Gen. Ndomba amrithi Shimbo

Status
Not open for further replies.
Hongera gen.shimbo,hongera jk kwa uteuzi mpya.matarajio yetu ni utendaji uliotukuka
 
Hongera yake, huyu Samuel Ndomba alishawahi kuwa mkuu wangu wa wilaya. Na sasa mtoto wake Allan ni mwanasheria wetu dah!
 
Tatizo lililokuwa limelikumba jeshi letu la ulinzi ni madai ya uingizaji wa siasa jeshini, na chembe za udini kushamiri ndani ya jeshi.

Simujui kwa undani Jenerali Ndomba, lakini kwakifupi inatajwa kuwa huyo ni moja ya masalia imara ya vijana wa Mwalimu Nyerere walioamini katika UZALENDO.

Nimtu mashuhuri mwenye uso wa kijana akijitunuku tabasamu la nidhamu ya kijeshi, wadadisi ndani ya SIASA za kijeshi wanamtaja kuwa ndie mrithi stahiki wa Mkuu wa Majeshi Aden Mwamunyange.

Anatajwa kuwa ni kijana na tokezo la akina Jen Waitara, Jen Mboma na Jen Mwamunyange.

Naamini katika safari hii iliyo ndefu na inayokaribia ukingoni yakulikomboa Taifa letu, General Ndomba asiwe kikwazo wa mageuzi haya ya kiraia yenye kuongozwa na alama za nyakati ambazo kihistoria na kimaandiko hazijawahi kupingwa kwa mtutu wala kombora.

kama tunakiri kuwa wakuu wa wilaya wanafanya kazi za ccm, Ndomba alishawahi kuwa mkuu wa wilaya
 
Shimbo hahitaji tuzo au pensheni kama kuna ukweli kwamba alipeleka matrilioni ya shilingi huko Afrika Kusini. Anaweza tu kwenda Uswisi na kuanza kutumia akiba yake.

Hivi tumepata kuarifiwa alizipata pataje hizo fedha? Ni kutokana na kuagiza zana feki za vita?
 
8E9U5294.jpg


SIKUJUA NI MZEE as WELL...
 
Kinachonishangaza siku hizi ni kwamba ili uje kuwa General na Luteni General lazima upitie na kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwanza. Mwamunyange, Shimbo na sasa Ndomba wote wamepita huko. Na kama sijakosea hata kina George Waitara nao walitokea JWTZ then JKT kabla ya kuwa Full General.

Sijui ndiyo formula au vipi!

TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),

tumbiri@jamiiforums.com
 
Kwani kupewa hvyo vyeo
mpaka wapandishwe kuwa sijui ma luten, na kama ni hivyo kwani hakuna
waliofikia huo u luten wapewe hizo nyazifa? naomba kujuzwa
bandugu

ndo hivo!mnadhimu mkuu kwa ukubwa wa jeshi letu lazima awe luteni kanali na ni mmoja tu nchi nzima,kwa hiyo lazima apandishwe na niyeye pekee mwenye cheo hicho!Nampongeza sana!
 
Sasa ni wakati muhafaka wa kudeal na huyu shetani Shimbo, hivi Tanzania hatuna sheria ya kufanya upelelezi binafsi na kumfungulia mtu mashtaka binafsi? huyu Shimbo amedhulumu sana ndugu zetu pesa za UN.
 
I hope hataingiza siasa jesheni kama alivyofanya Shimbo. Muda utaamua.

False Hopes.. So do u expect him to against na aliemteua??? These things never happen out of nowhere NOT in my beloved country Tanzania, Am sure keshapewa List ya Do's & Donts.........
 
Ni rafiki mkubwa wa JK sababu ya utendaji wake na msimamo wake!!alishapendekezwa hapo nyuma kumrithi Dr Hosea pale Takukuru!iliposhindikana akapewa utumishi jeshini,baadae akaenda JKT,,,ni mchapakazi sana na hodari!Hongera JK kwa hilo!

Ni spy aliyebobea pia....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom