George Simbachawene: Gesi Ya Mtwara; Gharama, Bomba na Mitambo

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,500
MRADI wa ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara na Songo Songo hadi Dar es Salaam, umegawanyika katika makundi mawili. Kwanza ni ujenzi wa mitambo miwili ya kusafishia gesi katika maeneo ya Songo Songo-Kilwa na Madimba-Mtwara Vijijini. Pili, ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi hiyo lenye vipengele vitatu. Kwanza ni kutoka Madimba-Mtwara Vijijini hadi Kinyerezi- Dar es Salaam lenye ukubwa wa kipenyo cha inchi 36 na urefu wa kilomita 487.

Kipengele cha pili ni kutoka kisiwani Songo Songo kupitia chini ya Bahari na kuungana na bomba linaloka Mtwara katika eneo la Somanga Fungu, lenye ukubwa wa kipenyo cha inchi 24 na urefu wa kilomita 25; kipengele cha tatu ni kutoka Kinyerezi hadi Tegeta, lenye ukubwa wa kipenyo cha inchi 16 na urefu wa kilomita 30. Jumla ya urefu wa bomba litakalojengwa ni kilomita 542.

Mitambo ya kusafishia gesi asilia

Gharama za mradi huu zinajumuisha, kwanza mabomba ya kusafirisha gesi kutoka kwenye visima hadi kwenye mitambo ya kusafishia pamoja na vituo vya kukusanya gesi hiyo (flowlines and gathering station). Hii ni tofauti na ujenzi wa bomba kuu la kupeleka gesi Dar es Salaam.

Pili gharama za mradi zinahusisha ujenzi wa mitambo miwili ya kusafishia gesi na tatu ni kuhusu ujenzi wa kambi za kuishi wafanyakazi wa mitambo ya kusafishia gesi na ofisi za kuendeshea mitambo hiyo.

Katika ujenzi wa mabomba ya kusafirisha gesi kutoka kwenye visima hadi kwenye mitambo ya kusafishia pamoja na vituo vya kukusanyia gesi hiyo (flowlines and gathering station), gharama yake ni dola za Marekani 18,211,000.

Lakini kwenye ujenzi wa mitambo miwili ya kusafishia gesi (Songo Songo-140 mmscfd- dola za Marekani 121,366,800 na Mnazi Bay-210 mmscfd- dola za Marekani 182,050,200, jumla ya gharama yake ni dola za Marekani 303,417,000, wakati ujenzi wa kambi mbili za kuishi wafanyakazi wa mitambo ya kusafishia gesi na ofisi za kuendeshea mitambo hiyo, gharama yake ni dola za Marekani 27,984,000.

Kwa hiyo, utabaini kwamba gharama ya jumla katika ujenzi wa mitambo ya kusafisha gesi ni dola za Marekani 349,612,000.

Bomba la kusafirisha gesi

Hapa kuna ujenzi katika maeneo manne. Kwanza ni ujenzi wa bomba kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Somanga Fungu. Pili, ujenzi wa bomba kuu kusafirisha gesi kutoka Somanga Fungu hadi Kinyerezi- Dare s Salaam.

Tatu ni ujenzi wa bomba kutoka Songo Songo kupitia baharini na kuungana na lile linalotoka Mtwara katika eneo la Somanga Fungu na nne; ni ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Kinyerezi kupitia Ubungo hadi Tegeta.

Tuanze na gharama za ujenzi bomba kuu kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Somanga Fungu (inchi 36, kilomita 290). Katika ujenzi huu, gharama ni dola za Marekani 379,794,598.

Lakini kwa upande wa ujenzi wa bomba kutoka Songo Songo kupitia baharini na kuungana na lile linalotoka Mtwara katika eneo la Somanga fungu (inchi 24, kilomita 25), gharama ujenzi ni dola za Marekani 174,542,400.

Katika eneo la tatu la ujenzi, yaani ujenzi wa bomba kuu la kusafirisha gesi kutoka Somanga Fungu hadi Kinyerezi jijini Dar es Salaam (inchi 36, kilomita 197) gharama yake ni dola za Marekani 257,998,399. Pia ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Kinyerezi kupitia Ubungo hadi Tegeta (inchi 16, kilomita 30), hili gharama za ujenzi wake ni dola za Marekani 15,025,209.

