George Weah vs Ronadinho

Papa Mopao

JF-Expert Member
Oct 7, 2009
4,107
2,506
Kuna siku nilicheki kipindi cha mahojiano cha George Weah na mwandishi, kuna baadhi ya clips walikuwa wanazionesha,Weah alicheza mipira ya ajabu sana, naona hata Ronadinho hajawahi kuvionesha akiwa uwanjani. Ronadinho kwa kweli hajamfikia Weah.
 
Kwangu mie:

Siwezi mlinganisha Weah na Gaucho.

Gaucho ni zaidi ya Soka! Ni mchawi!
 
if gaucho angekuwa dini ningekuwa number ONE worshipers. LIKE wale waliomuona maradona mpaka wakaanzisha iglesia maradoniana. ronaldinho ni next level mkuu.
 
Nimeangalia mipira ya hawa wote wawili, Ronaldinho sawa ana mipira ya nguvu, lkn Weah wakati mwingine alikuwa ananikuna sana na chenga zake pamoja na manjonjo ya kuongezea kwa juu!
 
Hao wote ni sawa, ila naomba niende nje kdg ya hao tuwaongeleao.
Okocha ndie tunaweza kusema ni mchawi wa soka, japo hakutunukiwa mataji yoyote...ila ndie aliemuweka Gaucho benchi kwa kipindi chote walipokuwa pale PSG, na manjonjo mengi ya Gaucho aliyapata toka kwa JJ-Okocha. Bara zima la Africa halijapata kuwa na aina hii ya mchezaji mwenye kufanya lolote uwanjani na kwa mazingira yoyote yale.
 
Kwa Okocha sawa kabisa nakubaliana na wewe yeye ni zaidi ya Gaucho kwa urembo wa uchezaji uwanjani, lkn kwa mipira ya George Weah ilinikuna zaidi, kuna mahali alipiga chenga mabeki watatu kwa mpigo mmoja na akamalizia kufunga goli kwa kumpitishia dobo kipa timu pinzani, ningekuwa na clips hapa ningezi-upload!
 
Gaucho Was From Another Planet Ndugu Yangu, I Should Still Is Kwa Sababu Talent Ya Mtu No Matter The Age Haiondoki.. He Is The Only Player In History Kupata Standing Ovation At The Bernabeu Stadium Uwanja Wa Real Madrid Kutoka Kwa Mashabiki Wa Marid.. Tafuta Mechi Ya Madrid Na Barcelona On Youtube
 
FYI: Hata mzee wa mabigijii alikuwa anammaind Jay-Jay

Manchester United must find a way of stopping Jay-Jay Okocha tonight .. and Sir Alex Ferguson said: "Okocha is a fantastic player. I enjoy watching him play...."
 
Weah hamfikii Gaucho hata robo.Nadhani mtoa mada hajapata clips za kutosha za Gaucho.Nenda katafute CD za Gaucho VS Zizzou,halafu tafuata cd ya mazoezi ya timu ya taifa ya brazil akiwa anafanya mazoezi na kina Robinho.Ktk karne hakuna mtu mwenye control kama Gaucho.

Nimeona moja ya clip zake anapiga mpira umbali wa mita 30 unagonga mwamba wa juu kisha unarudi kifuani kwake na anautuliza na kuupiga tena unarudi vile vile.Alirudia hivyo karibu mara tano na hajakosea.Tafuta CD zake kisha utapata jibu.Gaucho ni mtu wa kulinganishwa na Zizzou kwa ball control.Hata hao kina Pele na Maradona walikuwa na sifa zao lkn sio jinsi ya kuuchezea mpira.
 
Kuna siku nilicheki kipindi cha mahojiano cha George Weah na mwandishi, kuna baadhi ya clips walikuwa wanazionesha,Weah alicheza mipira ya ajabu sana, naona hata Ronadinho hajawahi kuvionesha akiwa uwanjani. Ronadinho kwa kweli hajamfikia Weah.
Acha ujinga wakati mwingine uje na vithibitisho
 
Hao wote ni sawa, ila naomba niende nje kdg ya hao tuwaongeleao.
Okocha ndie tunaweza kusema ni mchawi wa soka, japo hakutunukiwa mataji yoyote...ila ndie aliemuweka Gaucho benchi kwa kipindi chote walipokuwa pale PSG, na manjonjo mengi ya Gaucho aliyapata toka kwa JJ-Okocha. Bara zima la Africa halijapata kuwa na aina hii ya mchezaji mwenye kufanya lolote uwanjani na kwa mazingira yoyote yale.

Katika watu walioongea ushuzi hapa JF basi wewe unaongoza na kama likitokea punguwani jingine zaidi yako ntalinasa makofi na kulifukuza.

kwanza unatakiwa ufahamu Okocha kapiga PSG kuanzia 1998-2002.
Kisha mtakatifu Gaucho wa Dinho kakipiga kuanzia 2001 mpaka 03.

So jaribu kwenda kuangalia ni mchezaji gani kati ya hao wawili kaifungia magoli mengi zaidi PSG?

Kisha rejea kuwa wakati Okocha anaondoka PSG akaenda Bolton, je unaweza kunishawishi kuamini kuwa timu kubwa zilikuwa hazimuhitaji kwa kipindi hicho?
Au timu kubwa zilikuwa hazina pesa ya kumnunua?
Au alikataa mwenyewe na kuchagua kwenda Bolton?

Kisha nakufahamisha wewe na wakurupukaji wenzio kwa kukwambia kuwa wakati Dinho anaondoka PSG alikuwa anagombewa na Man UTD na Barca.
Na yeye kwa mapenzi yake akahamia Barca ambayo ilikuwa imepotea ktk ramani ya soka ulimwenguni kwani hata Champions League yao ya mwisho kubeba ilikuwa 1992.

Ila kiumbe aliyeshushwa baada ya Kutua Catalunya akaisaidia Barca kushika nafasi ya pili ya ligi ya La Liga kwa msimu wake huo wa kwanza.
Na kisha msimu wa pili Barca walibeba La Liga na kisha Dinho akachaguliwa kuwa mwanasoka bora wa Dunia na wewe mwenyewe unaweza kuendelea na historia ya mafanikio ya mtakatiifu Gaucho.

So usikurupuke siku nyingine kufananisha Paa na Mbingu...
 
pia ukae ukijuwa kuwa Okocha hajawahi kuwa mwanasoka bora wa Dunia, Ulaya wala Africa.
Na pia cha kukusaidia ni kuwa Okocha anacheza mpira wa jukwaani na si mpira wa kufurahisha jukwaa na kuipa timu ushindi na makombe.
Mfano mzuri ni kuwa tangu amekuja Bolton je Bolton wamechukua kombe gani au je bolton waliweza hata kucheza champions league?

Msitake kuleta porojo zenu eti mseme Okocha hakuwa na bahati ya kukubalika na wazungu.
huo ni upuuzi uliopevuka kwa mtu mwenye utimamu wa akili kuwaza mambo hayo.
 
Hao wote ni sawa, ila naomba niende nje kdg ya hao tuwaongeleao.
Okocha ndie tunaweza kusema ni mchawi wa soka, japo hakutunukiwa mataji yoyote...ila ndie aliemuweka Gaucho benchi kwa kipindi chote walipokuwa pale PSG, na manjonjo mengi ya Gaucho aliyapata toka kwa JJ-Okocha. Bara zima la Africa halijapata kuwa na aina hii ya mchezaji mwenye kufanya lolote uwanjani na kwa mazingira yoyote yale.

Hebu taja hayo manjonjo ambayo MT Gaucho aliyapata toka kwa Okocha...

Dinho hajaanza miujiza akiwa PSG.
Kwa wewe usiyekuwa mfuatiliaji wa maswala ya Soka ndie unaweza kusema MT Dinho kajifunza skills akiwa PSG tena kwa kumuiga Okocha.
Ila kwa mtu timamu anamjuwa MT tangu alipotoka mpaka aliposasa na ukimuuliza atakwambia Ronaldo Assis ni nani.

