Administrator said:TVT Walinyimwa kibali na Bwana Sauper
Mwanagenzi said:Wazee,
Kuna mtu alifuatilia kuhusu ile filamu ya Mererani ilipoonyeshwa Marekani?
Wachimbaji wenyewe wanadai kuwa filamu haina ukweli na wanadai kuna njama (conspiracy theory)...
Wazee, na hasa mliochangia mada hii huko nyuma mnasemaje?
AREMA waipinga filamu ya utumwa migodini
Na David Frank, Arusha
CHAMA cha Wachimbaji Wadogo wa Madini Mkoa wa Arusha (AREMA), kimeipinga filamu ya watumwa wa vito ambayo inaonyesha utumikishwaji wa watoto wadogo katika machimbo ya tanzanite, na kudai kuwa ina lengo la kushusha thamani ya madini hayo katika soko la dunia.
Taarifa ya AREMA kwa vyombo vya habari, iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Isaya Latema, imeeleza kuwa madai ya watoto kutumikishwa katika migodi hiyo si ya kweli.
Tunapenda kuujulisha umma wa Watanzania na ulimwengu mzima kwamba, madai kuhusu utumikishwaji wa watoto katika migodi ya tanzanite Mererani si ya kweli, na kwamba lengo la filamu hiyo ni kushusha thamani ya madini na mpango huu umeandaliwa na kundi ambalo tunalifahamu, ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Alisema filamu hiyo iliyoandaliwa na Shirika la Habari la IRIN imetengenezwa katika eneo maarufu la Machekecho ambalo tayari serikali ililifunga kutokana na kutokuwa na udhibiti na kusababisha vifo vya wachimbaji hao.
Alisema lengo la filamu hiyo ni kuporomosha biashara ya madini ya tanzanite Mererani ambayo hivi sasa imekua na kuingiza sh zaidi ya bilioni 300 kwa mwaka.
Katibu huyo ameeleza kuwa, pia madai hayo ya kutumikishwa watoto hayana msingi, kwani waandaaji wa filamu hiyo wangeweza kuwataja wamiliki wa migodi waliyochukua picha kwani migodi yote ipo kisheria na tayari imepiga marufuku utumikishwaji watoto.
Hata hivyo, chama hicho kimeiomba serikali kukanusha kwa nguvu zote filamu hiyo kwani ina lengo la kuwadhoofisha wachimbaji wadogo ambao hawana nguvu za kujitangaza kimataifa ili wauze madini yao.
Source: Tanzania Daima
HELA za ManyokaAdmin,
Nina imani kwa kuwa uko karibu na hao jamaa huko, watakuwa wamepata ujumbe