Lakini kuna gharama nyingine zinazoambatana na ujenzi huu ambazo ni pamoja na ujenzi wa karakana ya matengenezo ya bomba Somanga Fungu, gharama za dharura, gharama za vituo vya kupokelea gesi Somanga Fungu, Kinyerezi na Tegeta, pamoja na gharama za mitambo miwili ya kupunguzia mgandamizo wa gesi na gharama za kujenga ofisi. Hizi zote zimetengewa dola za Marekani 48,354,394 na kwa hiyo, gharama za jumla za ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi ni dola za Marekani 875,715,000.

Gharama ujenzi bomba la kitaifa

Kitaalamu, gharama za ujenzi wa boma hukokotolewa kwa kuzingatia urefu na ukubwa wa bomba, yaani kipenyo. Gharama hizi huwakilishwa kwa kiasi cha fedha kwa kilomita moja kwa milimita za kipenyo (USD/km.mm).

Hivyo basi, bomba la nchi kavu, kutoka Mtwara hadi Kinyerezi Dar es Salaam, likiwa na kipenyo cha inchi 36 na urefu wa kilomita 487, gharama yake ni dola za Marekani 1,309,637 kwa kilomita (US$/km) au dola za Marekani 1,426 kwa kilomita kwa milimita (US$/km.mm).

Bomba la nchi kavu, kutoka Kinyerezi hadi Tegeta lenye kipenyo cha inchi 16 na urefu wa kilomita 30, gharama yake (US$/km) ni dola za Marekani 500,840.3 au kwa dola 1,228 kwa kilomita na milimita (US$/km.mm) wakati bomba la baharini kutoka Songo Songo hadi Somanga Fungu, kwa kipenyo cha inchi 24 na urefu wa kilomita 25 ni dola za Marekani 6,981,696 (US$/km) au dola 11,408 (US$/km.mm).

Hoja za kuzingatia dhidi ya upotoshaji unaofanywa ni kwamba, hakuna ufisadi wowote. Na kwa kujua au kutokujua wanaozusha hoja hiyo wameshindwa kuwa makini na kutafiti ili kubaini ujenzi wa miundombinu kama hiyo huhusisha ujenzi wa ofisi na kambi kudumu za watumishi. Hii ni nchi yetu, tuipende na kuilinda kwa kusema ukweli.

Source:www.wavuti.com

Angalizo:
Kwa nini wizara ilikuwa inakumbatia maelezo ya gharama za mradi mpaka pale ilipopata shinikizo katika jamii kwa njia ya umwagaji damu. Hii wizara ya Nishati na Madini ina maswali mengi ya kujibu.
 
Huyu jamaa anavyotoa tuu huu mchanganuo wa jumla ndio itasaidia kweli kuaminisha GT Kuwa hakuna ufisadi?? Mbona hajaonyesha kama hizo price ni competitive? Atatuaminisha vipi kama hizo price hazijawa-inflated?? Kwa nini hakukuwa na open tender?

"wakati ujenzi wa kambi mbili za kuishi wafanyakazi wa mitambo ya kusafishia gesi na ofisi za kuendeshea mitambo hiyo, gharama yake ni dola za Marekani 27,984,000. " Huu ni wizi wa mchana kweupe kabisa kambi gani hizo za kuishi zinajengwa kwa dola 27M almost 50 Billion??? Au ndo wanajenga Mji wa Kigamboni? Hii laana ya ufisadi ipo siku itawala tu nyie ngojeni
 
hicho kilichotolewa ni maelezo ya jumla ya gharama; kitaalam kwa watu wanaofanya gharama za miradi haimsaidii kutolea hoja kwamba kuna ufisadi au la! Asante kwa maelezo;kama unaweza lete Bill of quantity ya mradi wote na sio haya maelezo ambayo yapo shallow kiasi hiki
 
"wakati ujenzi wa kambi mbili za kuishi wafanyakazi wa mitambo ya kusafishia gesi na ofisi za kuendeshea mitambo hiyo, gharama yake ni dola za Marekani 27,984,000. " Huu ni wizi wa mchana kweupe kabisa kambi gani hizo za kuishi zinajengwa kwa dola 27M almost 50 Billion??? Au ndo wanajenga Mji wa Kigamboni? Hii laana ya ufisadi ipo siku itawala tu nyie ngojeni

NI KWELI, LABDA AENDELEE KUTUFAFANULIA HIZO KAMBI NI ZA AINA GANI. Tusijedhani ni kambi kumbe ni "MIJI INAJENGWA". Hapa kuna walakini.
Naongezea, eti pale Kigamboni kwa awamu hii walitenga shilingi ngapi tena?
 
Nyie kila kitu mnallaamika. Mlikuwa wapi migodi iliporwa? Leo gesi inaenda kwa manufaa ya watz mnapiga kelele. Watanzania tunakwenda wapi?
 
Kwanza tuipongeze serikali at least kwa kusema ukweli sasa!. Hivi ni vitu ambavyo vilipaswa kusemwa kabla ili watu wawe well informed na hivyo kuzuia upotoshwaji wowote!.

Kiukweli, japo Simbachawene anatetea gharama hizo na kudai kuwa hakuna ufisadi, lets take time kufanya comparizon na ujenzi wa bomba kama hili kwenye nchi nyingine ndipo tujiridhishe tunaibiwa au la!.

Pili ili kuondoa mzizi wa fitna za kelele zote mradi huu wa gesi, mkataba uwekwe wazi, tunakopeshwa kiasi gani, kwa mashari gani, tunalipa riba kiasi gani na kwa muda gani, na jee tunalipaje huu mkopo!, aminini msiamini, niwajuavyo Wachina, usikute tutalipia deni hili kwa "gas export!" ndani ya kipindi cha miaka 100!.

Fununu za deni ni dola bilioni 1.2 kwa interest ya only 01%, with grace period ya 20 years na repayment time ya miaka 80!. Yaani deni ni la miaka 100!, katika miaka 100 hii, interest tuu pekeyake kabla hujaweka principal ni dola bilioni 1.2 na deni ni dola bilioni 1.2 hivyo tutalipa jumla ya dola bilioni 2.4!, kama mkopo ni wa dola bilini 1.2 na tunalipa jumla ya dola bilioni 2.4, then tumekopeshwa kwa riba ya 100%!.

Nimesema kuna uwezekano wa hili deni kulilipa kwa gas export, ukisikia gharama ya gesi itakayotumika kulilipa hili deni ndani ya hiyo miaka 100 na fedha ambazo zingepatikana kama gesi hiyo ingeuzwa utashangaa!.

Hii yote ni minongono tuu, dawa ya kumaliza minong'ono hii is to come clean na mikataba hii ya gesi.

Hili mimi nililizungumzia tangu mwezi Julai mwaka jana! Gesi asili: Is it "day light robbery?!"- watanzania tunaibiwa ..
Pasco.
 
Nyie kila kitu mnallaamika. Mlikuwa wapi migodi iliporwa? Leo gesi inaenda kwa manufaa ya watz mnapiga kelele. Watanzania tunakwenda wapi?
Hii siyo kelele, ni kuwajibika kwa nafasi na kwa lile watu wanajua. kama hukupinaga moja haina maana kuwa hata hilo lifuatalo usipinge.
Pia Migodi itaendelea kupingwa tu, sidhani kama kuna mtu anapenda hili.
Sijui kama una uhakika wa kiasi hicho kuwa ni kwa manufaa ya watz, HAYO YOTE YALISEMWA IVO IVO KUWA NI KWA MANUFAA YA HAO HAO WATZ!
 
Hivi pale Songosongo tayari kuna gas processing plant. Na hiyo submarine pipeline ya kutoka Songosongo kwenda Somanga Funga tayari ipo. Kwa nini wanajenga processing plant nyingine na pipeline nyingine?
Ndg. Waziri tunaomba maelezo hapo.
 
Huyu jamaa anavyotoa tuu huu mchanganuo wa jumla ndio itasaidia kweli kuaminisha GT Kuwa hakuna ufisadi?? Mbona hajaonyesha kama hizo price ni competitive? Atatuaminisha vipi kama hizo price hazijawa-inflated?? Kwa nini hakukuwa na open tender?

