Godbless Lema avuliwa ubunge

Status
Not open for further replies.
wana jf, gazeti la mwananchi la leo tarehe 6 april 2012 limeandika godbless lema amefungiwa kugombea ubunge kwa kipindi cha miaka mitano. Je,habari hii ya kufungiwa miaka mitano ni ya kweli?



Yote ya yote utapata kesho majaliwa ktk uwanja wa NMC!

Utapata live bila chenje majibu haya kupitia JF only na kwa muda muafaka toka meza kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo!

Mhalisi!

Using'atuke kwenye mtandao kijana!
 
Ndugu mjengwa nikueleze tu kwamba utapandisha presha bure ccm haikubaliki na watanzania hawadanganyiki tena, ni lini uliwahi kuona mahkama zetu zimetenda haki na kwa udhibitisho gani? wewe kama mtanzania mzuri mwana ccm mzuri na una haki ya kugombea popote Tanzania njoo uchukue hili jimbo kwa ticket ya ccm labda unaweza kununua shimo la kukufukia, kifupi ccm tafuteni handsome au very beautiful mumsimamishe hapa arusha na msisahau kuwaleta mwaziri wote mnaowaona wazuri na wanafaa na marais,mawziri wakuu na usalama wa taifa vyombo vya dola vyote hapa Arusha nakuhakikishia kuwa wote itawezekana kabisa mkafia hapa, Arusha huyo mwingulu mchimba kaburi akaanze kuchimba kule kwao,nape yeye saizi ya Mh. Nassary

gungu.
ccm sikio la kufa, tunataka tumjue atakayewafungulia camp yao mbali ya mgombea atakayeaibika!!!!
 
Mashitaka dhidi ya Mh.Lema yalikuwa hivi:

Alimkashifu MH.Batilda Burian kwenye Kampeni zake eti Batilda ana mimba ya lowassa, Batilda ni mdini, Batilda ameolewa zanzibar kwahiyo hatakuwa karibu na wakazi wa Arusha na vile vile katika jamii za kimasai,kichagga au kimeru hawawezi kuongoza na mwanamke..!

Sasa fananisha hayo maneno juu na matutsi ya Lusinde..,

Lakini cha ajabu,..mashahidi dhidi ya lema hawalikuwa wakijichanganya kwenye kesi na kukosa ushahidi wa video au wala sauti, na vile vile mh.batilda burian wala mume wake au lowassa hawakusilisha mashtaka yeyote polisi kama wamekashfiwa wala kufungua mashtaka dhidi ya lema..!

Na ikasemekana waliomfungulia kesi wana chuki binafsi na wivu dhidi ya mh.lema

Siochuki2 mku ikumbuke baada yauchaguz ccm ilitangaza mt yeyote anayeona ameonewa hakushindwa kihalali afungue kesi na chama kitagaramia garama zakesi.hiyo haikua shida kama haki ingetendeka kweli.tatizo kesi yalema haikua nakichwa wala miguu mimi nimeifatilia toka mwanzo haikua yakumshinda lema dhahiri ilikua ya kuchongwa.nimeshangaa hukumu iliyotolewa sijui jaji ametumia vigezo gani hata kama ametumwa au kuagizwa lakini yeye amehukumu kwa vigezovipi?ila wamechemsha kwahili chadema hawatoweza kuitoa arusha hata chadema watasimamisha jiwe arusha ushindi 90%
 
haya hongreni kama ndiyo wasiwasi wangu CCM safari hii watalichukua jambo la Arusha Kamanda MKUÛ ni nchemba
 
Lema ni mbunge halali wa mioyo ya wana-arusha. Ilikuwa hivyo, iko hivyo na itaendelea kuwa hivyo. Ova.
 
nazani huku haki haikutendeka,.igunga imetendeka
Bila shaka ulitaka kusema unadhani, siyo? Hata hivyo kwani jaji ni huyo huyo? Ngoja kwanza tusubiri tuone kama Kafumu naye atautumia muda huu kuzunguka TZ kuhamasisha wana CCM katika harakati za kukijenga chama chake?
 
Duh noma sana! Mbona hapakuwa na ushahidi? je anaruhusiwa kugombea?

Wacha uvivu wa kusoma Mkuu soma update mleta habari anasema ameruhusiwa na mahakama kugombea tena na ameambiwa alipe garama za kesi na amekubali kulipa na amefurahia hukumu japo mazingira ya hukumu yalikuwa na utata Kama ushahidi etc.... Mengine angalia taarifa za habari na magazeti ya kesho mkuu
 
Lema ni mbunge halali wa mioyo ya wana-arusha. Ilikuwa hivyo, iko hivyo na itaendelea kuwa hivyo. Ova.


Uko Sawa Mkuu, Mimi nawashauri ccm badala ya kupoteza hela na muda kwenye kampeni watumie muda wao kuwaondoa mafisadi na kurudisha hela zetu zilizotoroshewa ulaya, na vyama vingine vitumie hela kujenga vyama vyao wamuache lema apite bila kupingwa na CDM nao wasiangaike kutumia hela nyingi kwenye kampeni Bali lema akawakumbushe tuu wapiga kura wake wasisahau tarehe maana hakuna asiyemjua wala wakumpinga. The guy he own the territory hakuna wa kumtoa roger.
 
Status
Not open for further replies.
29 Reactions
Reply
Back
Top Bottom