Mjadala: Gharama na njia nafuu za kujenga nyumba ya kuishi Tanzania

Unajua dirisha la aluminium complete haipungui kilo 3 una dilisha 11 mlango mzuri mninga 250000 ceiling gypsum kwa nyumba yako hyo makadilio M 3.5 tiles bado Mabomba mziki wake usikie tu bado shimo la Maji taka bado Fundi hajaimba cement name
Gypsum powder kaka hapo bado sana wiring nilisahau
Mkuu usitishike na hiyo kitu, jamaa mpaka hapo anaweka dirisha za kawaida na milango then anahamia. Mbwembwe ulizotaja hapo juu atamalizia akiwa kwake kwa kutumia ile kodi ambayo angempa faza/Mazda house. Big up kamanda!!
 
Askari muoga na anayetisha wenzie uwanja wa mapambano hafai na yafaa aondolewe site mara moja..huo ni uoga na kumtisha mwenzio.nani alikwambia ujenzi huwa unaisha siku hyo hyo kwa uwezo wetu wa kibongo??kuna simulizi za kweli ukiambiwa humu na ukishuhudia mijengo ilivyosimama,ukawacheki waliosimamisha na ukaambiwa mipango mikakati yao hutashangaa.ujenzi sio kula bia counter kwa mikwala ukafananisha na ujenzi..nimewasalisha jct 'in good faith'

Hahahahah mkuu ulivyomalizia tu " in good faith" nimependa.
 
Binafsi naona kazi kubwa ni kuezeka finishing ni mbwembwe za mtu tu we weka milango na madirisha.

kaka nakuunga mkono. Katika hatua ya ujenzi wa nyumba ya kisasa hatua ya finishing huchukua pesa nyingi sana tofauti na hatua mbili za mwanzo. Hii hatua ndio hatua nyeti sana kwani ndio hutoa taswira sahihi ya nyumba uliyohitaji. Katika ujenzi hatua mbili za mwanzo zinakamilisha dhana nzima ya mtu kuanza kusema nina nyumba kwani kwahatua hizo mbili za mwanzo mtu akipatwa na dharula anaweza kabisa akahamia kwake na marekebisho mengine ataweza yafanya akiwa kwake.

Nafurahi kuona kijana akimili nyumba ujanani.
 
Mi nimeweza kwa kujipanga na kipato changu ni kidogo. Vijana tusitishwe na wanaotaja mamilioni ili kujenga nyumba. Hii inakaribia kuisha na sijafikisha hata m 20!

Hongera mkuu kwa jitihada hizo sio kwamba nakudis yaani kwa jinsi ulivyojenga hiyo nyumba utahitaji ukimalizia katika UBORA huohuo lakin
Pengine nikuambie tu mpaka unaamia hiyo nyumba itakuwa imekula gharama mara 3 zaidi Ya hiyo gharama iliyopo.
Mfano mdogo kitasa imara cha mlango mmoja tu walau sio chini Ya 60000 sasa kama unamilango 7 ni kama 420000 .
sasa bado gharama ya fundi.na gharama Ya hiyo milango.
Dirisha moja la aluminum pamoja pamoja na gril lake sio chin Ya 300000 kama hiyo nyumba ina dirisha. Kumi ni kama 3000000 bado kupiga draft za ceilin/gypsum
Bado miundo mbinu Ya maji , vigae vya sakafuni ,wiring na mengine .. mengi ..kama rangi yaani hiyo nyumba bado sana mkuu .. huko kuliko baki ndo pakubwa kulingana na UBORA wa hiyo nyumba
 
Mkuu usitishike na hiyo kitu, jamaa mpaka hapo anaweka dirisha za kawaida na milango then anahamia. Mbwembwe ulizotaja hapo juu atamalizia akiwa kwake kwa kutumia ile kodi ambayo angempa faza/Mazda house. Big up kamanda!!
Good response
 
Ya kwangu pia hiyo hapo mpaka hapo hata m15 bado...uwanja wa million 3.inawezekana bana
 

Attachments

  • 1419445076023.jpg
    1419445076023.jpg
    77.7 KB · Views: 1,302
Nahamasisha vijana wenzangu kumiliki nyumba zetu na tuachane na ujinga wa kushindanishana kununua magari ya kifahari huku tumepanga. Tabia kama hizi zinakuwa za kitoto.
Kijana mzima ambaye life yako unaoshi kwa kutegemea salary eti unanua simu ya milioni!! Na kijana huyo anayenunua hiyo simu hata kiwanja hana. Tubadirikeni vijana wenzangu.

Mzazi hufurahi anaposikia kijana wake sasa ana mji wake anaoumiliki kwa 100% sio kupanga. Kijana unakuta kajaliwa kazi nzuri mshahara mzuri eti yeye akili zake anazielekeza kuwa mtu wa kulewa lewa a.k.a chapombe na malaya.

Tuige mfano wa jamaa huyu.
 
Roma bado inajengwa.

Construction work for Metro line C at Porta Maggiore, Rome

Construction_work_for_Metro_line_C_at_Porta_Maggiore%2C_Rome.jpg

Safi mkuu kiranga kwa kutia moyo..ukisubiri umalize nyumba yote kwa mkupuo utajikuta kuna lumpsum ambayo yamkini kwa kipato chetu wengi wetu hutokaa uje utimize mpk unaingia kaburini.
 
Mkuuuu,tupe progress baada ya kuweka madirisha,miundombinu ya maji taka,safi,milango,ceiling boards n.k,huko ndio kwenye balaa,mbona kupandisha boma sio kazi,kazi finishing mkuu,hapo ndo utakapotoa macho utakapoambiwa wiring tu milioni unusu na ndipo utakapoanza

kuwachukia mafundi
Milango na madirisha tayari ninayo na ni Mkongo pure. Hayo mambo mengine kidogo kidogo. Ujenzi haufanywi siku moja, cha msingi usiifikirie pesa yako kwenye ujenzi, na usiwaze mpaka upate hela ya kufanya mambo yote kwa pamoja. Unaweka pesa kidogo kidogo. Kwa mfano ukipata 300k unanunua boksi kadhaa za tiles unaweka ndani, haziharibiki. Sisi masikini huwezi kufanya vitu vyote 'at a go'
 
hongera sana kiongozi, na nivizuri kuwa[a moyo vijana wenzako ili wawe na mumkari wa kujenga sio kununua vitz na spacio kumbe wanajipa matumizi yasio na tija, nyumba siku zote heshima
 
Heshima bar, halafu hao hao wanaokunywa naye pembeni wanamg'ong'a jamaa pesa yake yote inaishia kwenye kilevi hana hata kibanda.

Siku zote huwa namuheshimu sana mtu anaefanya kitu kama hiki......hata kama ni room moja........anastahili pongezi.......heshima kwako sana mkuu.......wenzio hiyo pesa ya kufanya hivyo wanaweka heshima bar.........
 
Back
Top Bottom