Geranimo E.K.I.A: Kutoka Makao Makuu ya CIA Langley, Oparesheni Ya Kukamatwa Osama Bin Laden

Inshallah inshallah..
Pale Maswala ya Siasa yanapotuumiza vichwa,pale ajira na pesa za kujiajiri zinapokuwa changamoto ,pale Matumaini yanapopotea kutoka kwa Mkulu na madogo wakihitaji pesa ya chuo maana MKOPO ni makopo! Basi ndio pale MKUU THE BOLD anapokuwa muhimu sana ( ni muhimu kila siku ) kutupa mambo ya kutusaahaurisha majonzi yetu na kutujuza yale tusiyoyajua!!!

Tupia Kitu Mkuu.
 
Pale Maswala ya Siasa yanapotuumiza vichwa,pale ajira na pesa za kujiajiri zinapokuwa changamoto ,pale Matumaini yanapopotea kutoka kwa Mkulu na madogo wakihitaji pesa ya chuo maana MKOPO ni makopo! Basi ndio pale MKUU THE BOLD anapokuwa muhimu sana ( ni muhimu kila siku ) kutupa mambo ya kutusaahaurisha majonzi yetu na kutujuza yale tusiyoyajua!!!

Tupia Kitu Mkuu.
Nashukuru sana Mkuu! Kitu kingine kinakuja very soon..
 
Hii nadharia ya US kujilipua wenyewe ili ati wapate sababu ya kuingia mashariki ya kati kuiba rasilimali kwa kutumia pazia ya vita, hii nadharia bado sijaikubali kabisa bado roho yangu inakataa kuamini.. Hasara iliyopatikana kutokana na kudondoka yale majengo ni kubwa mno mno mno, kiuchumi, kiusalama, kibinadamu!! Na bado kulikuwa na gharama za kuendesha vita, ukipiga jesabu haraka haraka sidhani hata hayo mafuta yanayodaiwa kuibwa yanafikia thamani hiyo..
Mkuu conspiracy theories zipo nyingi na pengine tunapata tabu kwasababu ya hichi kitu kinachoitwa classified information pengine tunaumiza vichwa hapa we lakini kuna watu 10 au 20 wanajua what really happen in sept 11 lakini katika kuufikirisha ubongo lazima kuna maswali ya kujiuliza.
1.Osama ni mtu aliyekulia Marekani, Taifa ambalo lina kila aina ya races na wote wana haki sawa kivipi huyu mtu akaja kuwageuka.
2.Mara kadhaa wamarekani wao wenyewe walidai kuna uwezekano akawa amefariki na baadhi waliamini hivyo then how comes.
3.Sept 11 haijabeba dhima ya kuongeza ukwasi tu lakini pia kupunguza idadi/ na ushawishi wa imani ya kiislamu duniani.
4.Wadau baadhi wameeleza namna ya kuanguka lile Jengo, Niko Field ya uhandisi Majengo sio rahisi leo hii Jengo lililojengwa kwa teknolojia ya karne ya 21 ligongwe juu ya ncha yake afu li collapse lote sio rahisi, otherwise hawa magaidi walifanikiwa kuweka Mabomu hadi chini ambayo yalilipuka pale ndege ilipo hit Jengo. Na kuna jengo pembeni kuna footage inaonekana lile jengo linaporomoka few seconds kabla ya ndege kuhit Jengo la WTC

Kuna vitu hatuwezi kujua ila kuna maswali ya kimantiki tukijihoji Wamarekani hawawezi kukwepa kuhusika kwao kwa lile jambo huo ndo ukweli, Na hiki tunachokishuhudia sijui training za hawa watu, offshare money transfer inawezekana kabisa ni tukio waliliratibu vizuri tu, ili kuja kucover story vizuri wenzetu wako smart, kama wanaweza kusema wamefika mwezini tena mwaka 1969 ili hali sio kweli sioni kama hili wanaweza shindwa. Hili nimefikiria baada ya kufikiria post ya hivi karibuni ya sleeper agent, Ambapo inaweza mchukua mtu hata miaka 30 akiwa kwenye mission pengine kwa kujua au kutokujua, akapelekwa na kukulia hata katika taifa flani na ku adopt kila kitu cha taifa lingine mki mtrace anaweza kuwa mtanzania lakini anaonekana ni Mnyarwanda ana biashara,ana familia,makazi anaongea kinyarwanda fasaha and so on, sasa je Osama hakuwa sleeper agent wa USA ambaye alikamilisha mission kwa kujua au kutokujua na baadaye akageuziwa kibao. My point juu nimesema hizi huwa ni classified information ambazo ni kundi dogo sana hufahamu motive behind na pengine wanaweza kucheza mchezo wa kukamilisha mission za wenzao hata pasi kujua wao wakijua wanapigania interest za Taifa lao
 
