Gosbert Blandes acha kutudhalilisha Karagwe

Kagera tuna bahati mbaya maana jioni hii nimesikia gamba jingine Jason Rweikiza likisema uongo kwamba limezunguka katika vijiji vyote vya jimbo lake kuchukua maoni ya wapigara kura wake. Ni aibu sana Bkb na Buhaya kuwa na wabunge waongo na wanafiki. Tusifanye makosa uchaguzi ujao hata kama Kanali Masawe atakua bado yupo Kagera.

shiiiiiti!! Huyu jamaa kapita saa ngapi kukusanya maoni!?. mwanzo bibi na babu zangu walionekana kumwamini kumbe ni zuzu,nasikia anawahadaa wananchi eti umeme kaupeleka yeye kule vijijini..huyu anatudhalilisha sana,hv bukoba tumelogwa?
 
Ntahakikisha kabla ya kurudi Kigoma next month nahamasisha kufanyika mkutano mmoja wa hadhara ili kuwaeleza wananchi juu ya upuuzi huu toka kwa Blandes.
 
Blunder hii ni kawaida yake, oh sorry, - Blandes mambo yake kila siku ni blunders tupu kama jina lake.
 
hata mimi naishi omurushaka lakini sijawahi kusikia kitu kama hicho, huyo jamaa hana akili, kwanza huwa anaogopa kuchangia bungeni, jama hanaga confidence kabisa, huwa anawambia wanakaragwe eti anachangia kwa maandishi, sijui huwa anachangia kwa kutuma sms kwa spika?
 
Kuna mabo mengine yanamshangaza kila mwenye kufikiri kwa kutumia kwa akili. Juzi madam speaker alisema aliwakataza wabunge kwenda kutafuta mawazo ya wananchi juu ya mswada. Kama nitakumbuka vizuri alisema "niliwazuia kwenda hata ulaya si mikoani tu". Sasa huyu the so called mbunge wa Karagwe alikusanya maoni kwa amri ya nani? Pili kama sikosei Blandes alikuwa kwenye tume ya Jairo muda wote huo. Sasa hayo maoni aliyakusanya lini na wapi? Hakuna sheria ya wapiga kura kum~vote out mbunge anayewasingizia?

Ndugu yangu maoni kwa mswada upi?
wakati huu ni mpya na wamepewa juzi tu hapohapo wanaanza kuuchangia?
na kusema eti wametumwa? nani kawatuma?
Wangu mimi wa ARUMERU hata sijuhi yuko wapi?
 
Mkoa wa Kagera una bahati mbaya msimu huu kwani wabunge wengi vilaza na mfano mzuri ni wabunge wa Nkenge,Karagwe,Bukoba vijijini! Nadhani wahaya wamepoteza heshima yao kwa kuchagua vilaza! Nakumbuka enzi za Kinyondo,Rwakatale,Zimbiile,Rwegasila,Mzee wa Biharamulo walikuwa majembe.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom