Geita iko gizani kwa saa ishirini na nne sasa

mwanamapinduko

Senior Member
Jan 24, 2011
178
41
Wakuu nimeongea na jamaa yangu yuko Geita ameshindwa kukamilisha kazi kwani mkoa huo mpya hauna umeme sasa kwa masaa 24 mfululizo sasa na hawajapewa taarifa yeyote.

Licha ya kuwa kando kidogo ya mji huo kuna utajiri wa mkubwa wa dhahabu ambayo inaibwa na wazungu wa anglogold kwa gia ya wawekezaji, mji huo haufaidiki na chochote na rasilimali MUNGU aliyowajaalia. Anasema mji huo maji ni shida, barabara ni vumbi la kufa mtu.

Wanasubiri jamaa yetu aende huko nako na lap top tatu, bastola na bunduki kubwa, pete za fedha mbili na mabegi matatu ya nguo labda atawaokoa. Nawasilisha taarifa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom