Govt slams UN report on Arms Trafficking; demands apology

Kuna harufu ya ndege za Victor Anatoliyevich Bout, by the way ata report ya UN ya tarehe 22 december 2000 wamezungumzia hili.
 
Meremeta and other front companies run by our intelligence services have been doing this all along.

We need to reclaim our country.

Godbless
 
Daa! kumbe hawa majamaa mimi nilifikiri kuwa wanatuua wenyewe tu kumbe wamevuka mpaka nchi za jirani? Lazima tuwafanyie kitu fulani hawa la sivyo history itatuhukumu
 
na Mwandishi Maalumu, Port of Spain, Trinidad & Tabago




WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema ripoti iliyotolewa hivi karibuni, inayodai kuwa Tanzania inawapa silaha waasi wa kikundi cha FDLR Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ili kuwadhuru wananchi wenye asili ya Rwanda na Congo wanaoishi katika eneo hilo ni ya uzushi, uzandiki wa makusudi na jitihada za kuchafua jina zuri la Tanzania.

Amesema kutokana na uongo huo, Tanzania inastahili kuombwa radhi na wote wanaohusika kuiandaa ripoti hiyo iliyoandaliwa na kikundi cha wataalam watano wanaohusishwa na Umoja wa Mataifa (UN).

Waziri Membe alisema ni jambo lisiloingia akilini kuwa nchi kama Tanzania iliyofanya mambo mengi na kujitolea mhanga kwa kila hali kuleta amani na kujenga usalama katika eneo la Maziwa Makuu, inaweza kushutumiwa kwa kutoa silaha kwa waasi wa FDLR.

Alitoa ufafanuzi huo alipozungumza na waandishi wa habari mjini hapa kuhusiana na habari za ripoti hiyo ambazo zimekuwa zinatangazwa katika vyombo vya habari.

Waziri Membe yuko mjini hapa akiandamana na Rais Jakaya Kikwete kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuia ya Madola unaoendelea.

"Ripoti hiyo ni uongo wenye nia mbaya kwa Tanzania ambayo imetungwa kwa kuchochewa na nia ya kulichafua jina zuri la Tanzania na serikali yetu," alisema.

Alisema Tanzania haijapata na kamwe haitapata kufikiria kujiingiza katika vitendo vya ovyo, visivyokuwa na maana na vya kutojali vya kushiriki katika biashara ya silaha kwa nia ya kuchochea vurugu dhidi ya majirani rafiki kama Rwanda na DRC.

"Tofauti na madai hayo, Tanzania itaendelea kufanya mema katika hali ya machafuko na vurugu. Tanzania itaendelea kushirikiana na wengine katika jitihada za kumaliza, na wala si kuchochea vurugu na migogoro. Kamwe hatutamwaga petroli kwenye moto.

"Hii ndiyo kazi ambayo Tanzania imekuwa inaifanya, na inaendelea kuifanya, katika miaka 15 iliyopita. Rekodi yetu katika hili inajulikana na inajisemea na kujithibitisha yenyewe. Tanzania kamwe haiwezi kushiriki katika unafiki," alisema.

Aidha, alisema tokea kutoka kwa ripoti hiyo, Tanzania imekuwa inashangaa ni wapi inapata silaha hizo.

"Kwa bahati mbaya sana, ripoti hiyo haisaidii kutoa mwelekeo katika jambo hilo. Inachofanya ripoti hiyo ni kukariri watu wasiotajwa, kusema uzushi na kufikia maamuzi yasiyokuwa na msingi.

"Kazi ya kikundi hiki imeiacha Serikali ya Tanzania ikishangazwa na kiwango cha kutisha cha ukosefu wa ufanisi na ukosefu wa weledi iliyofanywa na kikundi kilichoundwa na Umoja wa Mataifa, taasisi ambayo Tanzania inajua kuwa ni makini na yenye kuheshimika sana.

"Serikali ya Tanzania inakuwa haina jingine la kufikiria isipokuwa kuichukulia ripoti hiyo kama madai yanayostahili kudharauliwa na yenye nia mbaya," alisema Wazir Membe.

Aliongeza kwa kueleza kuwa, Tanzania haina maduka ya kuuza silaha za kivita na hairuhusu maduka hayo. Licha ya kutokuwa na mipango ya kufanya hivyo sasa ama siku zijazo.

Alisema katika Tanzania, silaha za namna hiyo zimo mikononi mwa majeshi ya taifa, hivyo kikundi hicho kuihusisha Tanzania na vitendo vya kudharauliwa kama hivyo, inamwacha mtu kuanza kuamini kuwa silaha hizo zimetoka mikononi mwa majeshi ya ulinzi ya Tanzania.

"Nataka kumhakikishia kila mtu kuwa jambo hilo halijatokea na halitatokea kwa sababu serikali kamwe haiwezi kuliruhusu kutokea. Kwa hakika, hakuna hata ripoti za kupotea kwa silaha kutoka kwenye maghala ya silaha za jeshi letu la ulinzi ama polisi wetu.

"Ndiyo maana nasema kwa nguvu zote kuwa, ripoti hii imetungwa makusudi kwa nia mbaya dhidi ya Tanzania. Tanzania siku zote imekuwa mwanachama mwenye wajibu mkubwa katika eneo letu na katika familia ya Umoja wa Mataifa. Tanzania imefanya mengi kutafuta na kudumisha amani katika eneo la Maziwa Makuu na nje ya eneo hilo," alisema.

Kwa mujibu wa Jarida la Africa Confidential ambalo huchapishwa London, Uingereza, kikundi hicho cha wataalam cha UN kinaundwa na watu watano kutoka Ubelgiji, Guinea, Marekani, Italia na Uingereza.



Jamani nawashauri mawaziri wajihadhari na research za western countries mara nyingi zina ukweli kwasababu hawa mabwana wanahifadhi their academic integrity. Je unayosema mkuu kuna ukweli ndani? au wao wanasema ukweli? na Meremeta je!!!!!
 
Kwa ufafanuzi zaidi kuhusu tuhuma hizi unaweza kusoma makala moja
iliyoandikwa na Joseph Mihangwa ( Ukweli Kuhusu Kilimo Kwanza )
Wanajeshi wastaafu wa afrika ya kusini walivyobuni mpango wa kujipatia
mashamba makubwa sehemu kadhaa za afrika , ndani ya mipango hiyo ni
kusaidia vikundi vya waasi na kuuza silaha kwenye baadhi ya nchi ,
Wanajeshi hao wametajwa kwenye Taarifa ya mwanakijiji ( Meremeta )
Kwahiyo unaweza kusoma hivyo vichache tu ukapata mwanga kidogo ni nini
kinachoendelea
 
Unachokizungumza nakifahamu na kukielewa na nimezisoma ripoti zote hizo unajua zama za mawaziri wetu kusimama na kutudanganya zinaelekea ukingoni. Mh. Membe anataka kutumia msemo wa funika kikombe shetani (mwanaharamu) apite hauendi kihivyo kwa Tanzania ya leo.
 
lisemwalo lipo kama halipo laja. Nina hakika serikali yetu inajua wazi maana ya siasa za chuki fitna na ulaghai. Kama ni ulaghai tusiseme tu tuombwe radhi bali tuchukue hatua, hata kuufukuza umoja wa mataifa hapa Tanzania, si kuishia tu kuomba kuoimbwa radhi. Sio siri si mara ya kwanza Tanzania kutumiwa kusafirisha silaha na kuwa na "mamluki" nje ya nchi.

Tujiulize kwanini wanasema uongo kuhusu Tanzania? je ni uongo au si uongo? nani ni muongo?
 
Si ajabu kwani tz tumekuwa tukiwalea watu wanakwenda kufanya mapinduzi nchi zao hasa za maziwa makuu.mfano ni kabila mtot na baba yake ambaye ni marehemu,Yowerii wa uganda,Nkrunzinza wa burundi bila kuwasahau akiana wamba dia wamba waliokuwa waalimu mlimani na wa chi kama msumbiji na south africa,ukweli utajulikana ila inaweza ikawa kweli
 
lakini huyu msemaji wa TZ aliyeko nje huko si amesema atakuja na report kamili kudusu swala hili
 
Everything we want to build on lies will collapse! Mheshimiwa Membe ajue na kutambua kuwa siku za ubabaishaji, kutunga uongo ili kulinda maslahi ya watu wachache kwa gharama ya nchi nzima zinafikia ukingoni. Kila mtu atabeba mzigo wake.Na kuuzia silaha waasi siyo kazi ya chombo chochote cha serikali maana conflict kama hizo hazitunufaishi sisi kama Taifa labda some few individuals.
 
Kuna mtu wenye hiyo Ripoti atuwekee hapa..........please.....ngoja nami niitafute
Shukran Ogah kwa kuisaka, ukiipata au yeyoye atakayeipata atuwekee hapa ili tuisome. Tumesoma ripoti ya Mwanakijiji, tumemsikia Membe akiikataa ripoti ya UN, tuisome na ripoti yenyewe ili tuwe na mjadala wenye manufaa.
 
Tumeshikwa pabaya. Lisemwalo jamani...........Kabla Rais wa Burundi wa sasa kuingia madarakani, Burundi iliipigia kelele Tanzania kwamba inawasaidia waasi, TZ waliruka viunzi, lakini kwa wale wanaotoka mpakani walijua kinachoendelea (TZ ilihusika). Kwa hili la sasa, yawezekana isiwe TZ kama nchi, lakini wanaohitaji utajiri kwa kuua albino, kulamba fedha za umma na kuacha waTZ wakifa kwa kukosa dawa mnadhani kuuza siraha kwenye maeneo yenye migogoro watashindwa?????????????Ufisadi maana yake ni pamoja na kukosa 'elements' za ki-binadamu kinachoangaliwa ni kujipatia fedha hata wote tufe bora yeye apate fedha zake. Hapa tuendelee kulichunguza inaonekana ni kundi la waroho wa fedha. Waziri usikurupuke, watafiti hao sio wajinga, kwa nini hawakuitaja kenya?Somalia penye siraha kama ubuyu? Burundi?Zambia au Rwanda??????
 
Hivi,wachunguzi wa mambo hayo mnasemaje? je, ripoti inalenga kuchafua taswira ya Tanzania kama Membe na wengine tuliosadikishwa au ni kweli kuna insider dealings zinaendelea?
 
Haiwezekani UN wakurupuke na watoe report ya uongo. Kwa sisi tunaowafahamu viongozi wetu wenyewe kusema uongo si tatizo kwao kwani wanafikiri watu wote dunia ni wajinga. Mnakumbuka issue ya mapanki (mabaki ya samaki)? hivi ni kweli wananchi wahayatumii kama kitoweo? mimi nipo kanda ya ziwa haya mabaki wananchi wanayatumia sana tu. Lakini kwa vile imeishajulikana nje walikanusha tena kwa nguvu sana.
 
Nilipokuwa Burundi zaidi ya mara tatu nilishawahi kuambiwa kuwa nyie watanzania mnasaidia waasi katika nchi za maziwa makuu uhsusani nafasi ya Tanzainia ni kubwa na shutuma za kusaidia waasi si za kubeza. Inawezekana ni minong'ono ya mitaani lakini Tanzania kusemekana kusaidia waasi lipo kitambo sasa ni wakati muafaka kusoma between lines ili kujisafisha badala kutumia nguvu kubwa kukanusha ili kuonekana nice guys.

Mandela, Kabila, Nkurunzinza, Museveni na Kagame wote hawa walikuwa waasi na kushinda mapambano ndio kutangazwa marais na Tanzania imewapiga tafu kwa hali na mali sasa kukataa ni sawa lakini uwasi unabaki kuwa uasi. Hawa watu kama si kuishi Tanzania basi walianza mapambano kutokea Tanzania na Kushinda na kijiografia nchi hizi zinategemea bandari ya Dar kitu ambacho kuongeza shaka kwamba hata silaha zinapitia bongo.

Membe anatakiwa kudadavua kwa undani zaidi ni namna gani hatuhusiki sio tu na Kongo bali na nchi nyingine ambazo tumewasaidia kwa nia njema kupigania uhuru manake hata ukishinda vita sio wote wana kukubali.
 
Back
Top Bottom