Gharib Bilal ateuliwa mgombea mwenza wa Kikwete 2010

cjiu wamemchagulia nini? huyu mtu alipokuwa katibu mkuu wa wizara fulani, alikuwa mbaguzi sana alitoa sana scholarship kwa watu wa visiwani na sio bara cjui caca itakuwaje, simfagilii kabisaaaaa
 
cjiu wamemchagulia nini? huyu mtu alipokuwa katibu mkuu wa wizara fulani, alikuwa mbaguzi sana alitoa sana scholarship kwa watu wa visiwani na sio bara cjui caca itakuwaje, simfagilii kabisaaaaa

Labda anajaribiwa tena. Ilisemwa kuwa anapendelea sana huyo watu wa aina fulani kutoka sehemu fulani
 
hali yake ya kifedha ilikuwa mbaya sana angalau afya itarudi kidogo sasa.

mawazo ya ulevi sana haya..alikwsiha pata kuwa waziri kiongozi na mpaka leo serikali inamlea kwa kila kitu.sasa mambo ya alikuwa hana hela yanatoka wapi....
 
  • Jamani kama hatuna majibu :bored:tusikurupuke mtu kaomba CV,s sio haya tunayoyajibu!!!!!!!!!!!
 
Dr.Gharib Bilal alizaliwa tarehe 6 Februari,1945.
1967: Firsrt degree at Howard University (atomic physics)
1969: Masters degree katika Chuo Kikuu Cha California
1976: PhD katika Chuo Kikuu Cha California.
1976-1990 :Lecturer University of Dar es Salaam
1990-1995: Katibu Mkuu katika Wizara ya Sayansi,Tekinolojia na Elimu ya Juu katika serikali ya Muungano.
1995-2000: Waziri Kiongozi wa Zanzibar chini ya utawala wa Salmin Amour Juma.
2000: aligombea nafasi ya kuwana Urais wa Zanzibar ndani ya ccm bila ya mafanikio.
2010: aligombea Urais wa Zanzibar na badala yake atakuwa Makamu wa Rais wa serikali ya Muungano iwapo Kikwete atajishindia uchaguzi


hiyo ni kwa ufupi...............kama kuna sehemu nimekosea niwieni radhi
 
Chuma.jpg


DR BILAL ALIYEVAA KOFIA

Dr.Gharib Bilal alizaliwa tarehe 6 Februari,1945 huko Unguja. Dr.Bilal ni mwanasayansi aliyepata stashahada ya kwanza katika sayansi ya nuklia kutoka Chuo kikuu cha Howard nchini Marekani mwaka 1967. Alipata Masters Degree katika masuala hayo hayo ya sayansi ya nuklia kutoka chuo kikuu cha California mwaka 1969 kabla ya kupata PhD katika fizikia kutoka chuo hicho hicho cha California mwaka 1976. Kuanzia mwaka 1976 mpaka mwaka 1990 alikuwa Lecturer(mkufunzi) katika chuo kikuu cha Dar es Salaam -Idara ya Fizikia

Kati ya mwaka 1990 na 1995 alikuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Sayansi,Tekinolojia na Elimu ya Juu katika serikali ya Muungano.Mwaka 1982 alikuwa Mkuu wa Kitivo Cha Sayansi,Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam.

Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, aliteuliwa na Rais Salmin Amour kuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar. Mwaka 2000 aligombea Urais wa Zanzibar bila mafanikio. Mwaka huu alikuwemo miongoni mwa waliojitokeza kuomba ridhaa ya CCM kusimama kama mgombea Urais Zanzibar lakini bahati hiyo ikamuangukia Dr.Ali Mohammed Shein.Badala yake na kwa maana hii,atasimama na Kikwete kama mgombea mwenza na hivyo,endapo watashinda,atakuwa Makamu wa Rais wa serikali ya Muungano.
 
mimi ninavyo jua jamaa ni mtaalamu wnuclear physics,alipaswa atumwe kule kwenye uranium na sio politics
 
Asante waliotoa data!...hakuna wanafunzi wake humu watupe undani wake zaidi! Pia ningependa kujua misimamo yake ya kisiasi zaidi.
 
Back
Top Bottom