. Ukikubali haya, basi ukubali na matumizi ya hizo silaha na destination zake kama vile kwenye mikono sahihi au mikono haramu ya waasi. lakini si kun'gaka tu, Mheshimiwa hujafunga zipu ya suruali yako, nasi tumeona.
 
Hivi kwa nini wamarekani na jeshi la NATO (EU) wasije kutoa kichapo kwa CCM, tumechoshwa na haya mambo. Waje hawa jamaa watuchapechape mpaka vitambi vya akina Makamba na Rostam vipungue labda viongozi wetu wanaweza kujali na kusikia vilio vya wananchi.


Wananchi wanakufa na njaa huku wachache wananeemeka kwa kupitia njia za kilaghai na kuchochea uasi nchi za wenzetu.
 
tumeanza kuwa kama Wamarekani! tunalia na kushangilia "nchi yangu, nchi yangu" huku inafanya mambo ya kijinga duniani; huu ni uzalendo wa kipumbavu!
 
Hujajibu swali? tanzania ina kiwanda cha kutengeneza silaha mpaka iwauzie rebel?

Mkuu ulisoma ripoti lakini? maana maswali yako yanajibika kirahisi tu kama ulipitia ripoti.Hivi utatupa kazi ya kuandika mambo mengi ambayo ingekua rahisi tu wewe kuyajua kama ungekua umesoma ripoti.
 
Yes Tanzania ni nchi inayeheshimiwa hata na majirani zetu na anga za kimataifa, lakini tujiulize sisi waTz, hivi hii ripoti ingeigusa kenya tungereact vipi?

Je nchi yetu ikiwa na heshima tele, does it mean kwamba hakua wachache wenye nia mbaya wanaoweza kutumia utulivu wetu vibaya

Yaani inawezekana kweli tusingiziwe na ripoti tofauti za miaka tofauti kuhusu jambo hilohilo?

Lipo jambo na dawa yake ni kulifanyia kazi na kutoa ahadi na timeline,

tusipoangalia tutaishia ya mbagala, mapaka leo tunasubiri, ya EPA, ya CIS, Ya Richmond

We need to wake up now and show everyone that we can be more accountable and serious!!
 
Ni ubishi usio na maana kwamba Tanzania haisadii waasi Kongo. Inahuzunisha kwamba hii yote inafanyika kwa maslahi binafsi ya watu wachache na si kwa maslahi ya Taifa. Wakati wa vita ya kumng'oa nduli serikali ilishirikiana na akina Obote waliokuwa waasi kwa maslahi ya Taifa letu, lakini si sasa. Tusiache kuhoji maamuzi ya serikali yanayochukuliwa kwa manufaa ya kikundi cha watu fulani.
 
Mjadala huu umekosa uzalendo kwa kiasi kikubwa na wengi wenu mko tayari kuamini wachonganisha wa kimataifa na kuliacha Taifa lenu kwenye matatizo makubwa...this is nonsense na kila mwenye harufu ya uzalendo lazima ajitahidi kuipinga .
 
Mjadala huu umekosa uzalendo kwa kiasi kikubwa na wengi wenu mko tayari kuamini wachonganisha wa kimataifa na kuliacha Taifa lenu kwenye matatizo makubwa...this is nonsense na kila mwenye harufu ya uzalendo lazima ajitahidi kuipinga .

Mkuu sasa ukatae tu kuwa jikoni kwako hakuungui wakati moshi unaonekana?
 
I am afraid what has met the eye of vi nzi and the UN panel is just a tip of the iceberg.
 
Tatizo la baadhi ya Watanzania ni kujifanya wazalendo sana na kuiona serikali na viongozi wake kuwa ni watu waadilifu wakati sote tunajua asilimia kubwa ya viongozi serikalini ni Mafisadi na Majambazi. Mnaoitetea Serikali na viongozi wake waliojihusisha kwenye biashara hii haramu mjijue mna uzalendo wa kifisadi na kijambazi.
 
its a big issue here, i wondre if thid report is true or not but what i think, is not true these reporters do not know very well about tanzanian, our country is THE ISLAND OF PEACE we cannot do that.
 
its a big issue here, i wondre if thid report is true or not but what i think, is not true these reporters do not know very well about tanzanian, our country is THE ISLAND OF PEACE we cannot do that.

Umesoma ripoti?

Umejaribu kupatab majibu ya maswali yanayoulizwa na ripoti?

Umeangalia majibu ya Membe yalivyo ya kitoto kulinganisha na details za ripoti hii?

Island of peace wapi wakati watu wanakufa kwa njaa kila siku, watu wamezikwa hai huko Bulyankulu?


Au unataka kuleta falsafa za mbuni kufukia kichwa kwenye mchanga? My country right or wrong style?
 
ASSA MWAMBENE hajaja kumtetea bosi wake?


Jamaa atakuwa na kazi kama ya wale Hollywood publicists wa Britney Spears, yaani wao wanajua kwamba Britney chizi na anaweza kubwatuka vyovyote saa yoyote, kazi yao ku spin PR.

Well, mi nishasema tutaona denial ya denial sasa hivi, either that au tunakubali kuanza kuwa a pariah state.
 
Back
Top Bottom