Good news wana JF: Pata viwanja vilivyopimwa

hizi gharama za kununua viwanja siku hizi mmh!mmh! ni kama unauziwa kivuko
 
Du mkuu hizo milioni siku hizi naona hazina tofauti na mamia, sq meter 500 milion 14, mtu mwenye kipato cha laki mbili kwa mwezi na anajitahidi kusave laki moja na nusu itamchukua takribani miaka minane kununua hako kakijipande kaardhi, jamani kuweni na huruma thamani ya ardhi haijapanda kiasi hicho.
na tajenga baada ya miaka 16..................good news nikajua mishahara imepanda kwa wafanyakazi wa umma
 
Mkuu vipo visivyopimwa kwa tsh 3m

Ndo maana watu wengi akikuta form anatakiwa ajaze namba ya kitalu na namba ya kiwanja ni kuacha blank tu, ya nini nitumie milioni 14 kununua kiwanja kidogo kisa kimepimwa, ingekuwa ukikaa sehemu iliyopimwa huugui ningejikongoja, wadau watakucheki kwa bei zako wenye nazo ila wengi wetu tutaishia kusoma tu hapa na kucomment, lakini bado nashauri muwe na huruma hiyo siyo thamani yake kabisa kwa kiwanja kidogo namna hiyo, tajeni bei reasonable mrudishe hela yenu na faida kidogo siyo unataja bei kuuubwa utafikiri binadamu kahusika kuumba ardhi.
 
Nilishawahi kutapeliwa pesa zangu kwa kiwanja ambacho kumbe kilishauzwa kitambo.
Natumai hii sio utapeli.
 

Nikusaidie maana nami nina cha kwangu kule!!
Mwanagati ipo Kitunda kuzunguka uwanja wa ndege wa DSM ambapo unaweza kupitia Ukonga Banana ukachukua gari za Kitunda,
Au unaweza pia kupitia Temeke ukashukia Davis Corner kama unatumia daladala kisha ulachukua gari nyingine za kukupeleka huko.
Ni eneo la viwanja vya mradi vya wizara kama lilivyo kigamboni, kijichi, bunju nk. Hivyo hata nyumba na viwanja vyake vimekaa kimpangilio.
Sina uhakika sana na bei aliyoitaja, but mimi nlinunua mwaka jana mwezi wa sita Sqm 620 kwa Tshs 12Mil.
 
Kwa ndugu zangu wana jf wote kwa wenye nia ya kujenga, Pata viwanja vilivyo pimwa maeneo ya Mwanagati square meter 500 kwa tsh 14m,square meter 1500 tsh 25m kuna maji na umeme vipo viwanja 8 tu Pia square meter614 tsh 15m umeme na maji vipo HAYA KAZI KWENU!
wasiliana kwa 0763 150 550, 0769 416 384 au 0612 42 66 33
Crazy Biashara huria.. Sq 500 14 m? bora nisepe mkoa... asante kwa taarifa mkulu..
 
Du mkuu hizo milioni siku hizi naona hazina tofauti na mamia, sq meter 500 milion 14, mtu mwenye kipato cha laki mbili kwa mwezi na anajitahidi kusave laki moja na nusu itamchukua takribani miaka minane kununua hako kakijipande kaardhi, jamani kuweni na huruma thamani ya ardhi haijapanda kiasi hicho.

na huyo mtu wakati anasave kwa ajili ya kununua kiwanja akumbuke time value of money. Maji yanazidi unga.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom