Goli ni Goli; la Mpendazoe nalo Goli!

Katika kutapatapa kwake Msekwa anasema Kuondoka kwa Mpendazoe ni kama kutoa ndoo moja ya maji kutoka mto Rufiji.

All in all he is ahead of them if at all they had any plans to expel him fro the party
 
Kuna habari kuwa msajili wa vyama vya siasa ana maagizo kutoka kwa mkulu kuwa asikipe CCJ usajili wa kudumu mpaka baada ya uchaguzi. Na ukizingatia kuwa hataki kuruhusu suala la mgombea binafsi bado CCM wataendelea kupeta
 
Tambwe ni mtu ambae yuko tayari kusema lolote ili atimize na kupata ugali wake wa kila siku, sasa kali zaidi ni kua Tambwe hiza ndie mshauri mkuu wa maswala ya kisiasa wa mzee Makamba.
 
PJ.. usiwe na wasiwasi.. kwa chama kidogo kama CCJ kitapewa usajili wa kudumu mapema sana kwa sababu it is not to THE INTEREST OF KIKWETE to deny them! Kwa mtu anayetukuwa wahisani na wawekezaji.. atafanya kosa ambalo hawezi kulitetea..
 
Huu ni mwanzo mzuri, sasa wale waliobaki nao wafunge magoli ya haraka haraka kabla mabeki wao hawajajipanga sawa
 
Kuna habari kuwa msajili wa vyama vya siasa ana maagizo kutoka kwa mkulu kuwa asikipe CCJ usajili wa kudumu mpaka baada ya uchaguzi. Na ukizingatia kuwa hataki kuruhusu suala la mgombea binafsi bado CCM wataendelea kupeta
Mimi mwenyewe nina wasiwasi jamaa wasijekuharibu mchakato wa kutoa usajili wa kudumu kwa CCJ.
 
Shida ni moja. Mpendazoe hatadhoofishwa kwa namna moja au nyingine? Tumewaona wengi tangu enzi za Mwalimu wakidhoofishwa kwelikweli akina mzee Chris KasangaTumbo, yule mzee wa CHAUSTA (Mapalala), Kolimba, Bibi Titi, akina Kadego,.......
 
CCM jamani acheni mambo ya longolongo, kama hakuwahi kuongoza hata shina,kwanini mlimpa ubunge? Me najua wabunge wengi sana hata mawaziri hawajawahi hata kuongoza katika CCM.
 
Kwa tunaoiombea nchi neema huu kwetu ni mwanzo mwema, mshikamano wowote wa wezi ni hatari kwa jamii inayowazunguka hivyo kwa vyovyote vile kutoelewana kwao ni faraja kwetu. Tunaomba yatokee zaidi ya haya!! Amina.
 
Leo nilisikia kauli ya Tambwe Hiza kuhusu kuhama kwa Mpendazoe
Alisema yeye amefurahi sana kuona Mpenda zoe amehama CCM kwani alikuwa anaibana sana CCM na amesema atafurahi akisikia wale wote waliokuwa kundi moja wapinga ufisadi wakihama Chama Hicho, kwani chama kitakuwa salama na hakitakuwa na migogoro. lakini hakusema endapo wanaotuhumiwa ufisadi nao wahame. jee Tambwe anafurahia Ufisadi ndani ya CCM? jee kiongozi anafaa kuwa Mbunge? anafaaa kutuongoza?Jeee akipata nafasi hizo hatozila Fedha zetu kwa kuwa wote wataobaki CCM watakuwa kimya baada kundi ambalo Tambwe halipendi likiondoka?

kweli haya maneno yametamkwa kama ulivyo mquote ama??
 
Lazima maumivu wanayasikilizia. ukiachana na hilo huyu Mh. kawamaliza sana manake ni kama timu mnaongoza mpaka dakika ya 90 then kwenye majeruhi jamaa wanarudisha na kuongeza bao. Natumaini CCM watakuja na hoja za msingi. Subiri siku moja ambapo vijana wa kitanzania watakapoamua kukipa talaka chama hiki hilo litakuwa sio tena bao bali gharika.

True mkuu... ni kama Man U jana na Bayarn, man u walikuwa wanaongoza ugenini mpaka dakika ya 76 jamaa wakasawazisha na dk ya 90 jamaa wakaweka la ushindi. So hata mimi sijakata tamaa nadhani hata dakika ya 90 tunaweza bado kuwashinda mafisadi. Bravo Mpendazoe!
 
Back
Top Bottom