Ghana yafunga maduka ya wageni

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
IDHAA YA KISWAHILI dw / Matukio ya Afrika
[h=4]Matukio ya Afrika[/h][h=2]
ghana_kumasi_market3_w.jpg
[/h]

Serikali ya Ghana haitaki mchezo. Tokea wiki hii biashara na vibanda vya raia wa nje vinafungwa. Vikosi maalumu vinaifanya kazi hiyo. Milango ya maduka na ya vibanda inatiwa kufuli.
Serikali ya Ghana imepitisha sheria inayowaathiri wafanyabiashara kutoka nchi za nje ikiwa pamoja na Waafrika wanaotoka nchi zilizomo katika jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS. Sheria hiyo inawataka wafanyabiashara hao wafungue biashara zao kwenye sehemu zilizotengwa maalumu, kila mfanyabiashara wa nje afungue biashara yenye thamani ya dola 300,000 na lazima awaajiri wananchi wa Ghana angalau kumi.


Wageni wengi wanaendesha biashara ndogo ndogo

Waziri wa biashara wa Ghana Hannah Tetteh amesema kuwa lengo la sheria hiyo ni kuyalinda maslahi ya wafanyabiashara wazalendo na amekanusha madai kwamba sheria hiyo inawanyima haki raia wa nchi nyingine na kuharibu mazingira mazuri ya kufanyia biashara Ghana. Naye waziri wa mabo ya kigeni wa nchi hiyo, Alhaji Muhammed Mumuni, amepinga shutumua kwamba sheria mpya ya biashara inakiuka mikataba ya ECOWAS inayotaka raia wote wa nchi mwanachama wapewe haki ya kuingia na kuishi katika nchi yoyote ya jumuiya hiyo bila kizuizi.
Wanigeria wengi wanafanya biashara ndogo ndogo tu
Lakini sheria hiyo imeshasababisha mvutano baina ya Ghana na nchi nyingine za Afrika magharibi kama Nigeria. Wabunge wa nchi hiyo sasa wanataka Nigeria ivunje uhusiano wa kibalozi na Ghana. "Wafanyabiashara wengi kutoka Nigeria wanafanya biashara ndogo kama vile kuuza CD, mikanda ya video pamoja kaseti za redio. Watawezaje kupata mtaji wa dola 300,000 unaohitajika kuanzisha biashara?" aliuliza mbunge mmoja, Abike Dabiri-Erewa.
Hofu imetanda miongioni mwa wafanyabiashara wa kigeni waishio Ghana. Amaefola Chijoke, raia wa Nigeria, anauza simu za mkononi katika barabara ya Kwame Nkrumah iliopo Accra, mji mkuu wa Ghana. Yeye anaeleza kwamba wafanyabiashara kama yeye hawajahamia Ghana wakiwa na lengo la kuyaathiri maisha ya Waghana bali wanakimbia umasikini nchini mwao. Mfanyabiashara mwingine wa Kihindi amelalamika kwamba tayari ameshawekeza mamilioni katika uchumi wa Ghana lakini anahofia kwamba hilo halizingatiwi tena. "Kwa kweli hatuji tufanye nini," alieleza mfanyabiashara huyo.

Mwandishi: Elizabeth Shoo
Mhariri: Mohammed Khelef
 
Report haijakamilika. Je, wafanyabiashara hao wa kigeni walikuwa wanafanya biashara hiyo kihalali au kwa kuvunja sheria? Kama walikuwa wanafanya kihalali, je, haki zao za msingi zimezingatiwa katika zoezi hilo? Kama walikuwa wanafanya kinyume cha sheria, then they shoul not only close their shops but also take them to the court of justice.
 
Je tanzania tunaweza haya?? angalia hata Wachina Bongo ni Machinga!!!!
Ili mtu aweze kufanya haya yote ni lazima medula oblongata yake iwe imekomaa vyakutosha na awe na akili timamu ya kuyatambua haya!Ni chadema tu wenye akili hiyo kwa sasa na wala sio manyang' au chama cha magamba CCM.
 
Back
Top Bottom