So mtafute mwingine aliyefundishwa skills na Okocha na ndio umuandike hapa lakini si huyo mtakatifu ambaye kama mpira ungekuwa unaongea basi kuna siku ungeomba upelekwe kwa Dinho kwa dakika zote 90 ili ukachezewe na kufurahi pamoja na wewe mkurupukaji.
 
Kwa Okocha sawa kabisa nakubaliana na wewe yeye ni zaidi ya Gaucho kwa urembo wa uchezaji uwanjani, lkn kwa mipira ya George Weah ilinikuna zaidi, kuna mahali alipiga chenga mabeki watatu kwa mpigo mmoja na akamalizia kufunga goli kwa kumpitishia dobo kipa timu pinzani, ningekuwa na clips hapa ningezi-upload!

Nitajie kitu kingine ambacho Okocha kamzidi Gaucho ukiachilia mbali umri...
Nenda katafute Quotes za wachezaji mabeki wa ulaya wakimuelezea Mtakatifu Gaucho na kisha utagundua kuwa yule mstahiki ni wa Ligi ya Mbinguni na si wa kufananishwa na Okocha, kwani kufanya hivyo ni kuchuma dhambi tu.

Kuna beki ''sorry jina limenitoka'' aliwahi kusema ''ni heri uende porini na kisha upambane na Simba Dume lenye njaa kuliko upambane na Ronaldinho ''Dinho'' Gaucho uwanjani''.

Jiulize
 
Kuna siku nilicheki kipindi cha mahojiano cha George Weah na mwandishi, kuna baadhi ya clips walikuwa wanazionesha,Weah alicheza mipira ya ajabu sana, naona hata Ronadinho hajawahi kuvionesha akiwa uwanjani. Ronadinho kwa kweli hajamfikia Weah.

Sasa narudi kwako wewe muanzisha mada.
Ishu ni kuwa Wear na MT Dinho kwanza ukae ukijuwa kuwa ni wachezaji waliokamilika ktk namna za kiuchezaji wa soka.
Hawa pia wanazidi kuongeza mafanikio ktk CV zao kwa kuweza kuichezea AC Milan klabu yenye mafanikio zaidi hapa Duniani.

Lakini unapomuweka Wear na kumlinganisha na Dinho ni kukosa akili kwani hawa watu hucheza namba tofauti.

MT Dinho anaweza kuzurura winga zote na pia anaweza kucheza nyuma ya washambuliaji wawili.
Pia anaweza kutoa pasi za ajabu za mwisho tofauti ya Weah ambaye ni mmaliziaji mzuri wa pasi za mwisho.

tukirudi kwenye swala la skills mtakatifu Dinho aliwahi kuwavalisha kanzu wachezaji watatu tofauti waliokuwa wanamkaba...hii ilipelekea kanzu hizo akaziita ''el tripple' barret''.

Pia kama huamini haya ninayokwambia kuwa MT Dinho ni Mfalme wa Skills basi nenda wafuate John Terry na Calvalho kisha wanong'oneze na uwaulize ''je nani nguli wa skills Duniani?''.....jibu watakalokupa pigia mstari kisha ufunge bakuli lako.

na siku nyingine kama huna cha kuposti basi kachukue kopo ukachambe na si kumdhalilisha Ronaldo de Assis Moreirra.
 
Hao wote ni sawa, ila naomba niende nje kdg ya hao tuwaongeleao.
Okocha ndie tunaweza kusema ni mchawi wa soka, japo hakutunukiwa mataji yoyote...ila ndie aliemuweka Gaucho benchi kwa kipindi chote walipokuwa pale PSG, na manjonjo mengi ya Gaucho aliyapata toka kwa JJ-Okocha. Bara zima la Africa halijapata kuwa na aina hii ya mchezaji mwenye kufanya lolote uwanjani na kwa mazingira yoyote yale.

Hii ni kweli kabisa, katika maisha yangu sina mchezaji ninayeweza kumfananisha na Okocha.
 
Back
Top Bottom