Gilrs talk...strictly not för men.

cheusimangala

JF-Expert Member
Feb 27, 2010
2,585
497
wasichana wenzangu amani ya Mungu iwe juu yenu.
Kuna habari fulan mtu kanieleza imepelekea niamue kuwashauri juu ya hili.
Ni hivi,
Nawashauri kama una rafiki yako mnapendana kiasi cha kuwa kama ndugu mnaoshirikiana na kusaidiana katika mambo mabalimbali,usihamie na kukaa naye nyumba moja sababu utampoteza.

Najua wengi wanafikiri itakua raha zaidi kama yeye na rafiki yake wanayependana watakaa katika nyumba moja lakini wanakua wanakosea sababu uchunguzi wangu unaonesha wengi wanaishia kugombana.

Hii ni kwa wale wenzangu na mie ambao bado hawajaolewa,wanaoishi peke yao.

SABABU ZA MIM KUPINGA MARAFIKI KUISHI NYUMBA MOJA NI HIZI;

..mkiishi mbalimbali mtakua mna hamu yakukutana kila mara lkn mkiishi pamoja mtagunduana madhaifu yenu hivyo kufanya mkinahiane.

..kila binadamu ana utashi wake,wewe unaweza kuwa uko very organized lkn mwenzio akawa haoni hatari kutotandika kitanda au kutupatupa nguo kila mahali jambo ambalo litakua litakua linakukera na kwa vile yeye ndio tabia yake hata ukimweleza anaweza akarudia hivyo lazima tu mwishowe utakua unanuna nuna na yeye ataona unamfanyia visa kwa kununanuna bila sababu na hapo upendo wenu utakua umepungua.

..mkihamia pamoja mtachanganya vitu venu,hapa kuna hatari ya mmoja wenu kuona vitu vyake mwenzie havithamini vinaharibika.Hii nishasikia watu
wengi wakilalamikia.
.
..Mkiamua kukaa pamoja lazima mtataka kushare gharama za kula na vitu kama hygienic materials,hapa kuna mmoja anaweza kuona yeye anagharamia zaidi ya mwenzake na kwa kuwaza hivi upendo utapungua.

..Pili wewe unaweza kuwa mtu wa kutumia vitu kwa ubahili kwa lengo la kusave pesa kwa maendeleo yako,mwenzio anaweza kuwa ni yule sabun anamimina kwenye mashine hadi nguo haziishi povu hapo lazima wazimu ukupande kichwani.

..mkiishi pamoja lazima msaidiane kazi kama vyombo na kusafisha nyumba lakini mwenzio anaweza kukutegea na hutafurahia au wewe unaweza ukawa majukumu yamekuzidi ukashindwa kumsaidia kama sio muelewa hatafurahia.

..ikitokea mmoja pesa zimekata kwa muda ndio hapo utata unapozidi maana yule anayegharamia ataanza kuona kama vile anakulea japo wakati mlipokua mkiishi mbalimbali alikua hasiti kukukopesha au hata kukusaidia bure.

..nyote ni watu wazima hivyo kila siku kumrekebisha mwenzio ni jambo ambalo hatalifurahia,au kama ni wewe kila siku unaambiwa sipendi ufanye hivi sipendi ufanye vile lazima utajiona huna uhuru.

Kwa kweli nimeshuhudia marafiki wengi waliokuwa wakipendana sana wakiishia kukorofishana baada ya kuwa wanaishi pamoja,kila mmoja anaondoka akimuona mwenzie mbaya lkn ukweli ni kwamba hakuna mbaya kati yao ni hali halisi tu.
Wenzetu wanaume naona wanaurahisi wakuishi pamoja na kuelewana lakini sisi katika hili asilimia kubwa linatushinda.

Halafu kama mmoja ana mtoto mmoja hana ndio inakua balaa lkn kama nyote mna watoto ndio balaa zaidi.

Ni rahisi kwa mwanamke kuishi na mwanaume 8mume)hadi kifo kiwatenganishe na wakaelewana japo kutoelewana kwa hapa na pale kupo lkn mwanamke kuishi na mwanamke mwenzie(rafiki) inaishiaga vibaya LKN PIA NAFAHAMU MARAFIKI WALIOFANIKIWA KUISHI PAMOJA NA WAKAZIDI KUPENDANA NA LEO WAMEOLEWA HAWAITANI MARAFIKI BALI WANAITANA SISTERS

HIVYO USHAURI WANGU NI KWAMBA MSIISHI NYUMBA MOJA NA MARAFIKI ZENU MTAWAPOTEZA.

with love.:A S-rose:
 
najaribu kubadili hiyo gilrs kwenye heading iwe girls lkn sijui kwa nini inakataa.
nadhan mmeelewa namaainisha girls...
 
Unachotaka kusema ni kuwa wanawake wanachukiana au nimelewa vibaya? samahani nilikuwa napita njia tu
 
tatizo mademu hamna upendo wa kweli na urafiki wa kweli kwa mademu wenzenu.lol
 
Unachotaka kusema ni kuwa wanawake wanachukiana au nimelewa vibaya? samahani nilikuwa napita njia tu

sijamaanisha kuwa hatupendani,
bali nimesema tu kuwa wanawake kwa wanawake kuishi pamoja sio rahisi.
Mim napenda kusema ukweli,na nilichokisema ni kweli,hata ndugu wa kike wanaoishi pamoja kwa wazazi hugombana kila siku lkn sio kama hawapendani.
 
utakuwa unawashwa wewe!!

mbona unanichukia hivyo jamani????
maana sio mara ya kwanza unanitukana,matusi yako kwa kweli huwa hayanisumbui ila kwa vile mim nakupenda huwa ukinitukana hivi naishia kukuonea huruma sababu una dalili za mtu asiye na furaha na maisha yake.
Watu wasio na furaha na maisha yao hutafuta relief kwa kujaribu kuwakosesha wengine furaha.
Kama kuna nilipokukosea naomba uniambie nitakuomba msamaha maana mie napenda amani na kila mtu.
VILE VILE KAMA KUNA KITU KINAKUSUMBUA KATIKA MAISHA YAKO HADI UNAKUA BINADAMU MWENYE HASIRA HASIRA FEEL FREE KUNIANDIKIA PM UNIAMBIE NI KIPI HAKIJAKAA SAWA KTK LIFE YAKO THEN SABABU MIM NI MWINGI WA UPENDO NAWEZA KUKUSAIDIA.
nitafurahi sana kukusaidia sababu unaonekana unahitaji msaada.
 
Mhhh naomba kupingana na wewe kidogo maana nna rafiki yangu nilikaa nae karibu miezi nane yani hata nikisafiri tu kwa wiki wote tunasikitika...na siku naondoka kabisa ndo usiseme mpaka chozi alidondosha!!
Matatizo yake yalikua yangu na yangu yake....akiwa hana tunatumia changu nikiwa sina tunatumia chake!!Mpaka sasa hivi najua nna sehemu yangu nyumbani kwake na wakati wowote nakaribishwa bila hata kuuliza!!

Kusema ukweli tunaendana sana kwasababu tabia zetu nyingi zinafanana na vile vitu ambavyo tunatofautiana tulijifunza kuvikubali.Kwa mfano nakumbuka mimi kuna siku aliniboa sikuongea nae kutwa kwahiyo na yeye akakasirika sana....mwishoni tukabuni kasystem ketu kwamba nikikasirika kama sitaki kuongea kwasababu najua hasira itaongezeka na badala ya kusubiria masaa ishuke ili niweze kumwambia nini tatizo namwandikia ananijibu tunayamaliza!!

Kwahiyo cha muhimu ni maelewano tu...ukishindwa kuishi na rafiki wa kike hata mwanaume huko mbeleni itakua ngumu tu.Kua muelewa...kubali madhaifu ya mwenzako ikibidi msaidie...usiwe na kinyongo au wivu kwake....usiwe mmbea yani akikwambia mambo yake sio unatangazia kila mtu...kua mstaarabu na usiwe mnafiki!!
Kama mnapendana kweli hata mtu mwingine akiingilia kati hawezi kuwagombaisha...najua hili maana lilitokea kwetu na bado tuko gado!:grouphug:

BTW waombe mods wahamishie hii thread MMU watu ili hata wasiopita huku waweze kuchangia ...pia inahusiana na mahusiano kwahiyo itafit kule!!!
 
@lizzy,
hujanipinga bali umekubaliana na pale niliposema kwamba wapo baadhi wanaweza kuishi vizuri bila shida,
rudia kusoma utaona mahala nimetoa mfano kuwa nafahamu wadada waliishi pamoja bila shida leo wameolewa hawaitani friends wanaitaka sisters.
Hata mim ktk maisha yangu nimekaa na marafiki lkn hakuna niliyeachana naye kwa ubaya,na wengi wao ni kama ndugu zangu kwa sasa,mm sijui kumnunia mtu na ni mwepesi wa kusamehe.
Ila nimeshuhudia wengi wakiishia kwa ubaya kwa sababu ndogo ndogo kama hizo nimetaja hapo juu,na ndio maana kama umenisoma vizur pia nimesema 'wanapotengana kila mmoja wao humuona mwenzie mmbaya lkn hakuna mbaya kati yao'
kuishi na watu ni sanaa inayohitaji uvumilifu na uelewa kuwa hakuna mkamilifu na mm nawashukuru wazazi wangu wamenilea kwa misingi ya kuelewana na kila mtu wa kila aina,leo hii ukigombana na mm watu wote wanaonifahamu watasema wewe ndio mbaya sbb hawajawahi kuniona nikigombana na mtu.
Ila pia sikubalin na ww kuwa mwanamke asiyepatana na wenzake hatapatana na mumewe,nawajua wengi wamezungukwa na maadui na faraja pekee aliyo nayo ni mumewe.
Tena ni wazuri wakumshawishi mumewe kuona kuwa yeye ndiye anayeonewa,kumbe usikute yeye ndiye hajui kuishi vizuri na watu.
 