Mkuu unapokuwa unataka kumtag mtu ili auone uzi uwe unaweka hii alama mwanzo mwa jina lake "@" eg: @ The bold, hapo me nimeruka ili uone lakini nisiporuka inakuwa na atach yani kama hivi The bold..
hapo mtu hupata notification kuwa ame be taged sehemu fulani so inakuwa rahisi kwa yeye kuuona uzi. chengine cha kuzingatia ni kufata jina la mtu lilivyoandikwa kama ni KENZY imeandikwa kwa herufi kubwa nawe andika hivyohivyo kisha weka hiyo alama mwanzoni mwa jina.. ama kama kuna mchanganyiko wa herufi kubwa na ndogo na we liandike hivyohivyo.
ni hivyo tu mkuu
Ahsante sana mkuu kwa kutuelewesha na mimi ilikuwa inanipa taabu jinsi kumtag mtu ngoja nijaribu Nifa
 
Story nzuri sana, nimependa aina ya usimuliaji inakufanya usichoke kufuatilia...ila Story ya Osama kushiriki 9/11 ni kama usanii flani, uwezekano wa kuwa inside job ni mkubwa zaidi

Ni kweli 9/11 it was an inside job, Bush na kundi lake walikuwa wanatafuta kisingizio cha kumuondoa madarakani Saddan Hussein na kuiba mafuta wakati wa occupation, njama hizo walishirikiana na Israel ndiyo maana siku ya tukio hakuna mu-Israel hata mmoja alipoteza maisha ndani ya majengo hayo pacha ingawa zilikuwepo ofisi nyingi za Makampuni ya Israel kwenye majengo hayo, walipewa taarifa mapema wasije kazini.

Niliona Rais Bush alipo pewa taarifa kuhusu tukio la ndege kubamizwa kwenye majengo, Bush hakushituka hata kidogo aliendelea kuwasomea adithi watoto wa chekechea - hii inamaanisha alijua kinacho endelea, hata kudondoka kwa majengo kilionyesha it was a controlled implosion/demolition i.e columns zilikuwa ringed na high explosives kwenye msingi/foundation na kulipuliwa kwa mpigo - watu wengi wanaojua mbinu zinazo tumika kudondosha majengo marefu bila madhala kwa majengo jirani, weledi wanajua kwamba milipuko yenye nguvu zaidi ndiyo zilizo wekwa kwenye columns za misingi ya majengo pacha na kuya dondosha - kilicho fanyika pale ni usanii mtupu!!

Linapo kuja suala la Bin Laden, Taifa la Merikani linavyo penda sifa na kutisha tisha watu si rahisi kumuua Osama wakasahau kupiga picha na kuzisambaza Dunia nzima kudhilisha Umahili wao wa ku deal na magaidi - awawezi kusahua hilo hata siku moja, cha ajabu ni watu achache ambao awahoji hilo i.e wawaulizi picha za mwili wa Bin Laden ziko wapi???

Mbona Bush alipotoa amri ya Kunyonga Sadam Hussein kila kitu kilionekana adhalani kupitia MSM, Bush alifanya kitendo hicho makusudi kutisha Viongozi wengine Duniani ambao wata jaribu kuingilia maslahi yao walihakikisha picha za Hussein akitiwa kitanza zinasambazwa Dunia nzima - je, za mwili wa Osama ziko wapi?

Binafsi naona operation nzima ulikuwa ni usanii mtupu, aidha Osama alikufa miaka mingi kutokana na ugonjwa wa figo alio kuwa nao, au bado ni nzima anaishi nchi fulani akiendelea kulipwa mshahara na marupurupu by CIA maanake wao ndio walimfundisha mambo ya Ugaidi kwa malengo maalumu, sisi wanaendelea kutuzuga tu.
 
Back
Top Bottom