Ghasia acha kudhalilisha Taifa; Kuwa Mwelewa

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,421
85,857
Jana usiku kwenye Taarifa ya TBC walimhoji Hawa Ghasia kuhusu bajeti yake hasa hasa suala la salary; katika mahojiano yale mafupi nilipata mambo kadhaa ambayo yalinitia kichefuchefu kumuona mtu mwenye dhamana kubwa kiasi kile akiongea kama mtu alielewa mnazi, gongo au boha (anisamehe kwa kutumia lugha hio).

Kwanza aligoma kutaja ni kiasi gani kimeongezwa (sio muhimu hata hivyo) kwa madai kwamba eti watu wakijua kuwa mishahara imeongezwa basi bidhaa zitapanda bei (first crap). My take; yaani tunaishi dunia ngapi au kuna dunia ngapi kati ya wafanyabiashara na Watumishi hadi wasijue kuwa mishahara imepanda? Pili, kinachopandisha bidhaa ni kuongezwa kwa mishahara au ni kitu kingine? Tatu; kwa mfanyabiashara suala ni kujua kuwa umeongezwa tu, yeye haaangalii umeongezwa kiasi gani kwasababu hata hivyo hizo nyongeza hutofautiana sana (kama ni kweli lakini kuwa bidhaa zinapanda kutokana na salary kuongezwa). Nne, kulikuwa na haja gani sasa kusema kuwa fungu la mshahara limeongezwa na at the same time ukisema kuwa ni siri kusema kuwa mishahara imeongezwa? Ni siri kwa nani, wapi na lini?

Jambo la pili (2nd Crap); "Wezi" wa nyaraka za serikali na kuzitumia kama evidence ni ukosefu wa uzalendo/utaifa; ok, sina tatizo na hilo ila dai lake kwamba Vijana wengi (nadhani hapa alikuwa akirejelea Wabunge vijana) hawana uzalendo kwa kuwa wanaenda Wizarani kuomba documents za "SIRI". My Take; Which is Good? Kuzichukua hizo documents na kuzitumia kuikosoa serikali kwa manufaa ya nchi (kama wabunge hao vijana wanavyofanya) au nzuri ni ile ya akina fulani wachache kuzichukua taarifa hizo na kwenda kuanzisha mashirika hewa akina deep Green, Kagoda na mengine ili kukwapua mabilioni ya Watanzania? Hapa napo nikamuona huyu Mama ana tatizo mahali fulani...........

Hoja ya mwisho ambayo ni mwendelezo wa hio hapo juu; Vijana hawa wanakosa uzalendo kwa sababu hawakwenda JKT..........hapa ndipo nikataka kulia kumuona Waziri akiongea kama Mlevi wa Mnazi au Chang'aa; Ni uzalendo upi anaouzungumzia? Wa kutokuikosoa serikali? Wa kukaa kimya? Aaah; lakini akisahau kuwa wale wote na walio wengi walioburuzwa mahakamani kwa jitihada za wabunge wa chama fulani wale ni wazeee ( akina mawaziri wale na akina fulani), Je Mh. Lowasa, Chenge na Rostam wenye kashfa kadhaaa (sijui kama ni za kweli au la, lakini wana kashfa) nao ni vijana? au wale ndio Wazalendo? Hebu atuambie ni Vijana wangapi (ukiacha wenye kesi za kuiba kuku, simu n.k na kesi za kubambikiwa) wana kesi leo mahakamani zinaotishia uhai wa Taifa? Je sio wazee hao ambao unadai ni "Wazalendo kwa kuwa wamepitia JKT? Ni Vijana wangapi ambao walisaini mikataba yenye kuigharimu Nchi yetu kiasi hiki? Hapana mama, umekosea bana.

Hitimisho; kama kweli vijana si wazalendo kwa kuwa hawajapitia JKT, je tunawezaje kuwaachia na kuwaamini, na kuwaweka kwenye Idara Nyeti kama Usalama wa Taifa letu (wengi ni Vijana), Jeshi la Kulinda Nchi (wengi ni vijana) na taasisi nyingine nyeti ikiwa ni pamoja na usalama wa Ikulu na BOT?

Well, unataka JKT irudi, sina tatizo na hilo, lakini umeshaona cost ya kuwaingiza kwenye mafunzo Vijana hawa kisha wakimaliza hawana ajira? Nyie mmetulia kwa sababu mlipomaliza mlienda kazini na kwa wale ambao hawakwenda ilikua ni kwa sababu binafsi....leo mmeshindwa kutengeneza ajira, halafu hawa vijana mnaenda kuwapa mafunzo, hahaa hahaaaa sijui kitakuja kutokea nini, hata sijui. Hebu wapelekeni fasta ili tuweze kuona yale ya Misri na kwingineko yakitokea pia. Haya ni mawazo na mtazamo binafsi, hauna ushabiki na chama chochote cha Siasa.

Mungu Baba, tubariki sisi wanano, tunatubu kwa kukosea kuwachagua Viongozi wasio Viongozi.
 
Back
Top Bottom