Gharama za kivuko kigambon zapaa

Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,730
1,201
Kuanzia tarehe 1 mwezi januari mwakani nauli ya kuvuka kwenda na kutoka kigamboni itakua shiling mia mbili kwa mtu mmoja,na gari zitatozwa sh elfu mbili!
Walalahoi tujipange kufunga mikanda,
 
litakamilika Mungu akipenda muungwana mwenzangu. Kama mishahara tu ya watumishi haipo ndo litajengwa daraja??? Tafakari na uchukue hatua. Ngwan ngwan ngwan.
 
Serikali imeona ndo njia pekee ya kuwatimua wanaoishi kigambo ili wawalipe kiasi kidogo wakati wa ujenzi wa mji mpya
 
Nahama Mji Mwema wacha nikajibane na wahindi na kina FF katikati ya mji maana kukaa mbali foleni kero kigamboni niliona ujanja sasa inakuwa kero na kuogelea naogopa kuliwa na samaki mimi.
 
DSC00760.JPG

Daraja letu liko mbioni.
 
Kama mmesoma makala ya Mbwambo kwenye Raia mwema wiki hii ametoa tahadhari ya umma kujiandaa na hali ngumu zaidi 2012 kuliko hii ya sasa kwani serikali imekwama haina tena mbinu mbadala za kujiongezea mapato zaidi ya kuwakamua wananchi.
 
Nilitegemea wangeanza kuwalipisha maaskari na maafisa wa jeshi ambao huvuka bure.

Kabla ya uchaguzi waliweka tangazo la kuongeza nauli ya kivuka lakini hawakutekeleza, na wakazi wa kigamboni waliyachanachana matangazo hayo.

Tusubiri tuone, kama gharama za uendeshaji zimeongezeka, sio kweli, mv magogoni in injini nne na sasa wanawasha injini mbili hadi 3 tu, kutokana na hali hii, kivuko hiki kinachoka kila siku. Ninaamini ni suala wanalolipanga ili kuiba mafuta-kupiga nyoka.

Tusubiri tuone, wakazi wa kigamboni wa jana si wa juzi, enzi za kitwana kondo na upuuzi wake wa sh.50 zimepita.
 
Jk sijui tukuelewe je kwani kuna vitu havijawahi kupanda zaidi ya miaka 20 iliyopita japo hali ya maisha na kushuka thamani ya hela kushuka kama nauli ya wanafunzi ilikuwa sh. 50 kwa muda mrefu sana ila tangia uingie madarakani imepanda mara 2 kwenda mia na sasa 150 na nahisi mpaka uondoke madarakani 2015 kama waTz wataendelea kuwa wavumilivu yaani wasipokuondoa kwa nguvu ya uma tunategemea itakuwa zaidi ya 300, kivuko kinapanda bei ambayo ilidumu kwa muda mrefu tena inapanda kwakudable, Nishati za mafuta na umeme tunapata kwa mgao, je wanauchumi wako na uchumi uliosomea pale mlimani ndo ulikufundisha kuwa taifa linaendelea pasipokuwa na nishati kama hizi? Yafaa ujiulize na kuchukuwa uamuzi ambao utakuwa na faida kwa taifa na kuwafurahisha wengi kwakujiuzulu kwa manufaa ya taifa mliloliweka rehani mdomoni mwa simba mwenye njaa kali
 
Mbona hicho kivuko cha kigamboni,wamechelewesha!inawezekana ni kati ya hudumu ya mwishoni kuchelewa kupanda.
 
Back
Top Bottom