mbona unanichukia hivyo jamani????
maana sio mara ya kwanza unanitukana,matusi yako kwa kweli huwa hayanisumbui ila kwa vile mim nakupenda huwa ukinitukana hivi naishia kukuonea huruma sababu una dalili za mtu asiye na furaha na maisha yake.
Watu wasio na furaha na maisha yao hutafuta relief kwa kujaribu kuwakosesha wengine furaha.
Kama kuna nilipokukosea naomba uniambie nitakuomba msamaha maana mie napenda amani na kila mtu.
VILE VILE KAMA KUNA KITU KINAKUSUMBUA KATIKA MAISHA YAKO HADI UNAKUA BINADAMU MWENYE HASIRA HASIRA FEEL FREE KUNIANDIKIA PM UNIAMBIE NI KIPI HAKIJAKAA SAWA KTK LIFE YAKO THEN SABABU MIM NI MWINGI WA UPENDO NAWEZA KUKUSAIDIA.
nitafurahi sana kukusaidia sababu unaonekana unahitaji msaada.

mmh, jamani umejibu kwa upole hadi najisikia hatia kwa kejeli niliyokurushia. naomba unisamehe na nitaku-PM tuyamalize

peace
 
mmh, jamani umejibu kwa upole hadi najisikia hatia kwa kejeli niliyokurushia. naomba unisamehe na nitaku-PM tuyamalize

peace
Huu ndio uungwana
Na kuongezea ni kuwa kama mtakuwa machured kuna uwezekano mmoja akiwa na boyfriend basi kuna uwezekano ikawa balaa zaidi.Boyfriend akimkosa mtu wake akataka kujua yuko wapi GF kwa mwenzie basi inaweza kutafsiriwa unataka ku-take over au kuua ndege wawili kwa jiwe moja hiyo inakuwa mgogoro.
 
Kweli cheusi, nimeishi hosteli nimeona hicho kitu.
Sio tu marafiki, hata ndugu unapokaa nae karibu lazima kutakuwa na vimigogoro kama hivyo. Jambo la msingi sio kuepuka kukaa na rafiki bali ni kujua madhaifu yake na kujitahidi kumrekebisha kivitendo. Mfano, unaweza ishi na mtu halafu swala la kusafisha vyombo kwake ni gumu. We fanya hiyo kazi, tena bila kumwambia chochote ipo siku ataanza kuona aibu na atajirekebisha au wakati we unafanya hiyo kazi yeye anaweza kuwa anafanya kazi nyingine ya usafi kwahiyo mpangilio wa kazi ukaenda sawa.
 
Duh yaani Cheusi umenikumbusha mbali sana. Nakumbuka semister ya tatu chuo niliishi na shoga yangu mmoja, kwa kweli ni ngumu sana ukizingatia kila mtu kakulia kivyake. Tulikuwa tunapika kwa zamu, ikifika zamu yake visingizio haviishi kumbe maskini alikuwa hapendi kupika na mimi kupika napenda saana. Basi tukakubaliana awe anaosha vyombo mie napika, duu hali ilikuwa mbaya manake vyombo hadi siku inaisha havijaguswa, au vinalipuliwa hadi karaha. Ili kuokoa jahazi semister iliyofata kila mtu akaishi kivyake.

Please usiishi na rafiki wako wa karibu maana ni ngumu kuvumilia madhila kitu kinchoweza uhatarisha urafiki wenu.

Thanx sana dada Cheusi.
 
Duh yaani Cheusi umenikumbusha mbali sana. Nakumbuka semister ya tatu chuo niliishi na shoga yangu mmoja, kwa kweli ni ngumu sana ukizingatia kila mtu kakulia kivyake. Tulikuwa tunapika kwa zamu, ikifika zamu yake visingizio haviishi kumbe maskini alikuwa hapendi kupika na mimi kupika napenda saana. Basi tukakubaliana awe anaosha vyombo mie napika, duu hali ilikuwa mbaya manake vyombo hadi siku inaisha havijaguswa, au vinalipuliwa hadi karaha. Ili kuokoa jahazi semister iliyofata kila mtu akaishi kivyake.

Please usiishi na rafiki wako wa karibu maana ni ngumu kuvumilia madhila kitu kinchoweza uhatarisha urafiki wenu
.
Thanx sana dada Cheusi.

u r welcome.
nimefurahi umetoa mfano hai.
Mi huwa nawaangaliaga watu wanahamia kwa mbwembwe pamoja lkn haviishagi vizuri.
hapo pink ndo hasa point yangu,nashukuru umeniunga mkono.
Nina imani utakua umejifunza mengi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom