Godbless Lema aitikisa Tarime; Kagasheki adai anachochea vurugu

hiyo safi,Lema ni kamanda wa kweli! Tungekuwa na kina Lema 10 TZ sijui Tungekuwa wapi sasa.
Hapo kwenye red, saizi Tanzania ingekuwa kama Somalia, Lema Hamna kitu wewe ni Mbunge wa Arusha unakwenda Tarime kama nani? msitulete vita Tanzania:sorry:
 
Tbc kagasheki amesema amekwenda kuhamasisha fujo. Nashangaa waziri mzima anaongea udaku na tbc wanarusha. Hajui kama lema ni waziri kivuli. Kama analeta fujo si wamkamate? Poor kagasheki
 
Naibu waziri wa mambo ya ndani Balozi Kagasheki amesema kuna mbunge kutokea chama ulani na mkoa fulani yuko Tarime anachochea vurugu
MyTake...anamaanisha Mh. Lema wa Arusha ambaye yuko Tarime hivi sasa...
Source...TBC1
 
mawaziri wengine wakishashindwa kazi visingizio kibao tehe. eti na yeye waziri hovyoo kabisaaaa
 
Kuna mtu jana alitahadharisha kuwa huenda serikali ika-mbrand Lema kuwa ndiye anayechochea hizi vurugu na kweli imekuw hivo...
 
Tbc kagasheki amesema amekwenda kuhamasisha fujo. Nashangaa waziri mzima anaongea udaku na tbc wanarusha. Hajui kama lema ni waziri kivuli. Kama analeta fujo si wamkamate? Poor kagasheki
Mkuu mbona unakurupuka, hapo kwenye red ebu tuambie Katiba ya Tanzania inasemaje kuhusu hicho cheo ulichokitaja
 
tutasikia mengi mwaka huu...kila jambo ambalo serikali watakuwa wanaboronga watakuwa wanasema chadema wamechochea!....
 
Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh Hamis Kagasheki amesisitiza kuwa mbunge wa Arusha mh Godbless Lema ndiye aliyekwenda kuchochea wananchi wa Tarime kuvamia mgodi wa Morth Mara. "nilisema jana na leo narudia tena, huyu mbunge ametoka mkoani kwake na kwenda kule kuchochea fujo. Hii haikubaliki" amesisitiza
source-tbc 1
 
lema ana sababu zote za kwenda pale kama waziri wa mambo ya ndani kivuli na kujua kitu gani kinaendelea sasa anachochea vp hizo vurugu'? Kwani hyo jana wakati nyambari anapigwa kwani yeye alikuwepo uko nyamongo kauli za kagasheki sijazipenda kusema kuwa wale waliouwawa na polisi walikuwa ni wahalifu afai kuwa waziri
 
Kagasheki Muoga kashindwa Kumtaja Lema Ndie aliyenda Tarime Ati kuwa ndie anaehamasisha Fujo Nawasiwasi na Uwezo wake kifikra na Busara Hajui mtu aliyefiwa tena kwa kunyofolewa Uhai kwa Kusudi Hupatwa na Hasira.. Sasa Lema na Fujo wapi na wapi.. Na TBC Chombo cha Uma kinarusha hewani upuuzi na ukilaza wa Waziri wa Jk akiitia aibu Serikali

Yeye anastahili kwenda huko sasa anajua kuwa hatakiwi na MAgamba hayapendwi anaona gere waziri kivuli akikubalika Kagashiki ana roho ya aina yake hajaweza kulaani mauaji Kashindwa iana na JK alipoionea huruma Roho ya Osama... Sasa ya watanzania wenzake anafurahia ati wamejitakia... Sasa hizo kauli zao Zitawahukumu....

Hii nchi inajiendesha yenyewe Nimaamini
 
Kweli Huyu Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Zoba kabisa ktk Taarifa ya Habari ya Saa mbili usiku TBC1 anadai Mbunge kutoka Jimbo lingine ameenda Tarime kuhamasisha vurugu(Jimbo ambalo si lake)!!Is he serious? ina maana hajui Majukumu ya Lema kama Waziri Kivuli wa mambo ya ndani au anataka kutuaminisha Lema kaenda Tarime kama mbunge wa Arusha.Watanzania wa sasa sio wa mwaka 47 wakudanganya ovyo ovyo hii ishu inalihusu Jeshi la Polisi ambalo lipo chini ya Wizara ya Mambo ya ndani ndomana Lema yupo hapo pia Wawekezaji Barick ndomana Ester Matiko kama Waziri wa uwekezaji yupo hapo Tarime.Kagesheki yupo Dar anafungua Semina nakuongea Upupu huku akilamba posho ya Semina.Lema na Matiko wako Tarime wakitimiza majukumu yao kwakuhakisha Haki kwa waliouawa na Wananchi wa Nyamongo.
 
