Gazeti RAI lailipua CCM kuhusu njama dhidi ya CHADEMA.

ukifikiri kwa kina utagundua hili gazeti la ccm linataka kukuza mgogoro,read between the lines you will realize this

Ni kweli mzeehili ni kazeti la Rostamu hapo zamani lilikuwa linaandika mabo ya ccm kwa kuona limekosa soko lina mdaa sasa limebadilisha jinsi ya kuandika habari na kujifanya rafiki wa Tanzania la hasha hili gazeti ni nyoka aliyejificha ndani ya gunia tuwenalo makini kabisa wadishi wake ni wasomi haswa na wanajua wanachokifanya.
 
Rai lazima waangalie upepo wa kibiashara, hawawezi kuwa pro-magamba wakati wenzao wapo against.
 
Watachemka,CHADEMA ni zawadi yetu sisi wanyonge toka kwa Mungu,na mwanzo wa CCM kuchemka mpango wao ni kama hivyo unaanza kugundulika.mungu ibariki Chadema
 
Gazeti la RAI linalomilikiwa na Habari Cooperation limefichua njama kubwa zilizoandaliwa na Chama cha Mapinduzi dhidi ya Chama kikuu cha upinzani Tanzania CDM.Gazeti hilo toleo la leo alhamisi limedai mkakati huo kabambe uliosukwa kwa muda mrefu na kwa ustadi mkubwa tayari umeiva na hatua ya kwanza imeanza kwa kuwatumia baadhi ya makada walioko ndani ya CDM ambao ni mbunge wa Maswa Mashariki John Shibuda na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CDM-BAVICHA Bi Juliana Shonza.Gazeti hilo limezidi kudai kwamba mkakati wa CCM ni kuhakikisha inawatumia makada hao kuisambaratisha CDM.

RAI imetumwa kuongeza malumbano!, hakuna atakae shughulika na hili, CDM ni kuangalia mbele kwenye TARGET, kama SIMBA mawindoni.
 
ushauri wa bure, chadema leadership, achaneni na shibuda, endeleeni na mkakati wa kuimarisha chama kwa lengo la kushika dola 2015, shibuda atajifia mwenyewe kwenye kura maoni, utakapofika wakati tarajali, hata hao bavicha, wasiangaike na shibuda ambaye kwa sasa amepoteza muelekeo hata kwa wapiga kura wake, tusonge mbele kuwakomboa watanzania, wenye kuwa na matumaini makubwa na nyie, acheni cheap politics kwa sasa, hazina nafasi kwa wakati huu. let us go to solve problems facing our nation.
 
Serikali yoyote ONEVU kwa Raia wake Mungu anainyima maarifa na mwisho wake itakufa na hivyo ndivyo CCM inakoelekea.
 
Hilo si tishio kwa ustawi wa chama chaguo la watu kwa sasa who is SHIBUDA na huyo dada?? Ni wachumia tumbo tu. CCM kama wana nia ya kweli kuisambaratisha CDM wadeal na mfumuko wa bei, mafisadi wote wafikishwe mahakamani (EPA, RICHMOND etc), waeleze wananchi utata unaozunguka kwenye mikataba yote michafu iliyoingia, wawapatie wananchi ahadi yao ya maisha bora kwa kila mtu........ yaani hata juwezi kuyataja yote. Hapo kidogo ndo wataweza kuisambaratisha NGUVU YA UMA.

Samahani wana CDM wenzangu kwa kuwaambia maadui zetu siri hiiii
 
Ku-deal na Shibuda ni rahisi sana, viongozi wa CHADEMA hawatakiwi kuumiza kichwa. Dawa yake ni kum-ignore.

Viongozi wa CHADEMA wakianza kujibizana na Shibuda atawatoa kwenye hoja za msingi na hivyo kupoteza focus ya 2015.

Hizo ndio gharama za zoa zoa, maana wakati mwingine unaweza kuzoa hata nyoka ukidhani umenasa samaki!

I second your submissions
 
haitawezekana, hata kama CDM walikuwa wanabeep umma, nao itakula kwao maana umma umeshawapa imani iliyokuwa nayo ccm miaka mingi. Irrevesrible process.
 
Gazeti la RAI linalomilikiwa na Habari Cooperation limefichua njama kubwa zilizoandaliwa na Chama cha Mapinduzi dhidi ya Chama kikuu cha upinzani Tanzania CDM.Gazeti hilo toleo la leo alhamisi limedai mkakati huo kabambe uliosukwa kwa muda mrefu na kwa ustadi mkubwa tayari umeiva na hatua ya kwanza imeanza kwa kuwatumia baadhi ya makada walioko ndani ya CDM ambao ni mbunge wa Maswa Mashariki John Shibuda na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CDM-BAVICHA Bi Juliana Shonza.Gazeti hilo limezidi kudai kwamba mkakati wa CCM ni kuhakikisha inawatumia makada hao kuisambaratisha CDM.

....Tumeisha waambia acheni kupokea hao watu hawasikii wanaendelea kujivunia vua gamba vaa gwanda,hata yule mallya wa arusha mtamjua baadae kuwa ni mamluki...
 
CCM inadhihirisha ni kiasi gani imezeeka na kwamba inashindwa ku-focus kwenye mambo ya msingi yanayolikabili taifa kwa sasa na kupeleka nguvu zake nyingi kuwaza na kujipanga namna ya kuendelea kutawala. Ni viongozi wenye mawazo MGANDO kama akina Nape na Wassira ndio ambao wanaona kuwa CHADEMA ni tatizo kwa ccm kuendelea kutawala nchi hii. Lakini kwa sisi ambao tunafahamu mambo yanavyokwenda, tunaamini kuwa tatizo kubwa na ambalo linaingusha sisiem, siyo Chadema, Ni ccm yenyewe kushindwa kutatua matatizo ya MSINGI ya wananchi kama, KUPAA KWA B

Watapanga mipango yote, lakini mwisho wa siku watashindwa kwa sababu kuibomoa CHADEMA, hakurudishi imani ya wananchi kwa CCM, ila kuongeza chuki dhidi ya viongozi wake. Kuiongea CHADEMA kila siku, ni kuingezea umaarufu na kuifanya izidi kupendwa zaidi. Hata mwalimu alisema, CCM HAIKUMZAA, na wala ccm haijamzaa Mtanzania yoyote yule...! Kama bado wanatumia mbinu za 1947 katika dhama hizi za sayansi na teknolojia, ni aibu.

Washauri na viongozi wakuu wa ccm wameishia, hawana maono tena, hawana dira wala mwelekeo kama chama chenyewe. Yaani akili zao zimezeeka kama chama chenyewe. Mwalimu aliwaambia, "wananchi wataendelea kuichagua ccm na mabaya yake, kama hakutakuwa na chama kingine cha upinzani ambacho kinaweza kutatua matatizo yao!!!" Sasa hivi kuna mbadala, kama ccm ina mpango wa kuua upinzani Tanzania, Watanzania tutakuwa tayari kuongozwa na jeshi, kuliko kuicha ccm madarakani kwa miaka mingine mitano, ni kifo chetu na vizazi vyetu.

Lakini, kikubwa na kizuri, ccm wamechoka kufikiri na akili zao zimedumaa, nashukuru kuwa tumeanza kuzifahamu mbinu zao mapema, hii ni katikati ya 2012, bado tuna miaka karibu mitatu na nusu kufika uchaguzi 2015, tunajipanga zaidi kukabiliana na mbinu zao, na tunazidi kutangaza sera zetu kwa wananchi hadi vijijini. Kasi hii ya elimu kwa umma ikiendelea hadi 2015, hakuna ubishi kuwa ccm haitashinda uchaguzi wowote ule ki halali, na ni imani yangu kuwa, hata polisi na wanajeshi watatuunga mkono, kwani ni askari wachache sana ambao wananufaika na uongozi wa ccm, wengi ni walalahoi tu kama waalimu, madaktari na watumishi wengine wa umma, tatizo ni kwamba wao hawawezi kugoma.

STK ONE,
TOGETHER WE CAN BRING THE CHANGES WE NEED.....YES WE CAN, GOD BLESS CDM!!!!
[/SIZE yanayofanywa yote na ccm kwa cdm ni kukikomaza chama
 
Ushauri wa Bure kwa Shibuda na Makamu mwenyekiti wa BAVICHA. Jitengeni na muunde chama chenu na au mrudi mlikotoka maana CDM haitikisiki kwa kauli zenu chafu. M4C ni wingu la moto limetanda kuteketeza mfumo uliodumaa kwa miaka 50. Hakuna wa kuuzima moto huu. Shibuda huwezi. Dawa yake ni kuondoka mwenyewe na utuachie na CDM yetu maana umetukuta na ndio bado mgeni. Mgeni nuksi wewe.
 
NAICHUKIA CDM LKN NAICHUKIA CCM ZAIDI.
bora cdm muingie madarakan ccm ife,ili 2020 2tafute chama chenye mvuto mzr wa kuingoza nchi
 
Back
Top Bottom