Genge laundwa kumkabili Kikwete: Agenda 21?

Huu msigano wa wanamtandao itakuwa neema kwa watanzania kama rais atakuwa na ujasiri wa kuwatosa. Vinginevyo itakuwa balaa kwa taifa. Lowasa alipokwenda kwao alipokelewa kama shujaa. Jana Chenge si tu kapokelewa kama shujaa, lakini alipata ujasiri wa kusema kuwa mnyantuzu hawezi kunywa sumu afe na kuacha vijisenti vyake. Nashindwa kuamini kuwa ujasiri wao hautokani na ukweli, kama ilivyoandikwa na mwanahalisi, kuwa mambo haya ya ufisadi waliyafanya pamoja au alijua kuwa waliyafanya na yalimnufaisha. Mwalimu alikuwa rafiki mkubwa wa Kambona lakini walipo part njia ilibidi Kambona akimbie nchi. Nashindwa ku imagine kuwa Kambona angekwenda kwao Manda na kutamba mbele ya wananchi. Call it dictatorship or anything.
 
Je Kuna Mtu anamuweza Jk.kuna mambo ambayo watu hawajafahamu kuhusu Muungwana.He knows what he is doing,na ndiyo sababu ya kuweka ndugu zake na rafiki zake katika nafasi za juu za usalama ili waweze kumsaidia pindi wakitokea watu wa kumgeuka..hauhitaji macho kutambua hili..
 
Washindwe na walegee,JK kaza buti raia maskini wa Taifa hili tuko nyuma yako
 
Washindwe na walegee,JK kaza buti raia maskini wa Taifa hili tuko nyuma yako
Mkuu Njowepo naungana na na wewe sisi wananchi ndiyo wenye uwezo wa kumlinda Rais. Kikundi hicho kidogo hakina uwezo wa kutanua kiasi hicho. Nami nasema WASHINDWE, WALEGEE NA WAPARARAIZI.
 
Hivi siku hizi huu ubunge ni kama ka njia ka kuingilia kwenye ufisadi wa daraja la juu? Ukiangalia juhudi na resources zinazotumiwa na hao wanaojiita wana-ccm kuutafuta huo ubunge inanitisha!!!

Ama kweli CCM ni chaka la kuficha majambawazi.....
 
Washindwe na walegee,JK kaza buti raia maskini wa Taifa hili tuko nyuma yako
Mkuu Njowepo naungana na na wewe sisi wananchi ndiyo wenye uwezo wa kumlinda Rais. Kikundi hicho kidogo hakina uwezo wa kutanua kiasi hicho. Nami nasema WASHINDWE, WALEGEE NA WAPARARAIZI.
Totally nosense, mshindwe na mlegee wenyewe maskini gani walio nyuma ya jk, labda wa akili.__________________
 
Hii habari inajitahidi kutuonyesha kuwa JK ni mtu makini na "mjanja" sana, wakati si hivyo! Mara nyingi amepata nafasi ya kuonyesha umakini wake lakini ameshindwa! Na wapinzani wake (kama anao) wanalijua hilo!

Na sasa tunamsubiri kwenye ile agenda yao ya "siri" wanayokwenda kujadili hivi karibuni!
 
kubenea hii habari au hadithi!! hakuna jina hata moja katika habari nzima!
 
Ndio maana nasema hii habari inahitaji ukweli zaidi na hasa ushahidi maanake inawezekana hizi habari zinatungwa na waandishi wa habari ama jamaa kutuonyesha kwamba JK amejenga maadui...hali hakuna hata kiongozi mmoja aliyefikishwa mahakamani, kupoteza mali zake na bado wanabeba Ubunge dhamana kubwa ya wananchi...
Hatuwezi kuendelea kuwa wajinga wa habari hiyo ya Agenda 21 ni mtungo wa tenzi...
Wafanyaji mambo hawasemi, hufanyiza kama mbwa...
 
Je Kuna Mtu anamuweza Jk.kuna mambo ambayo watu hawajafahamu kuhusu Muungwana.He knows what he is doing,na ndiyo sababu ya kuweka ndugu zake na rafiki zake katika nafasi za juu za usalama ili waweze kumsaidia pindi wakitokea watu wa kumgeuka..hauhitaji macho kutambua hili..

