Geita: Mapambano makali polisi, raia mgodini - raia mmoja auawa

Nchi inauzwa mchana kabisa na baadhi yetu tunashangilia uonevu wa watanzania wenzentu kwa kisingizio cha sheria lakini hawaoni mwanzo wa tatizo ni kuwaondoa wao na kumpa mtu mwingine bila kujali mamia hao wanaondoka wanakwenda wapi? Iko siku inakuja FF anasema labda kuna kikundi kina mobilize hizo fujo, ni kweli kipo kikundi kinacho nufaika na raslimali za nchi na kuwasahau raia wa nchi hii, hao ndio wanaomobilize hizi zinzoitwa fujo na siku yao ikifika sheria itawahukumu kama sio umma huu wa watanzania ndio utakao toa hukumu!
 
mwita na candida, kwani serikali ikifanya maamuzi haraka na kuwa-organise wananchi kwa ajili ya kufanya uchimbaji ingekuwaje? na nyie mnaona suluhisho ni wawekezaji kwenye kila kitu?

natamani ningeweka machozi hapa ila nimeshindwa! Hivi hawa jamaa ndo wale wenzao na wahindi wa rites waliotumwa kuuwa reli ili kutuharibia barabara nn? Wananchi wakichmba madin wajenge nyumba bora wanaitwa wavamizi,wanapigwa na polis,wanauawa. Mwekezaji akija kuchukua madini na kuturudishia 3percent ya asilimia moja ya madini anayoondoka nayo mnamshangilia,mnampa ulinzi, masikio yote! Mungu walaani hawa watu na vizazi vyao vyote!
 
Wakiwachiwa wavamie bila sheria nchi itakuwa haikaliki, kila ataetamani akionacho atataka kukivamia bila kufata sheria na kanuni zilizopo.

Fitna moja kubwa katika dunia ni "mali".

Kinachotakiwa ni Serikali kuwa makini katika kugawa sehemu za wachimbaji wakubwa na sehemu za wachimbaji wadogo, ambako kila mmoja atafata sheria na kanuni zilizo wazi. Na nna uhakika sheria na kanuni hizi zipo, kwa kuwa zipo, tatizo ni nini? Amma usimamizi usiotosha, amma kucheleweshwa kwa kutolewa vibali, hukumu na miongozo ya malalamiko kwa sehemu husika amma kuna kikundi cha watu kilichoandaliwa kuanza kuchochea hizi fujo,

Hili la mwisho lina maana zaidi na kama kipo kitajulikana, watajulikana na watasulubiwa kwa mujibu wa sheria
.


duh! FF nilikuwa najiandaa kukugongea like hapo, kwa maelezo uliyoanza nayo, lakini nilipofika hapo penye blue, Upheeeeeew! Vidole vyangu vikagoma kubofya kipanya. Anyways watu wakichoka kuisubiria haki itendeke, watatenda yasiyo ya haki. Na ndicho kinachotokea sasa
 
kwa taarifa wameshafika sita, na hio sehemu watu wa kijijini hapowalikuwa wana chimba miaka yote .kilichofanyika ni muafirka mwanzao alipopata pesa akawageuka na kwenda kupata hati miliki ya eneo hilo wala sio mwekezaji mgeni na ni mzaliwa wa hapo hapo nyarugusu
 
Kwenye movie ya SARAFINA walimkamata yule kibaraka wakampa kipigo halafu wakachoma moto, nadhani kuna mijitu humu ndani inastahili the same punishment! Haiwezekani tunaongea kitu halafu mpuuzi mmoja anahoji ujinga, laiti ungejua!

Unakumbuka hii akili ya TANU? "Kuna njama za kuhujumu na kudhulumu mtu na uchumi wa Mwafrika daima dumu. Njama hizi si ndogo, ni kubwa na zinatekelezwa usiku na mchana na mabepari wa dunia nzima. Udhalimu wa mabepari hawa kamwe hauwezi kufanikiwa bila ya kuwatumia Waafrika wenzetu limbukeni wachache wenye tamaa za ukubwa na uroho wa utajiri wa harakaharaka. Limbukeni hawa ni lazima tuwakomeshe!"
 
Mambo mengine watanzania mnajitakia wenyewe! Hiyo serikali mnayoilalamikia inawasumbua na kuua raia si mliiweka madarakanni kwa kura zenu wenyewe? Tesekeni tu hadi mtakapopata akili!

Ni kweli kabisa lakini bado ni safari ndefu bado kwa sababu wanaoteswa sana na serikali hii ndio hao hao wanaoongoza kwa kuipigia kura. Sijui tuna laana gani
 
serikali imezidi kukumbatia sana wawekezaji,kuna viongozi wachache sana wanaofaidika na haya madini ya hii nchi,
bora wavamie tu,maana watakuwa wajinga kuwa masikini wakati wanapoishi kuna utajiri na wageni wanachimba madini na kuondoka
 
Mungu ibariki Tanzania,ibariki CDM iingie madalakani ili iutoe udhalimu huu na wananchi wapate uhuru wa kweli hatimae wafaidi matunda ya nchi yao.
 
mchangiaji mmoja katika mdahalo jana aliifananisha Tanzania na hawa wavamizi kama; majambazi waliovamia nyumba na kumwomba mwenye nyumba wamuibie na awaambie na walinzi wake wawalinde wakati wanaiba endapo watoto wa huyo mwenye nyumba wakiamua kukabiliana nao. hii inaonesha wazi kuwa serikali yetu inauza nchi kwa wawekezaji na kuua raia yeyote atakaeonekana kupinga uuzaji huu
 
Naomba ufute jna lako la Mwita 25, kwani nahisi ww si Mtanzani! Ulishawahi lala na asubuhi ukaamka ukakuta serikali imekuwekea gunia la pesa pembeni ya kitanda chako? Hawa ndugu zetu wanajua ni wapi riziki yao ya kila cku inakopatikana! Sioni sababu ya wao kuirudia serikali kuitaka ifungue migodi kwani serikali ya sasa si sikivu kiasi cha kuiamini ktk maamuzi yanayogusa maisha ya watu moja kwa moja.

Ombi langu: Liandaliwe kongamano la wana JF wote ili tutambuane kwa kwani kwa sasa naona kama kuna watu wametumwa!
 
Eeh Mungu wa rehema tunakuomba uturudishie mwl nyerere japo kwa siku chache aje ajionee huu unyama unaotendeka kwa watz wenzetu wasiokuwa na hatia. Eeh baba tunakuomba chondechonde. Utajiri wetu unatuua wenyewe kwa manufaa ya wachache baba.
 
Sio haki hata kidogo kuwalaumu polisi kwa mauaji! Polisi hawana makosa bali wanatimiza tu ahadi za utii kwa serikali mliyoichagua wenyewe! Hayo mateso, dhuluma, rushwa na mauaji, watanzania mnajitakia wenyewe! Watu wakifa kwa mtindo huo, ndio mtapata akili ya kuondoa ushabiki kama ule wa Simba na Yanga wakati wa uchaguzi. Kama hamuoni sababu ya kuichagua serikali inayotumia jeshi la polisi kuwalinda na baadala yake mkaichagua serikali inayotumia jesi la polisi kuwaua, sasa mnamlamikia nani?
 
mwita na candida, kwani serikali ikifanya maamuzi haraka na kuwa-organise wananchi kwa ajili ya kufanya uchimbaji ingekuwaje? na nyie mnaona suluhisho ni wawekezaji kwenye kila kitu?

Nimekukubali mkuu kwenye hili .Yes wazo zuri sana .
 
Back
Top Bottom