Kwa kweli kama kuna tahariri za uhuru ambazo ziliwahi kunishangaza ni ya toleo la leo jumanne
Mhariri ametoa tahariri ndefu na kuhitimisha kwa madai kuwa mgombea wa CCM hakuwa chaguo la CHAMA na wana arumeru na kwamba ndiyo sababu wameambulia nafasi ya pili.
kama gazeti la chama linaandika haya,tambua wao jikononi mambo yanakwenda ndivyo siyvo
HALI ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Arumeru Mashariki, bado si swari baada ya mchakato wa kura za maoni kumpata mgombea wa chama hicho katika kinyang'anyiro cha ubunge kukamilika, Raia Mwema.
Ingawa mshindi katika kinyang'anyiro hicho amepatikana ambaye ni mtoto wa Mbunge aliyetangulia, marehemu Jeremiah Sumari, Sioi Sumari, wenzake wamelalamikia ushindi wake wakidai umetokana na matumizi ya fedha na si kukubalika kwake kisiasa wakionya kwamba, ameshinda ndani ya chama kwa nguvu ya fedha, lakini nje ya chama hicho, hali itakuwa ngumu kwake kushinda.
Katika hatua nyingine baadhi ya washindani wake wamedai kuwa hata kanuni za CCM hazijazingatiwa ambazo zinataka mshindi wa kura za maoni apate zaidi ya asilimia 50 ya kura zote lakini kwa upande wa Arumeru Mashariki, ameshinda kwa asilimia Kama mgombea huyo atapitishwa katika vikao vingine vya juu vya CCM ambavyo ni Kamati Kuu na Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho 34.91, ambayo ni sawa na kura 361 (34.91).
Kijana huyo wa marehemu Sumari ambaye pia kwa sasa ni Mkwe wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond, ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, alifuatiwa kwa idadi ya kura na William Sarakikya aliyepata kura 259 ambazo ni sawa na asilimia 25.
Wengine waliofuatia katika kinyang'anyiro hicho ndani ya CCM ni pamoja na Elirehema Kaaya aliyepata kura 205 sawa na asilimia 19.82; Elishilia Kaaya kura 176 sawa na asilimia 17.02, Antony Musani kura 22 sawa na asilimia 2.12 na Rashiankira Urio aliyeambulia kura 11 ambazo ni sawa na asilimia 1.06.
Kwa upande mwingine, wepesi wa kampeni za mgombea huyo wa CCM kama atapitishwa na vikao vya juu vya chama hicho utategemea zaidi na ushirikiano kutoka kwa washindani wake hao kwenye kinyang'anyiro hicho ambao baadhi wamesikika wakisema mwenzao huyo alitumia fedha kupata ushindi huo.
Uchaguzi wa Arumeru Mashariki utarajiwa kufanyika mapema Aprili, kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Jeremiah Sumari, ambaye alifariki dunia kutokana na maradhi ya saratani yaliyokuwa yakimsumbua.
Wakati wa awamu ya kwanza ya ubunge wake, Sumari alipata kushika wadhifa wa Naibu Waziri hadi Serikali ya awali chini ya Waziri Mkuu, Lowassa, ilipovunjwa mwaka 2008 na kuundwa nyingine chini ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Mkuu FJM hiki ni kituko cha mwaka. Sioi alipitishwa kwa kufuata taratibu zote za chama cha CCM,sasa gazeti la chama linapotoka na madai kama haya linataka kumhadaa nani? Hii ndiyo shida ya wana CCM kuiona nchi yetu ni yao tu. Na wao ndiyo wenye akili ya kufanya jambo lolote kwa nchi hii! Ndiyo maana wenye akili tumeishabaini kwamba CCM haitoachia madaraka kwa njia za kidemokrasia kwasababu haijui kushindwa ktk uchaguzi,itaondoka kwa nguvu ya umma!Wanasheria watusaidie, Sio anaweza kulishitaki gazeti za Uhuru kwa deformation?
Kama kuna kutokubaliana kati ya wajumbe wa CCM hilo ni tatizo la ndani lakini kwenye official level CC ya CCM ilimptisha Sioi. Sasa kwa mhariri wa UHURU kuharamisha maamuzi ya CC ambayo mwenyekiti wake ni Kikwete ni kituko. Hivi kama Sioi angeshinda Uhuru wangesema hakuwa chaguo la CCM?
Minyukano ya CCM inatia kinyaa!
Kikao halali cha chama kinatoa chaguo la chama, tena chini ya mwenyekiti wa chama. Wacheni kudhalilishana, Sababu sio mgombea, ila ni chama kupoteza mvuto kwa wananchi. Msitafute kondoo wa sadaka.