Ghorofa la Bernald Membe - Wizi Mtupu

Mkuu ulieleta hii thread,nadhan ingekuwa vyema ukatuwekea vielelezo vya ushahidi wa umiliki wa ghorofa.
Kama great thinker ni vyema kufanya hivyo ili kuondokana na hisia kwamba hii ni siasa ya kuchafuana bila kuwa na ushahidi wowote,leo hii mtu anaweza piga picha gorofa moja arusha na kusema la fulani ili tu kupanda mbegu ya chuki kwa wananchi.
Otis

Nimekuwepo eneo lenye ghorofa mara mbili na picha sijapewa nimepiga mwenyewe baada ya kuongea na majirani na baadhi ya informer kutoka VETA. Majina anayotumia kwenye usajili wa hilo jumba si yake bali amemtumia mtu kama wachangiaji wengine walivyosema. Mimi si mtu wa ardhi ila elewa kwa asilimia 100 hilo ghorofa ni la Membe na lipo kwenye hatua za mwisho kabisa kukamilika
 
aaa kawaida tu, kwa hyo akiwa waziri ndo asifanye chochote cha kutumia pesa kwa maendeleo yake? Acha unyerere!!!!
 
Huyu Membe hiyo ni hotel yake kweli. na ana nyingine iko karibu na standa ya mabasi Mtwara inaitwa NAF BLUEVIEW
Pia pale Lindi anataka kumpora mzee mmoja ile Lindi Oceanic hotel ambayo mzee huyo alinunua kwenye mnada kihalali uliofanywa kwa niaba ya CRDB.

Naogopa hata kumuita Mheshimiwa maana matendo yake huku kusini wala hayafanani na cheo chake. Nasubiri M4C waje kusini niwauzie hili gazeti

Mkuu unauthibitisho juu ya membe kumiliki NAF BLUE Hotel?Una kithibitisho chochote?
 
nimefuatilia majadiliano yote! Ninachojiuliza ni watz wangapi ambao wangepata nafasi km alizopata membe wasingefanya hicho ambacho amekifanya! Ok,membe kuwa na mali sioni kosa hapo,tatizo hapo ni kwamba kapataje? Tupeni ushahidi kwamba kajenga ghorofa hilo kwa ufisadi hapo ndipo patakuwa na shida!
 
Endelea kubakia na utomaso wako hupati vielelezo vingine zaidi ya hii picha ya kweli. Kama unataka kujua ukweli zaidi kwea ndege nenda Mtwara maeneo ya VETA mita kama 100 kutoka bahari ya Hindi

Nzuri sana,msaidie kijana kujenga imani yake.lol!
 
Hili ni ghorofa linalokamilika kwa spidi la Mh. Bernald Membe pale jirani na VETA Mtwara ambapo pia alitaka kukitwaa kiwanja cha VETA ili apate parking. Hapa anajenga hoteli na sitaki niseme ni ghorofa ngapi we hesabu mwenyewe.

Kwa wale wasiojua fedha zetu walipa kodi zinakokwenda hadi watoto wa shule kukalia mawe darasani kwa kukosa madawati na wagonjwa kulala sakafuni kwa kukosa vitanda basi jioneeeni wenyewe. Wafanyakazi mnaokatwa kodi mlikuwa mnauliza zinakwenda wapi basi jioneeni wenyewe ndio hapa zimehifadhiwa kwenye hili ghorofa.

Mtu akibisha anieleze ana basis zipi kwani mi ninao ushahidi wa hii picha.

attachment.php

Ujenzi ukiendelea wa ghorofa la Bernald Membe: Waziri wa Mambo ya nchi za nje eneo la VETA Mtwara
a.k.a. BLUE VIEW Hotel. Ila pamoja na hayo wanatubadilishia ka-mji ketu ka Mtwara, maana walikasahau...! Soon after 6th June this year mradi mkubwa wa ujenzi wa barabara kutoka Magomeni (junction ya kwenda Newala au Airport) kuja Shangani, kupitia mbele ya mjengo huo, utaanza. Mkandarasi D.B. Shapria ameshatia timu maeneo...! Sasa sijui na hapa tusemaje..!? Ni kampeni za kifisadi au..?
 
TATIZO lako labda hufahamu Kiswahili au hamnazo vinginevyo, ungeona niliyoyaandika nimesema "INASEMEKANA" kwahiyo kama ni ujinga basi wewe ndie MJINGA zaidi ambae huijui hata lugha yako. But all in all, main point hapo ni kuhusu lini Membe ameanza kuwamo serikalini. Binafsi sipendi kujitia upuuzi wa kujifanya nawafahamu vigogo wa serikalini vinginevyo wala nisingesita kufanya hivyo hususani kuhusu Membe.Membe yupo kwenye system zaidi ya miaka 30 na hiyo ndiyo hoja ya msingi. Na huyu wakati wote amekuwepo kule kule jikoni tofauti na wengine ambao walikuwa mara katibu wa chama, mara chipukizi mkuu.
Umemaliza mkuu, it is just a matter of using common sense. Ukiwa unabishana na mtu wa aina hii, face to face, inabidi umkalie mbali maana anaweza kukuogesha mate...
 
weka huo ushaidi mvumbuzi kwani hapa jf pia ni public na pia ni chombo cha habari hakuna haja ya kwenda habari maelezo. tupia mzigo huo hapa wanahabari watachukua kutoka jf

Ushahidi ni hiyo picha ya jengo lake ambayo nimeipiga mimi mwenyewe. Maelezo ninayoyatoa nimepewa na majirani na nimepata fursa ya kutembelea eneo lenyewe several time ku-confirm. Kusema niweke ushahidi ni kupoteza muda kwani hata registration hawezi andika jina lake anajua kabisa fedha za kujengea siyo za halali na hivyo kuficha mambo lazima ajifiche nyuma ya jina la mtu anayemwamini sana. Unajua mwizi hawezi pita mtaani akijitangaza kwani anajua anachofanya ni kinyume cha sheria; similarly hutakuta mahali hati ya hilo jengo imeandikwa jina la Bernald Membe
 
a.k.a. BLUE VIEW Hotel. Ila pamoja na hayo wanatubadilishia ka-mji ketu ka Mtwara, maana walikasahau...! Soon after 6th June this year mradi mkubwa wa ujenzi wa barabara kutoka Magomeni (junction ya kwenda Newala au Airport) kuja Shangani, kupitia mbele ya mjengo huo, utaanza. Mkandarasi D.B. Shapria ameshatia timu maeneo...! Sasa sijui na hapa tusemaje..!? Ni kampeni za kifisadi au..?

Mawaiba kumbuka kwamba hii barabara inayokatiza hapa VETA Mtwara ikiamba ambaa na bahari ina vigogo wengi akiwemo Hawa Ghasia a.k.a shemejie Mkulu kwa hiyo wameamua kujitengenezea barabara za kwenda nyumbani kwao na haswa hiki kitega uchumi cha FISADI
 
Acheni ujinga jenga kwenu, kumbuka huyu ni Waziri wa Mambo ya Nje sio kapera kama wewe. Anazo resources nyingi na advantage nyingi sasa unataka pesa zake akahonge baa au unataka nini. Ni lazima tumuunge mkono ili amalize nyumba yake itoe huduma inayo kusudiwa sio mawazo ya kimasikini unataka nai aje kujenga Tanzania ... mpuuzi wewe
 
Naomba Dr. Slaa na Mbowe waje na list ya mali zao tuzione!!!!

Pili hivi Zito Kabwe kumiliki Hammer la milioni 500 sio ufisadi wa hela yangu ya kodi????

Nimefurahi, membe ni mzalendo, hotel itasaidia kuinua kipato kwa wana- Mtwara, mji uapendeza na ajira itapatikana!!! Mlitaka aje kujenga Moshi????

Alaf ni muungwana, hajajificha, ni muwazi... Wapi Lowasa na Sumaye, lete mali zao tuzijuwe!!!!!!

Hili ni ghorofa linalokamilika kwa spidi la Mh. Bernald Membe pale jirani na VETA Mtwara ambapo pia alitaka kukitwaa kiwanja cha VETA ili apate parking. Hapa anajenga hoteli na sitaki niseme ni ghorofa ngapi we hesabu mwenyewe.

Kwa wale wasiojua fedha zetu walipa kodi zinakokwenda hadi watoto wa shule kukalia mawe darasani kwa kukosa madawati na wagonjwa kulala sakafuni kwa kukosa vitanda basi jioneeeni wenyewe. Wafanyakazi mnaokatwa kodi mlikuwa mnauliza zinakwenda wapi basi jioneeni wenyewe ndio hapa zimehifadhiwa kwenye hili ghorofa.

Mtu akibisha anieleze ana basis zipi kwani mi ninao ushahidi wa hii picha.

attachment.php

Ujenzi ukiendelea wa ghorofa la Bernald Membe: Waziri wa Mambo ya nchi za nje eneo la VETA Mtwara
 
Tuache mawazo finyu na fitina zisizo na mipaka kwa kila anaefanya maendeleo kama haya! Kwanza kawekeza nyumbani! Pili vyanzo vya fedha za miradi kama hii vipo vingi! Kwa mtu aliyevuka mipaka ya Nchi yetu kama yeye anao ufahamu mkubwa wa kupata uwezo huo! Tusiwe kama mbuzi anaeishia urefu wa kamba yake! Tujue pia mbuzi wengine hawafungwi wako huru!Sio kila kitu unaangalia mshahara tu! Mtu hatajiriki kwa mshahara! Watanzania wengi hawajajua siasa zimebadilika! Sasa ni Uwekezaji tuu!Na ukiona mtu kafanikiwa usianze kupigia panda kodi yako! Kwanza anaepigia panda kodi wala si mlipa kodi mkubwa! Kila zama na vitabu vyake! Kwa mwendo huo tutatawaliwa tena upya na Wazungu! Mbona hatuwapigii kelele wazungu wanaowekeza hadi Bongo kuwa ni wezi?Tuondoe Bifuu!!!
 
Tafuta vyako mkuuu....
Anamiliki jasho lake, juhudi zako ndio mafanikio yako.... Acha stori za vijiweni!!!!
Bana wewe? Wenye kubisha wabishe lakini hilo ghorofa na hoteli ya NAF BLUE VIEW iliyoko stand ni vya Membe. Subiri tutaomba picha ya nyumba zake zilizoko dubai na kanada kisha tutawawekea. Ghorofa na hoteli ya naff blue hotel vimeandikwa jina la shaibu lakini mali ni za membe. shaibu tunamjua nadani na nje alikuwa akiuza simu na haouse za simu hana uwezo huo. binafsi nimewahi kumdodosa shaibu na alikiri kuwa ni mali za membe. you may take it.
 
Nachelea kuwa miongoni mwa watu wa ajabu kuweka msimamo kwamba Bernard Membe sio mwizi/fisadi kwavile simfahamu Membe vizuri kama ninavyojifahamu mwenyewe.Vilevile, nachelea kuwa miongoni mwa watu wa ajabu ku-conclude kwamba Membe ni mwizi/fisadi; kwa ku-base kwenye ujenzi wa hiyo hotel peke yake. Awali ya yote, nina-assume kwamba hilo jengo kweli ni hoteli ya Mheshimiwa Bernard Membe.Kwanini nachelea ku-conclude kwamba Membe ni mwizi kwa kuangalia tu hilo jengo?! Awali ya yote, jengo hilo si la kutisha sana kwa kuzingatia muda aliokuwapo Membe kwenye system. Bernard Membe amekuwepo kwenye system tangu alipomaliza tu masomo ya sekondari.....narudia, amekuwepo kwenye system hata kabla hajagusa chuo kikuu! Inasemekana kwamba, Membe alisoma shule ya Seminary, bila shaka ilikuwa ni one step forward kuwa mtumishi wa mungu. Aidha, inasemekana kwamba, siku ambayo alitakiwa kuapa ili aingie rasmi kwenye masomo ya utumishi wa mungu, Bernard Membe aligoma kufanya hivyo. Bila shaka alijiona hakuwa na wito wa kuwa mtumishi. Hakutaka kuwa mnafiki kama wengine wanaoingia huko na kufanya mambo yaliyo kinyume kama vile kuwa na vimada wakati ni jambo lisilokubalika kwa upande wa dini yoyote achilia mbali Ukatoliki ambao hahuruhusu hata kuona.Aidha, inasemekana kwamba siku hiyo ya kiapo hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerer nae alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa! Hivyo basi, baada ya Membe kugoma kuingia kwenye utumishi, Mwalimu Nyerere akakata shauri la kumchukua dogo (Membe)!! Hivyo basi, tangu hapo Membe akaingia kwenye system.Hata alipoingia UDSM, tayari Membe alikuwa ndani ya CCM! Ikumbukwe kwamba, hayo ya kuingia kwenye system ilikuwa miaka ya katikati ya 70, which means ni more than 30 years now.Baada ya kuchukua shahada ya International Relation pale UDSM (i think miaka ya mwisho ya 70, au mwanzoni kabisa ya 80) Membe akazidi kupaa zaidi. Na miaka ya mwanzo ya 80 akapelekwa ubalozi wa Canada ambako nako alikaa muda usiopungua miaka 5. Aliporudi toka Canada, mwaka 2000 akagombea ubunge wa Mtama na tangu wakati huo hadi leo amekuwa mbunge na waziri (Uwaziri since 2005)!! So, kwa kuangalia mlolongo huo, wala sichelei kutamka wazi kwamba uwezo wa kujenga jengo kama hilo anao hata kama ni kwa mkopo!

Mimi nasema hata kama si kwa mkopo.
 
Tuache mawazo finyu na fitina zisizo na mipaka kwa kila anaefanya maendeleo kama haya! Kwanza kawekeza nyumbani! Pili vyanzo vya fedha za miradi kama hii vipo vingi! Kwa mtu aliyevuka mipaka ya Nchi yetu kama yeye anao ufahamu mkubwa wa kupata uwezo huo! Tusiwe kama mbuzi anaeishia urefu wa kamba yake! Tujue pia mbuzi wengine hawafungwi wako huru!Sio kila kitu unaangalia mshahara tu! Mtu hatajiriki kwa mshahara! Watanzania wengi hawajajua siasa zimebadilika! Sasa ni Uwekezaji tuu!Na ukiona mtu kafanikiwa usianze kupigia panda kodi yako! Kwanza anaepigia panda kodi wala si mlipa kodi mkubwa! Kila zama na vitabu vyake! Kwa mwendo huo tutatawaliwa tena upya na Wazungu! Mbona hatuwapigii kelele wazungu wanaowekeza hadi Bongo kuwa ni wezi?Tuondoe Bifuu!!!

Aaaah na wewe hiyo Avatar yako vipi? Kama unavunja sheria ya haki miliki na hati miliki!
 
well, kama Benard hana kashfa nyingine, hiki kijighorofa nakiona kibanda tu... kuwa kiongozi haina maana uwe maskini!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom