Gen. Ndomba amrithi Shimbo

Status
Not open for further replies.
Naomba nielemisheni wana JF mimi hufikiri kuwa JKT ni jeshi dogo kwa JWTZ sasa mtu wa JKT kuingia JWTZ hivi inakuwaje?
 
Disgusting. CDF, from JKT. Chief of staff, from JKT. Hawa kweli ni wapiganaji?

kwani wewe unaelewa nini mtu akikwambia kuwa Juma alikua CNS-Chief of national service amekua CDF ?au tatizo lako ni kusikia katokea JKT?
 
Naomba nielemisheni wana JF mimi hufikiri kuwa JKT ni jeshi dogo kwa JWTZ sasa mtu wa JKT kuingia JWTZ hivi inakuwaje?

Jeshi ni moja (TPDF) ndani yake kuna Makao Makuu ya jeshi na kamandi nne ambazo ni kamandi ya nchi kavu, ya anga, ya majini na JKT. Mwanajeshi yeyote anaweza kupewa majukumu katika mojawapo ya hizo kamandi kama itakavyoonekana inafaa.

Hii kamandi ya JKT ilianzishwa kisiasa zaidi baada ya vijana wa TANU kutoa ushauri huo. Lengo kuu lilikuwa ni kujenga uzalendo.
 
Ahsante kwa maelezo, sasa hawa JKT si tungewatumia kujenga miundombinu ya nchi kama jina lao linavyojieleza badala ya kukaa tu huko maporini wanakula bure!
 
Ahsante kwa maelezo, sasa hawa JKT si tungewatumia kujenga miundombinu ya nchi kama jina lao linavyojieleza badala ya kukaa tu huko maporini wanakula bure!

Political will ndiyo inayokosekana otherwise vijana wako tayari kwa kazi ya kulijenga taifa lao.
Mkuu, kuna wakati tulianzisha shughuli za kujitolea kitaalam katika shughuli mbalimbali za serikali, huwezo amini jinsi tulivyopigwa vita na wale tunaotaka kuwasaidia ingawa wao walikuwa wanalipwa posho sisi tunafanya kazi ya kujitolea bure, lakini walikuwa wanatuona kama maadui. Mwishowe wakatupa live kuwa hawahitaji msaada wetu. Hiyo ndio Tanzania na watu wake!!!
 
Tatizo lililokuwa limelikumba jeshi letu la ulinzi ni madai ya uingizaji wa siasa jeshini, na chembe za udini kushamiri ndani ya jeshi.
Asasi pekee nchini ambayo nahisi bado haijaingiliwa na uoza wa haya mawili ni jeshi, hasa katika ngazi za juu kama hii ya Unadhimu Mkuu wa Jeshi. Nasema hivi kwa sababu jeshi la ulinzi halishughuliki na [mambo ya ki] raia moja kwa moja tafauti na jeshi la polisi ambalo hupokea amri za wanansiasa.

Kuhusu udini jeshini ndio kabisa, hili halipo. Nahisi huwa ni sisi wenyewe tunaojenga mlima kutokana na kichuguu kwa tabia yetu ya Kitanzania ya kulalamikalalamika, kulialia ovyo na kukosa kila kitu, baada ya kuangalia mteuliwa anatoka dini gani. Imekuwa ni kawaida kwetu akiteuliwa Mkristo, Waislamu hulalamikia udini na akiteuliwa Muislamu Wakristo hulalamikia udini, kwa ubinafsi wetu wa kutaka tumuone mtu wetu akiongoza asasi hiyo, wakati masikini mteuliwa mwenyewe haendi kutoa misa kanisani wala hotba msikitini. Dini imekuwa ndio siasa zetu, na siaa zimekuwa ndio dini yetu.

Tuache hizo Watanzania, tujadili maendeleo!

Ninampongeza Jenerali S. A. Ndomba kwa kuteuliwa na ninamuombea ufanisi katika kazi yake.
 
Ahsante kwa maelezo, sasa hawa JKT si tungewatumia kujenga miundombinu ya nchi kama jina lao linavyojieleza badala ya kukaa tu huko maporini wanakula bure!

jifunze kutoropoka kwa kitu usicho kijua.Nani kakwambia kuwa askari wa JKT wanakula bure?au unataka kila wafanyalo watoe taarifa kama mbunge?
 
Ana sifa ndio maana kateuliwa si kwa sababu ya Ukristo, ndugu zangu kwa huu udini wenu hamtafika kokote.

Nakubaliana na wewe ni sababu ya uwezo wake- ingependeza sana kama teuzi nyingine pia watu wangeamini hivyo, kwamba ni sababu ya uwezo na wala sio dini ya mtu!!
 
Political will ndiyo inayokosekana otherwise vijana wako tayari kwa kazi ya kulijenga taifa lao.
Mkuu, kuna wakati tulianzisha shughuli za kujitolea kitaalam katika shughuli mbalimbali za serikali, huwezo amini jinsi tulivyopigwa vita na wale tunaotaka kuwasaidia ingawa wao walikuwa wanalipwa posho sisi tunafanya kazi ya kujitolea bure, lakini walikuwa wanatuona kama maadui. Mwishowe wakatupa live kuwa hawahitaji msaada wetu. Hiyo ndio Tanzania na watu wake!!!

Ni balaa kama Manpower ipo halafu sisi tunahangaika tu hapa tunatafutana uchawi!

Ukute hawa jamaa wangewezeshwa utalaam tungekuwa tumetia lami na kujenga madaraja nchi nzima!!

Ndio bongo tena hii yetu macho!
 
Asante kwa taarifa mkuu Maxcence, hopeful ameteuliwa kwa stahili na hana mrengo wa kisiasa!!! Yaani kutumikia chama badala ya wananchi.

Huyu hakuwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kama siyo Mkuu wa Wilaya? Kazi za hivyo vyeo vya wakuu wa mkoa au wilaya si ziko kwenye katiba ya CCM?
 
jifunze kutoropoka kwa kitu usicho kijua.Nani kakwambia kuwa askari wa JKT wanakula bure?au unataka kila wafanyalo watoe taarifa kama mbunge?

Lets say they are being underutilised will that be okay with you?

Ukiangalia namba ya wanajeshi tulionayo na gharama tunazotumia kwenye jeshi unadhani ina justify ukilinganisha na umaskini huu? au ulifikiria kula nazungumziwa ugali tu?

Zaidi ya kwenda kwenye parade na kurudi home hebu nambie kazi nyingine kubwa zinazofanywa?
 
Kwani kupewa hvyo vyeo mpaka wapandishwe kuwa sijui ma luten, na kama ni hivyo kwani hakuna waliofikia huo u luten wapewe hizo nyazifa? naomba kujuzwa bandugu
Ndiyo! Mnadhimu wa JWTZ lazima awe Luteni Jenerali na Mkuu wa JWTZ lazima awe Jenerali!

Hivyo JWTZ lina Jenerali mmoja na Luteni Jenerali mmoja!
 
Maundumula, usichokijua usihitimishe, ila uliza. Paka akifukuza panya wote nyumbani akibaki kwako utasema hana kazi. Unapenda uingie vitani ili ujue wanajeshi wanafanya kazi? Nenda mipakan halafu ulete ***** wako hapa jf.
 
Lets say they are being underutilised will that be okay with you?

Ukiangalia namba ya wanajeshi tulionayo na gharama tunazotumia kwenye jeshi unadhani ina justify ukilinganisha na umaskini huu? au ulifikiria kula nazungumziwa ugali tu?

Zaidi ya kwenda kwenye parade na kurudi home hebu nambie kazi nyingine kubwa zinazofanywa?
Inawezekana uko sahihi kwa kusema kuwa jeshi letu ni kubwa mno lakini si sahihi kuwa wanafanya paredi tu!

Ili ufanye jeshi letu liwe dogo na madhubuti ni lazima wawe na zana za kisasa ambavyo vinakuwa operated na watu wachache lakini kama hakuna zana za kisasa za kutosha ni lazima kuwa na jeshi kubwa kwa maana ya idadi ya watu!

Kwa sasa jeshi letu linafanya kazi nzuri sana katika nyanja za kimataifa kwa kufanya kazi za kulinda amani. Hata hapa nchini hali hii tuliyonayo ni kutokana na nidhamu ya hali ya juu ya jeshi letu otherwise kungekuwa na hekaheka kila mahali!
 
Basi tuwape wananchi sababu nyingi zaidi za kuwa proud na jeshi lao kwa kushirikisha hawa wanajeshi kwenye miradi ya maendeleo kama ujenzi wa miundombinu, kilimo cha kisasa nk sio kusubiri hadi maafa yatokee ndio waende kuokoa jahazi.
 
Maundumula

Sio kuwa JKT ni dogo tu kwa JW Bali ni idara "kamandi'' mojawapo iliyo ndani ya JW na inaongozwa na Major Gen kama kamandi nyngne tatu, kiUtawala Majos Gen wote ni candidates wa uLuten General so ni sawa Huyu Ndomba kutoka JKT kwakua vyeo vya kijesh ni Universal
 
Last edited by a moderator:
asilimia 40 nyingine tukampigia kura mtu ambae hatujui kwa nini alivuliwa upadri!
Labda wewe unajua!

Hakuvuliwa.Inasemekana aliamua yeye mwenyewe kuacha upadri na kuingia kwenye siasa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom