Gazeti Raia Mwema nalo mfukoni?

Mkitaka kujua kinachoendelea hapo someni makala ya mwandishi habari mkuu Bw Dillunga katika toleo la leo ukurasa wa 17 alafu mtajua mwigulu kishatia mguu ndani yake!!...
 
Ule uhariri wa mlengo wa kushoto ni staili ya Jenerali Ulimwengu na zaidi ya miezi 3 sasa hayupo Bongo, inasemekana alipata kibarua Bondeni. Hayo unayoyaona sasa ni wale wahariri wenzake ambao karibu wote ni 'bendera fuata upepo'
 
Afadhali mmeliweka hili hadaharani ,wanasikitisha sana ila kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho
 
Facts ni sturbon things. Wanachosema raia mwema ndicho tulichokisema baadhi yetu pale mwanzoni mkatuona labda tuna chuki binafsi!. Nawaombeni sana msinielewe vibaya au labda na mimi pia nimenunuliwa, Watu wa Igunga ni watu wa ajabu sana!. Kwanza wanaishi kwenye lindi la umasikini ulio topea uliosababishwa na CCM lakini subirini matokeo ndio mtajua kuna makabila fulani ya kuwaaminia kwa misimamo na kuna makabila bendera fuata upepo, hebu subirini matokeo ndipo mtalielewa hili!.
 
Ndugu wadau nimepata kusoma gazeti la Raia Mwema toleo la Jana http://www.raiamwema.co.tz/ na kuona jinsi gani Makala zake nyingi ikiwemo maoni ya Mhariri yalivyofuata ule Mpango wa Nape.Watu wa Igunga wanashida na matatizo mengi ambayo kwa miaka 50 ya CCM hayakupatiwa ufumbuzi..,suala la DC si hoja kwa sasa..,hoja ni kwa namna gani wana IGUNGA wanaweza kutumia uchaguzi huu kujiletea ukombozi.
Kutokana na hili sasa..,nadiliki kusema RAIA MWEMA limenasa katika ule mtego wa fedha zilizoandaliwa na CCM kwa ajili ya kuwakirimu wanahabari kwa sababu hiyo sasa..,sioni sababu ya kuendelea kuliamini tena gazeti hili.Tusubiri kuona zaidi kutoka RAIA MWEMA.
Nawasilisha.
 
Gazeti hili lilipokuwa linakandia CCM lilikuwa halijanunuliwa. Sasa linaposema ukweli kuhusu CDM...limenunuliwa. ULIMBUKENI HUU!

Mashabiki wa cdm watakomaa lini na kuachana na uvivu wa kufikiri unaowafanya watoe mawazo ya kipuuzi kama hii pumba iliyomwagwa hapa?

nepi hujambo?
 
Yaani we jamaa huna hata chembe ya utu. Kwako wewe habari ya ukweli ni ile inayosifia magwanda lakini nyigine zote ni za uongo. Basi endelea kusoma Tz daima kama unataka aina hiyo ya habari.

habari za asubuhi mwita25
 
kwa tunaofuatilia hili gazeti at first asili yake ni RAI,kabla pacha RA hajanunua kampuni ya New Habari Cooperation,labda historia inataka kujirudia!ila pia tukumbuke hawa jamaa huwa wanaandika vitu baada ya utafiti makini na vingi walivyoandika na kutabiri vingi vimetimia na kudhibitika ni kweli hata kama baada ya miaka!
mashabiki wa cdm msitake daima kuona hbr zinazo wafurahisha hata hbr mbaya mzichukue positively na kuona how thngs can be changed
 
Kwahiyo wewe wataka gazeti liwasifie CDM ndio utaamini kuwa linaandika habari za kweli? CDM hatoki igunga huo ndio ukweli.

Ndo matatizo ya kuzoea kupendelewa. Jamaa wanadhan kila wanachofanya kinastahili kusifiwa na wakipondwa tu wanakuja juu. Usikute wanaandaa tukio la uhalifu dhidi ya Gazeti hili.
 