..nawe kuna mengi hujafahamu kuhusu hii issue. anyways,utafahamu tu as time goes!
 
Ndio maana nasema hii habari inahitaji ukweli zaidi na hasa ushahidi maanake inawezekana hizi habari zinatungwa na waandishi wa habari ama jamaa kutuonyesha kwamba JK amejenga maadui...hali hakuna hata kiongozi mmoja aliyefikishwa mahakamani, kupoteza mali zake na bado wanabeba Ubunge dhamana kubwa ya wananchi...
Hatuwezi kuendelea kuwa wajinga wa habari hiyo ya Agenda 21 ni mtungo wa tenzi...
Wafanyaji mambo hawasemi, hufanyiza kama mbwa...

Watanzania sie ndo akina Tomaso.Mpaka mpapase ndo muamini.Mliambiwa JK hawezi kitu hamkuamini mpaka mmepapasa. Sasa mnaambiwa ya ajenga 21 yapo mnasema hakuna,mnasubiri kupapasa.

Kubenea kawaletea nyepesinyepesi ambazo sio habari za uchunguzi, mnataka majina. Akitaja majina na akipelekwa mahakamani hatukawii kusema kwa nini hakuandika habari bila kuandika majina.
 
Da!!! hii inaweza kuwa kweli? sijui, lakini hawa jamaa zake wanaweza kumsaliti na kumdhohofisha JK? Kamwe hiyo haitatokea, msisahau Jk amewasahe kwa yote yale tunayoyajua.
 
Kama kweli kuna genge ambalo linaandaa njama za kumwondoa Kikwete inafaa kujiunga nalo. Kazi ya kumwondoa ikishafanikiwa, kwa sababu na genge hilo nalo ni uzao huo huo, inafaa kuligeuka nalo kuliondoa ili madaraka yashikwe na wengine ambao si wa uzao huo
 
Luyungu,
Labda lugha zetu zinagongana.. Kikwete hawezi kitu ni hoja inayokubaliwa na wengi bila kupapasa kwa sababu yeye ndiye ngao ya hawa agenda 21. Habari inayotolewa hapa ni kinyume..yaani inaonyesha kuna uwezekano Kikwete akafanya kweli (KAWEZA)...hivyo Mafisadi wanajiandaa kujibu mapigo...
Habari hii ni uzushi mtupu, mfanyaji kweli hajitangazi wala kusema nitawashitakia wananchi.
Hivyo basi,hakuna kinachoendelea hapa wala haja ya kupapasa kwa sababu hatupo kizani.. Kikwete hana maadui isipokuwa washikaji na hili deal ni tungo za tenzi kwa sababu nani kati yao anaweza kusimama against Kikwete anayewaweka huru mjini..
Ukimwondoa Kiwete hapo kitini mkuu hakuna msalie kwa hawa jamaa na kwa taarifa yako nusu ya wabunge na wana CCM wanasubiri tu Kikwete afanyize ama atoe go ahead.kasindwa siku nyingi ndio maana wanajiuzuru tu kuondoa usiku.
Kwa hiyo ni ujinga mkubwa kufikiria Kikwete anaweza kuwa na maadui leo hii wakati ni yeye ndiye Umsolopagazi wa mlango mkuu.
Just imagine Kikwete kesho hatolewa Urais nani atashika nafasi hiyo na kuna uwezekano gani wa kuigawa CCM for good.
 
hiyo ni flashback,,,,ni gazeti la mwanahalisi mwaka 2008,,,

so kumbe mafisadi walianza kumsakama kikwete miaka miwili na nusu tu tangu achukue madaraka na baada tu ya lowasa kujiuzulu....

kosa kubwa la kikwete ni kujitenga na mafisadi na kutowasaidia wanapobambwa na scandal......

no wonder kikwete kabadili sana baraza la mawaziri,kumbe ilikua aina fulani ya kujaribu kupata watu waadilifu....

so pia hapa ni wazi kuwa mr lowasa ndiye kwa miaka yote hii amekua kinguge wa mafisadi waliokua wakiichokonoa kila mara serikali ya jk...

ha ha ha,mi nilikuaga nashangaa,mbona huyu lowasa anakaa bungeni kimya kama bubu,,,,,,kumbe,,,,,,,,,,,
 
Hii aliyoitupa sasa ndio karata yake ya MWISHO...
Hapa ni kazi tu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom