Nyalotsi
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 6,978
- 5,025
Nampenda na yeye ananipenda. Kinachoniumiza kuna watu wanaonifahamu wanamfeed mambo yangu ambayo hayamvutii. Kuna wengine wanamtajia wasichana niliowahi kuwa nao. Mwingine alifika mbali zaidi na kumwambia mimi nimeoa na kuacha mke. Huwa ananiulizia majina ya hao wasichana na tulikuwa na uhusiano gani! Nilishamwambia kuwa nilikuwa na mahusiano huko nyuma na nimeacha lakini sikumtajia majina yao. Hivi haniamini? Nifanyeje? Naona kama itavunja uhusiano, maana kuna muda huwa nakasirika ila najishusha.