Utafiti wangu umejionyesha dhahiri baada ya hekaheka za kampeni za Igunga kuanza.Gazeti hili likiripoti habari ya Igunga limekuwa likionyesha waziwazi kwamba CCM itashinda. Tafuta nakala ya wiki iliyopita.

Gazeti la leo limetoa taarifa kwamba Chadema na CUF watashindwa kwa sababu watagawana kura za upinzani,na habari hii imewekwa ukurasa wa mbele kwa makusudi na naamini imepangwa.

Sasa nikajiuliza kwanini gazeti hili liseme eti CUF na Chadema watagawana kura? Ina maana kura za kugawanyika ni za CUF na Chadema tu?


Ningependa kuwashauri wahariri wa gazeti hili watambue kwamba imani kubwa wananchi waliyokuwa wanaonyesha kwa gazeti hili inaanza kufifia na hakika mimi ni miongoni mwa watu watakaokuwa wanafikiri mara mbilimbili wakati wa kununua gazeti hili.

Nawasilisha.

Ya nini kulalamika wakati mna gazeti lenu la TZ Daima?
 
Raia Mwema limesema kweli CDM watagawana kura na CUF, huo ndio ukweli si mmeona Magamba juzi kwenye gazeti wanaorodhesha wapiga kura wao ili wajue idadi yao ukijumlisha na za kuchakachua waona watashinda.
Gazeti la Raia Mwema bado nalikubali kuna watu makini kama Johnson Mwambo, Jenerali Ulimwengu
 
Bado nakuamini sana mheshimiwa Kyoma Ulimwengu waweza kurekebisha upepo huo mbaya sana. Je Igunga ikiisha uatauza tena gazeti au kuna kitu kidogo umepewa kama tender hivi?
 
Afadhali mmeliweka hili hadaharani ,wanasikitisha sana ila kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho
Mimi mtizamo wangu uko tofauti kidogo. Kwenye gazeti hilo hilo kuna makala za kina zinazoelezea upande wa pili wa shilingi, makala ya Raimwema na ile ya lula wa Nzela ni mfano.

Raia mwema ina watu makini sana kwenye tasnia ya habari hapa Bongo na wasio na njaa ya sifa hata kidogo. Inawezekana wamefanya utafiti na kutokana na facts fulani fulani ndiyo wakafikia hitimisho la habari zao. kama tunapingana nao dawa si kuwashutumu bali ni kuleta data za ukweli kuthibisha kwamba wao ni "waongo".

Si wao si sisi tunaojua siku ya kupiga kura nani atampigia mgombea fulani kura. kuna kijiji fulani mgombea wa CDM alipata 25% ya kura wakati kwenye kijiji hichohicho DR.Slaa alilamba 80% ya kura. Wapiga kura walewale mitizamo tofauti kwa wagombea toka chama kimoja.

Ushabiki hausaidii sana bali uzowefu ndiyo kila kitu. Ni wangapi humu ndani watapiga kura siku ya tarehe 2/09/2011 huko Igunga?
 
Siku nyingi lilishakuwa toilet paper! Kwishineeeeee, walipewa matangazo kpndi cha bunge. Poleni bado mnasoma toilet p.
 
nimekuwa muumini mkubwa wa gazeti la raia mwema kutokana na ukweli kwamba ni moja ya magazeti yanayoandika habari kwa weledi mkubwa.

Waandishi wa gazeti hili nimekuwa nikiwaona ni miongoni mwa waandishi wenye weledi mkubwa na wasioyumbishwa. Hata waandishi wa kujitegemea wanaotuma taarifa kwenye gazeti hili ni wa kutiliwa mfano.

Nimeanza kuwa na mashaka baada ya kufanya tathmini kwa muda wa miezi kama mitatu hivi kama bado baadhi ya waandishi wa gazeti hili wanatilia maanani kiapo chao cha uandishi.

Nakumbuka katibu wa itikadi na uenezi wa ccm, nape nnauye alitembelea vyombo karibu vyote vya habari na gazeti raia mwema likiwa mojawapo. Tangu wakati huo nimekuwa siridhishwi na habari zinazoongoza kwenye gazeti hilo ukurasa wa mbele. Ni habari ambazo ni tofauti sana na zilivyokuwa zinaripotiwa mwanzo.

Wadau mtanisaidia lakini mwenye kufanya tathmini alinganishe habari zinazoongoza ukurasa wa mbele kwa muda niliotaja na jinsi ilivyokuwa inaripotiwa kabla.

utafiti wangu umejionyesha dhahiri baada ya hekaheka za kampeni za igunga kuanza.gazeti hili likiripoti habari ya igunga limekuwa likionyesha waziwazi kwamba ccm itashinda. Tafuta nakala ya wiki iliyopita.

Gazeti la leo limetoa taarifa kwamba chadema na cuf watashindwa kwa sababu watagawana kura za upinzani,na habari hii imewekwa ukurasa wa mbele kwa makusudi na naamini imepangwa.

Sasa nikajiuliza kwanini gazeti hili liseme eti cuf na chadema watagawana kura? Ina maana kura za kugawanyika ni za cuf na chadema tu?


ningependa kuwashauri wahariri wa gazeti hili watambue kwamba imani kubwa wananchi waliyokuwa wanaonyesha kwa gazeti hili inaanza kufifia na hakika mimi ni miongoni mwa watu watakaokuwa wanafikiri mara mbilimbili wakati wa kununua gazeti hili.

Nawasilisha.

magazeti yataandika kila kitu kwa sasa mwisho wa siku ni tarehe 2 oktoba. Baadaya ya hapo utajua ni gazeti lipi lilikuwa linaandika habari zake kwa umakini. Kama kura zitagawanyika ua la tutajua baada ya wapiga kura wa igunga kutimiza haki yao ya kupiga kura.
 
Tena km toleo la leo trh 21-Sept, habari km ya WASTAAFU KUWAKABILI SLAA, LIPUMBA..... nahisi Philip Mangula ndo kaiandika halafu Raia Mwema wakaitoa..... Vichwa vilivyobaki labda ni Msomaji Raia na Johnson Mbwambo? Kulikoni Jenerali siku hz, haonekani? No wonder karibu matangazo yote ya serikali wanayapata wao...........
Mimi naamini gazeti la Raia Mwema liko huru kuandika habari yoyote ile wanayoona inafaa kwa kipindi fulani ili mradi haivunji maadiri ya uandishi wa habari. Matharani ukisoma kwa makini maudhui yaliyomo kwenye habari ya "WASTAAFU KUWAKABILI SLAA, LIPUMBA...."habari hii ni nzuri sana kwa ajili ya mikakati ya ushindi kwa CDM. Tuwe tayari kusoma hata yale tusiyoyapenda ili kujua wale waliyoyaandika wana mawazo gani kuhusu suala hili ili kupanga mikakati ya uhakika
 
.Gazeti la leo limetoa taarifa kwamba Chadema na CUF watashindwa kwa sababu watagawana kura za upinzani,na habari hii imewekwa ukurasa wa mbele kwa makusudi na naamini imepangwa.Sasa nikajiuliza kwanini gazeti hili liseme eti CUF na Chadema watagawana kura? Ina maana kura za kugawanyika ni za CUF na Chadema tu?[/B].
Analysis ya Raia mwema ilikuwa correct, but sadly wrong conclusion. The correct conclusion ilitakiwa iwe hivyo, CCM Igunga watashindwa kwasababu wamesimamisha vyama viwili CCM A na CCM B, hivyo wa-CCM watagawanya kura zao kati ya CCM A na CCM B, na kuipa ushindi mwepesi CDM.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom