Gharama ya demokrasia ni kubwa, tuwe makini na wanopindisha sheria na kanuni za uchaguzi

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Serikali makin siku zote ni sikivu na husimamia utawala bora.Kama utawala bora ukisimamiwa ipasavyo hata mambo yaliyopo ndani ya serikali uwekwa kwa uwazi kwa wananchi walioipa dhamana.Haina haja ya kuficha mikataba na kuifanya ya siri,usiri huu ndiyo bridge ya kutengeneza ufisadi ndani ya taifa.Kwa mantiki hii basi kuna haja ya serikali kuvunja ukimya na kuweka wazi kuwa, kuna haja ya kufanya min budget ili kuziba gaps ambazo zimejitokeza na serikali kukaa kimya.Ikiwa mafungu ya budget ya maendeleo ambayo nayo ni madogo yanatishiwa kupunguza ili serikali iweze kujiendesha kuna haja gani ya kukaa kimya na kushindwa kufanya min budget.

Kuna suala lingine ambalo tusipoliangalia kwa makini tutafanya uchaguzi kwa kipindi chote cha miaka mitano na kushindwa kusimamia shughuli za maendeleo kutokana na watendaji wasio waaminifu kuchakachua kwa makusudi taratibu za uchaguzi kwa lengo tu la kuwanufaisha watu fulani walio amini wamezaliwa kuwa watawala wa nchi hii milele.Kuna haja ya kuweka sheria kali kwa watendaji wote wanao tuingiza kwenye gharama za uchaguzi kwa makusudi kwa kupindisha matokeo ya uchaguzi.Ni kweli gharama ya demokrasia ni kubwa lakini haitoshi watendaji hawa kuachwa hivi hivi bila kuchukuliwa hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine wanaocheza na demokrasia.

Tunawaomba wabunge walio makini, watumie fursa hii kutunga sheria ya uchaguzi yenye meno, ikibidi ikadhibitika mtendaji wa tume ya uchaguzi kapindisha sheria na kanuni za uchaguzi kwa makusudi adhabu kali juu yake ichukuliwe na ionekane ichukuliwa kweli na hata ikibidi kunyongwa anyongwe kwani lengo lake si zuri ,kwa kutaka kutuingiza kwenye machafuko ambayo mwisho ya siku ni umwagaji wa damu kwa wasio na hatiya.Tanzania ni ya kwetu sote,hatupendi tuikumbuke awamu ya nne kwa historia ya kurudia chaguzi mbalimbali zilizosababishwa na upidishaji sheria na kanuni za uchaguzi kwa makusudi.Watanzania tuwe wakali na watu wa aina hii,kwani bado tuna kumbukumbu ya uchaguzi wa Kenya iliyogubikwa na machafuko kutokana na mtu mmoja aliyepewa dhamana akashindwa kuisimamia kwa nidhamu ya hali yajuu kwa kuwa tu yeye ni mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kwa lengo la kumfurahisha bwana mkubwa.Kamwe hatotalala mpaka tuone haki ikitendeka na ikiwezekana kila mmoja atimize wajibu wake.
 
na mimi nakuunga mkono kati ya watu wanaochangia matumizi mabaya ya pesa ni wanasiasa naomba itungwe sheria si tu ya kuwabana wasimamizi bali hata vyma husika ili kama mgombea weao akikiukla sheria za uchaguzi chama husika kitozwe faini ambayo ni nusu ya gharama za uchaguzi hii itawafanya vyama husika kudhibiti wagombea wao
 
Pia mfumo dume wa tume ya taifa ya uchaguzi ubadilishwe ikibidi tuifanyie reform tume hii.Wakati mwingine mapungufu mengi tu huorodheshwa na tume kulalamikiwa lakini hakuna hatua zinazo chukuliwa na tume hii.Tume imekuwa ya kisiasa zaidi na upendeleo kwa malalamiko yatayotolewa na chama tawala.Gharama inayotuingizia tume zingeweza kujenga zahanati kwa kila kata na shule zote kupatiwa madawati.Hatuwezi kuendelea kuwa na serikali inayojaribu kutumia mabavu yake kuhakikisha inaendelea kutawala japokuwa haikubaliki kwa wananchi wake.

Kitendo cha taasisi ya kuzuia rushwa kukaa kimya bila kuwachukulia hatua aidha kuwafikisha mahakamani kwa makosa ya kushinda uchaguzi kwa ushawishi wa rushwa ni udhalimu na anguko dhidi ya serikali ya CCM.Haitoshi mahakama kutengua tu matokeo kwa wwabunge waliotumia rushwa bali wangefungwa kwa kutumia ushahidi uliotolewa hapo tungeamini serikali ya CCM ina nia ya kutokomeza rushwa nchini.

Kitendo cha rushwa kuitwa takrima na kupiganiwa bungeni kimedhihirisha ni aina gani ya watunga sheria tulionao nchini mwetu.Wakati mwingine nawapongeza sana CDM kwa kutoka kwao bunge pale wanapoona haki inabakwa na wao kuwa sehemu ya kubaka haki hiyo.Tuna tegemea baada ya majumuisho ya kesi zote za uchaguzi Mwenyekiti na mkurugenzi wa tume ya taifa ya uchaguzi nao wapandishwe kizimbani kwa kushindwa au kwa makusudi kusimamia haki ya kikatiba ya mtu kuchaguliwa.Pia kuelekea katiba mpya ,iwe ndiyo fursa ya pekee kutoa kila aina ya ukandamizaji wa sheria na mazongezonge kwenye mfumo wetu na tume yetu ya uchaguzi..
 
Back
Top Bottom