Gharama za ujenzi wa barabara zinatisha

Msharika

JF-Expert Member
May 15, 2009
947
69
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli amesema gharama kubwa ya ujenzi wa barabara ya lami kwa kilometa moja ni changamoto kwa serikali kwani inazidi hata viwango vya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa Dk Magufuli gharama hiyo inafikia kati ya Sh. bilioni 1.4 hadi bilioni 1.8.

Pia amesema kiwango hicho kinaweza kuzidi hata kile cha dunia na kuwataka wadau wote wa barabara kushirikiana kupambana ili gharama hiyo ishuke na kuwezesha barabara nyingi kujengwa kwa kiwango cha lami.

Alisema hayo jana kwenye kikao cha pamoja na wadau wa sekta ya ujenzi kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Magufuli alisema tatizo la gharama kubwa linaathiri nchi nzima na kuwataka wadau wote washirikiane na wakandarasi kwa uaminifu ili kushusha gharama hizo.

Akizungumzia suala la wakandarasi wa barabara, Magufuli alisema serikali inatambua deni kubwa inalodaiwa linalofikia Sh. bilioni 395 na kwamba madeni hayo yanashughulikiwa huku mengine yakianza kulipwa.

Alisema kati ya Sh. bilioni 19 za Mfuko wa Barabara, Sh. bilioni moja itapelekwa Mwanza kwa ajili ya kuanza kupunguza madeni ya wakandarasi wa barabara na kumtaka Meneja wa
Wakala wa Barabara (TANROAD) mkoani hapo kuhakikisha fedha hizo hazipangiwi matumizi mengine.

Amewaomba wakandarasi kuwa wavumilivu kwa kuwa watalipwa polepole na kuendelea kuomba zabuni nyingine pale zinapotangazwa huku akizitaka halmashauri kutumia fedha za
mfuko wa barabara kulipa madeni ya wakandarasi ili wasidai riba.

Kuhusu kupandisha hadhi baadhi ya barabara, Waziri Magufuli alisema zipo barabara zenye urefu wa kilometa 2,000 zinazohitaji kupandishwa hadhi kutoka kwenye halmashauri na kwenda Wakala wa Barabara (TANROADS).

Alisema barabara zimekuwa zikipandishwa kwenda Tanroads lakini fedha zilizokuwa zikitumika kwa matengenezo ya barabara hizo, zimeendelea kubaki katika halmashauri na
kusababisha barabara hizo kukosa matengenezo.

Ameahidi kuwa barabara hizo zitatengewa fedha katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha lakini maombi mapya hayatapokewa kwa sasa ili fedha zinazopelekwa halmashauri ziendelee kutengenezwa.

Source: HabariLeo | Gharama za ujenzi wa barabara zinatisha

 
.......................Akizungumzia suala la wakandarasi wa barabara, Magufuli alisema serikali inatambua deni kubwa inalodaiwa linalofikia Sh. bilioni 395 na kwamba madeni hayo yanashughulikiwa huku mengine yakianza kulipwa. ..................


Duuhh...........how and why tumefika hapo?
 
Gharama zilijuwaje zikawa juu hivyo?

Tanzania ina sifa gani kupelekea gharama za ujenzi kuwa juu zaidi duniani?
 
Back
Top Bottom