Genius bibi kizee

aduwilly

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
1,176
305
Bibi kizee mmoja alidondosha shilingi 1,000, akawa anahuzunika na kulaani sana, basi mjukuu wake akamwambia, bibi usijali kwani hiyo ni sawa na kutoa sadaka na Mungu atakulipa mara kumi zaidi.

Basi baada ya siku kama mbili yule bibi kizee akaokota noti ya shilingi 10,000,kuona vile akaamua kuliuza shamba lake shilingi milioni 1 kisha akaenda kuzidondosha maeneo yale yale aliyoangushia shilingi 1,000 (ili baadae apate milioni 10 kama alivyodondosha shiling 1,000 akapata shilingi10,000)
 
Back
Top Bottom