Mkuu mbona unakurupuka, hapo kwenye red ebu tuambie Katiba ya Tanzania inasemaje kuhusu hicho cheo ulichokitaja
<br />
<br /

Mzee ukisikia Waziri Kivuli utacheka mwenyewe japo nafasi hiyo iko nyuma ya pazia ya kambi ya upinzani.Lema ni mwehu sasa ukisikia kichaa kapewa rungu sokoni basi ujue maafa lazima yatokee.Seriously ni mchochezi mbali na hilo gamba la kivuli alilonalo,wala usidhani anapenda kuona Nchi ikitulia kwani ajira yake ni machafuko kama ilivyotokea Arusha.
 
LEMA! mbunge shujaaa saaana kwa kweli ananipa raha saaana huyu mbunge. hatuhitaji watu km kagasheki ktk zama hizi tunahitaji wabunge shujapu km LEMA. hakika haki yetu inayokandamizwa na serikali dhalinu ya CCM tutaipata very soon
 
Na mie nimesikia mkuu, kweli mfa maji haachi kutapa tapa!!! hawa wanatafuta pa kuegemea na lililotokea Tarime, wananchi sio wapumbavu kiasi cha kusukumwa na mtu yeyote kufanya fujo...
 
lema ana sababu zote za kwenda pale kama waziri wa mambo ya ndani kivuli na kujua kitu gani kinaendelea sasa anachochea vp hizo vurugu'? Kwani hyo jana wakati nyambari anapigwa kwani yeye alikuwepo uko nyamongo kauli za kagasheki sijazipenda kusema kuwa wale waliouwawa na polisi walikuwa ni wahalifu afai kuwa waziri

kinachomsumbua kagasheki na serikali yake ni hofu na woga dhidi ya chadema ambacho kinatikisa nchi nzima.
 
Mkuu hii taarifa ni nzuri ila iweke vizuri basi tuichambue kwa kina.
Mbunge wa arusha mjini na waziri kivuli wa mambo ya ndani akiwa ameambana na mbunge wa vitimaalum chadema ester matiku leo walitembelea tarime kwenye yale mauaji ila kabla hawajaenda huko walienda kwanye ofisi za mbunge wa jimbo hilo na kuwachwa mdomo wazi pale mbunge wajimbo hilo na watendaji wake walipo kimbia ndipo lema na matiku wakaamua kwenda kwa mkuu wa wilaya napo huko walikutana na vizingiti

ila lema akamlazimisha mkuu huyo wa wilaya kumpa taarifa za awali ndipo mkuu huyo alipo ropoka na kusema hawa wananchi ni wajinga sana walistahili kuuwawa na lema akamjibu nashukuru sana hii itakuwa nimoja ya taarifa zangu.

lema na msafara wake ukawa unaelekea kwenye eneo la mauaji ndipo wakakutana na kundi kubwa la wananchi watarime wakamzuia lema na kusababisha umati mkubwa sana na wakamlazimisha lema kuhutubia ndipo lema alipo anzakuongea nao na baada ya hapo walimlazimisha lema kufanya maandamano ndipo lema alipo kataa kuepusha vurugu zaidi na hivyo lema akashindwa kuendelea na safari yake ya ukaguzi, kamanda LEMA alikuwa akitokea JIJINI MWANZA

Naikumbukwe pia LEMA ni waziri kivuli wa mambo ya ndani so alikuwa ameenda kutembelea eneo la tukio na ndipo alipo amua kufuata hizo taratibu kwa kumfuata mbunge wa jimbo hilo ili amueleze kilichotokea ndipo walipo ingia mitini .

SOURCE JF
 
Kagasheki (kwa kihaya) as his name implies - its meaning is 'useless' au hakatoshelezi.
Kagasheki aina amaela kyonka, kama walivyo wafanya biashara wa CCM.
 
Kagashek ametoa kauli tata kuwa waliouwawa Tarime walikuwa wahalifu lakini serikali imetoa msaada wa mazishi. je serikali imeanza lini kuoa msaada kwa waharifu? Amepima kauli yake kweli au ndio sias za Tanzania?
 
wamechanganyikiwa kwa hyo wewe kagasheki nini unataka kufanya juu ya mh lema na ghati matiki? Acheni mambo ya ajabu hapa huo mgodi siume mwaga maji ya sumu kwenda kwenye mito na watu wanekunywa maji yake wamebabuka ngozi serikali ilichukua hatua gani dhabiti? Mifugo mingapi ilipoteza maisha? Mmesha toa tamko juu ya utafiti wenu na wananchi wakaona kama ni kweli mmechukua hatua? Ww kagasheki acha kabisa kauli zako nazikemea
 
Back
Top Bottom