Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,550
- 6,062
Huyu Mwandishi kachemsha maana naifahamu hii kampuni kama ya Austria.
Nimegoogle kuhakikisha na kukuta ni kweli data zangu maana nilifikiri labda Wageruman wamenunua.
Kujenga stendi ya Mabasi nje ya mji ni USHAMBA uliopita kiasi.
Ningelipendekeza kujenga somewhere Buguruni kati ya Reli ya TAZARA na Reli ya kati na wakati ule ule ni One Way kwenda Air Port. Kutoka hapo, ijengwe barabara moja kwa moja kwenda Ubungo na pawe na Fly-Over au wajenge RING nyingine kama ilivyo Mandela Road na hiyo barabara ije hadi hapo kwenye kituo cha Mabasi.
Kujenga kituo cha mabasi nje ya MJI au AIRPORT ni kuonyesha kwa kiasi gani MIJITU inavamia fani za watu bila kujua.
Nenda hata Washington, Railway Station inakuja hadi almost kwenye jengo la Congress.
Sweden wao wameunga kituo cha mabasi, Metro na Railway Station katika sehemu moja na mjini kabisa Stockholm.
Ila sisi tunataka tuweke PORINI, sasa sijui ukishuka huko usiku, utaendaje nyumbani na vibaka hawa mitaani.
Kuna mtu akili zake kwa kweli si sawa na kama ni homeboy Magufuli, tafadhali okoa hela za Taifa hili maana hiki kituo na Airport nje ya mji wa Dar, hakuna atakayetaka kuteremkia huko. Mie ni heri nilipe dola 100 zaidi na niteremkie JKNIA Kipawa kuliko niteremkie Bagamoyo saa moja asubuhi na kuingia foleni ya Dar na kuja kufika Temeke nyumbani, imeshakuwa saa sita mchana.
Tafadhali Magufuli, panueni hiyo barabara ya Morogoro na wekeni hizo Fly Over. Airport ibaki hiyo ya Dar ambayo nasikia hata kuipanua mmeshindwa maana hela mmeishiwa (data zipo kwenye Internet na hiyo ramani ya Wachina).