From the start, the whole issue was shamble. Katika hali ya kawaida, inapotokea jambo linaanza kufanyiwa spinning lazima kuna lake jambo. Wizara imekuwa kama haipo na pale ilipotokea ilikuja na majibu ya kejeri kwa wenye mali zao matokeo yake ndiyo haya, watu wamepoteza maisha na mali zao. Kwa nchi zilizoendelea hili ni tukio tosha linahitaji independent enquiry. Kwa Tanzania is just another day in office. Yetu macho.
 
"wakati ujenzi wa kambi mbili za kuishi wafanyakazi wa mitambo ya kusafishia gesi na ofisi za kuendeshea mitambo hiyo, gharama yake ni dola za Marekani 27,984,000. " Huu ni wizi wa mchana kweupe kabisa kambi gani hizo za kuishi zinajengwa kwa dola 27M almost 50 Billion??? Au ndo wanajenga Mji wa Kigamboni? Hii laana ya ufisadi ipo siku itawala tu nyie ngojeni
Sio bil 27 kaka ni 27,984,000x1500 = 41,976,000,000Ni 0ver 42 bil
 
Simbachawene anatakiwa aweke mkataba mezani watanzania wausome wenyewe. Na wabunge wa CCM kama hakuilazimisha serikali yao iweke wazi huo mkataba watakuja kulia na kusaga meno, 2015. Mkataba wa Kichina utakizamisha CCM. Sikio la kufa?
 
Sio bil 27 kaka ni 27,984,000x1500 = 41,976,000,000Ni 0ver 42 bil

Ni kweli bosi na nimesema almost 50B hiz 27M ni USD ,sasa hizo ni kambi gani zinajengwa kwa gharama kubwa hivyo? Kama sio wizi ni nini?
 
Kwanza tuipongeze serikali at least kwa kusema ukweli sasa!. Hivi ni vitu ambavyo vilipaswa kusemwa kabla ili watu wawe well informed na hivyo kuzuia upotoshwaji wowote!.

Kiukweli, japo Simbachawene anatetea gharama hizo na kudai kuwa hakuna ufisadi, lets take time kufanya comparizon na ujenzi wa bomba kama hili kwenye nchi nyingine ndipo tujiridhishe tunaibiwa au la!.

Pili ili kuondoa mzizi wa fitna za kelele zote mradi huu wa gesi, mkataba uwekwe wazi, tunakopeshwa kiasi gani, kwa mashari gani, tunalipa riba kiasi gani na kwa muda gani, na jee tunalipaje huu mkopo!, aminini msiamini, niwajuavyo Wachina, usikute tutalipia deni hili kwa "gas export!" ndani ya kipindi cha miaka 100!.

Fununu za deni ni dola bilioni 1.2 kwa interest ya only 01%, with grace period ya 20 years na repayment time ya miaka 80!. Yaani deni ni la miaka 100!, katika miaka 100 hii, interest tuu pekeyake kabla hujaweka principal ni dola bilioni 1.2 na deni ni dola bilioni 1.2 hivyo tutalipa jumla ya dola bilioni 2.4!, kama mkopo ni wa dola bilini 1.2 na tunalipa jumla ya dola bilioni 2.4, then tumekopeshwa kwa riba ya 100%!.

Nimesema kuna uwezekano wa hili deni kulilipa kwa gas export, ukisikia gharama ya gesi itakayotumika kulilipa hili deni ndani ya hiyo miaka 100 na fedha ambazo zingepatikana kama gesi hiyo ingeuzwa utashangaa!.

Hii yote ni minongono tuu, dawa ya kumaliza minong'ono hii is to come clean na mikataba hii ya gesi.

Hili mimi nililizungumzia tangu mwezi Julai mwaka jana! Gesi asili: Is it "day light robbery?!"- watanzania tunaibiwa ..
Pasco.

You are right mkuu watuwekee Mikataba hadharani tujiridhishe hapa kuna harufu kali sana ya ufisadi halafu wanajifanya kupulizia Perfume haisaidii kitu dawa ni kuondoa uchafu tu
 
Umeme wa gesi umeyeyukia wapi baada ya kuingia gharama kubwa sana za pesa za walipa kodi?
 
Back
Top Bottom