Gharama za kutunza viongozi wastaafu - marais, waziri wakuu na makamu marais

Nyang'oma

Member
Jan 25, 2011
8
1
Gazeti la raia mwema wiki hii limeandika uvumi kuwa waziri mkuu wa sasa ameomba asifikiriwe katika baraza jipya linalotazamiwa kutangazwa siku za usoni. Kama uvumi huo utakuwa kweli basi Pinda anaongezeka katika listi ya mawaziri wakuu wastaafu. Suala hili la gharama za kuwatunza hawa viongozi lilikuwa katika "election platform" ya Dr Slaa 2010 na kama leo Dr Slaa angelikuwa rais basi natumaini Taifa lingeliweza ku-save mamilioni ya fedha ambayo yanapotea kwa jina la "kutunza viongozi wastaafu" I stand to be corrected, sheria ya pensions za viongozi hawa ni 80% ya benefits za viongozi walioko madarakani. Mfano: Kama leo Pinda analipwa mshahara + marupurupu Tsh 25,000,000 kwa mwezi ( huu ni mfano) basi : Sumaye 80%* 25,000,000
Msuya 80%* 25,000,000
Warioba 80%* 25,000,000
Malecela 80%* 25,000,000
Hizi ni sehemu tu ya mafao ya hawa viongozi (direct costs) achilia mbali gharama za magari yao na safari za kwenda ulaya kutembea ana matibabu. Kuna gharama za watumishi majumbani kwao n.k. Ukiliangalia suala hili kwa undani utaona kwamba Taifa lina mzigo mkubwa sana!!! Tuna matatizo makubwa katika elimu yetu kuanzia mfumo wake mpaka namna inavyotolewa. Hela hizi kama zingelielekezwa huko basi nadhani zingeliweza kufanya japo sehemu ya mabadiliko katika sekta hiyo aidha kwa kununua madawati katika shule husika. Hao hapo juu ni mawaziri wakuu na bado hujaweka maspika na marais wastaafu. Nchi zinazotufadhali hazina upuuzi kama huu. Mfano ni Kanada ambapo kila politician including PM wanachangia towards their "defined pension contribution plans" na kwa kufanya hivyo unaona Kanada ina "transfer risks" kwenda kwa pension companies na siyo kama tunavyofanya hapa nyumbani. Huwezi kujitwisha mzigo mzito namna hii wakati tuna NSSF, LAPF, PPF nk. Mh Pinda naomba ufikirie uamuzi wako tena ili usaidie kuokoa mamilioni yatakayoenda kumtunza waziri mkuu mwingine. It is very costly!!!
 
Bado kuna mzigo mwingine utakuja kutoka msoga after 2015 election, ukiangalia alichoifanyia nchi in 10yrs, ZERO...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom