Gharama za Kufunga wiring nyumba Dar

Mzee2000

JF-Expert Member
Aug 7, 2009
527
221
Naomba mnisaidie,je gharama za Kufunga wiring nyumba ya vyumba vitatu vya kulala size ya wastani yaani Kuweka na luku, Dar es salaam ni kiasi gani?

Naomba gharama rough tu kwa anayejua au kwa experience.

Nitashukuru sana.
 
Inategemea na ukubwa, na LUKU uwekayo ni service line tu au unavuta na nguzo juu ?!

Ila kiharaka haizidi milioni kama ni hizi za kawaida sana
 
Roughly sh. laki sita inatosha.

Laki 6? Hapa kuna vitu viwili. Kwanza kufanya wiring, pili kuingiza umeme. Kuhusu wiring bei inategemea material unayotumia (quality ya nyaya), quality ya fundi, main switch, sockets etc. Kwa mfano switch za taa zipo za tsh 2000, 3500 na 6000. Nyaya ndo zinatofuti kibwa sana ya bei. Nafikiri budget ya 1.5m ni ideal.

Kuingiza umeme inategemea pia nguzo ngapi. Kama ni nguzo moja ni Tsh 1.4m. ongeza laki 7 kwa kila nguzo inayoongezeka. Punguzo lililotangazwa bungeni halijaanza kutumika hado Jan
 
Swali ni gharama ya wiring na luku.
Luku hailipiwi. Wiring laki sita inatosha kwa nyumba ya vymba vitatu.
Gharama ya wiring na kuingiza umeme 1.3 mil inatosha. Hii ni kwa mahesabu ya bei ya zamani, kutokana na taarifa za kushuka kwa bei za kuingiza umeme, inawezekana 1 mil ikatosha...
 
Labda nieleweshe zaidi.Nyumba ni vyumba vitatu vya kulala dining sitting room na choo size wastani.

Kuna kuweka wiring pamoja na kuvuta umeme.Umeme upo si zaidi ya mita 15, yaani upo kwa jirani next ya nyumba yangu.je nitahitaji nguzo?breakdown ya gharama za kuvuta umeme na Kuweka wiring kwenye nyumba ndio natafuta.

Ahsanteni kwa wale walionipa majibu ya awali.
 
Huhitaji nguzo na kwa makadirio angalia post yangu hapo juu...
 
mkuu ni PM nikupe fundi wangu wa uhakika na kazi anapiga vizuri tu
 
Back
Top Bottom