Gharika CCM: Viongozi na wanachama 1,005 wahamia CHADEMA Kagera

katika uchaguzi wa 2010 wanachama wengi wa CCM ndio walioipigia kura chadema sababu zilizo wasukuma kuipigia kura sijui ni kuchoshwa na chama chao au imani? wao wanajua zaidi, lakini sasa wanaamua kuachana na chama chao na kujiunga rasmi na CDM, kwa hiyo kinachofanyika sasa ni wanachama wa CCM ambao ndio walioiwezesha kupata kura 2200,000 sasa wameamua kujivua gamba na kujiunga CDM, kwa hiyo katika uchaguzi ujao chadema wasipofanya uchunguzi vizuri inaweza ikapata kura hizi hizi za wanachama wake waliotoka CCM.

Ni kweli aisee.Na kuthibitisha hilo kura CDM walizopata Arumeru na Igunga ndio kura hizo hizo wamepata kwenye chaguzi ndogo.
 
katika uchaguzi wa 2010 wanachama wengi wa CCM ndio walioipigia kura chadema sababu zilizo wasukuma kuipigia kura sijui ni kuchoshwa na chama chao au imani? wao wanajua zaidi, lakini sasa wanaamua kuachana na chama chao na kujiunga rasmi na CDM, kwa hiyo kinachofanyika sasa ni wanachama wa CCM ambao ndio walioiwezesha kupata kura 2200,000 sasa wameamua kujivua gamba na kujiunga CDM, kwa hiyo katika uchaguzi ujao chadema wasipofanya uchunguzi vizuri inaweza ikapata kura hizi hizi za wanachama wake waliotoka CCM.

Hata kama waliipa kura CDM 2010, bado walibaki kuwa wanachama wa CCM, sasa CDM inawavuna rasmi na mungu akitujalia utashuhudia 2015 CCM itakavyosombwa na maji
 
KATIBU wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) tawi la Byarushanje kata ya Katoke, wilayani Muleba, Kagera, Evelina Eladius (36), amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Uamuzi wa katibu huyo umetokana na wanakijiji 1,005 waliokuwa wanachama wa CCM kukihama chama hicho hali iliyompa wakati mgumu katika utendaji wake hususan kazi za chama hicho.

Evelina alitangaza uamuzi huo hivi karibuni wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye mji mdogo wa Izigo ambapo katibu huyo na mumewe Eladius Theobald walipokea kadi za CHADEMA kutoka kwa mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Bukoba mjini, Victor Sherejei.

“Kujiunga kwetu CHADEMA ni kama tumechelewa kwani kati ya watu wazima wakazi wa kijiji chetu wapatao 2,620 CHADEMA imevuna wanachama 1,005 nina imani kwamba baada ya sisi kuondoka CCM wengine wengi watatufuata,” alisema.

Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Byarushanje Leonidas Bayona alisema nguvu ya CHADEMA ni kubwa kwani miongoni mwa wajumbe 25 wa serikali ya kijiji hicho 20 wanatoka CHADEMA.

Kwa mujibu wa Evelina ameondoka CCM baada ya kuchoshwa na uongo wa miaka 50 ya chama tawala ambapo huwajali viongozi na wanachama wake wakati wa uchaguzi ili kutafuta kura.

Alisema amebaini ubovu wa CCM baada ya miaka tisa aliyoitumikia kwa nafasi ya katibu wa tawi UWT na miaka sita aliyokuwa katibu wa CCM kata ya Katoke.

Mkutano huo ulihutubiwa pia na Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Bukoba Mjini, Renatus Kilongozi, Diwani wa Rwamishenyi Dismas Rutagwelera (CHADEMA) na Katibu wa CHADEMA jimbo la Muleba Kaskazini, Salehe Mashaka.

Source: Tanzania Daima

huu ni upepo tu unapita
 
Back
Top Bottom