Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 56
FM,
Najua Kifukwe sio mzungu (namfahamu yeye binafsi kwa karibu mno)ila hiyo ni kampuni ya Wazungu na ndio maana ilifanikiwa kufanya kazi kubwa kubwa miaka kumi bila hata kuguswa.
Ingelikuwa kampuni ya mswahili ungeona wasingemaliza hata mwezi.
Middle class ya Watanzania ndio wasaliti wakubwa wa nchi. Wanaweza kuja hapa JF kulaani viongozi mafisadi lakini kama ni mtu clean na umewahi kufanya biashara TZ, utajua ninasema nini. Hao hao walioko Brela, TRA, banks, ardhi nk. wanaihujumu TZ kwa njia chungu nzima. Kibaya zaidi wanakwamisha Watanzania wenzao, wakati wakija Wazungu wanalegea, shame on them!
Ndio maana watu kama akina Kifukwe kwa kutumia ukaribu wao na Wazungu wakaweza kupeta miaka yote hiyo bila kuguswa wala kulipwa kodi.
Na hili ndilo tatizo kubwa sana huko serikalini no wonder kina Rostam wanaiba na kupeta bila kujali hata kidogo. Ukitaka kufanya mambo yako kwa halali unazungushwa kama mjinga wakati wenye dola tano mifukoni toka nje wanapata mabilioni!