Gazeti Mzalendo: TRA yamwita DR. Slaa fisadi, halipi kodi

Sijaelewa hapa. Wana JF naomba mnieleweshe. Yaani hajalipa kodi tangia mwaka 1992, wakati yeye amejiunga na CHADEMA 1995, na amekuja kuwa katibu mkuu baadaye sana. Au wanamaanisha mshahara wake wa tangu November mwaka jana alipogombea urais? Lakini pia, hivi kati ya mwajiri na mwajiliwa, je ni nani anayetakiwa kubanwa kuhusu kama mwajiriwa analipa kodi au la? Kwa mfano, mimi huwa nakatwa kodi, lakini sijawahi kwenda TRA kubisha hodi ili nilipe kodi, huwa inakatwa automatically tu kabla hata mimi sijaugusa mshara wangu. Au wanamaanisha CHADEMA kama chama ndo hailipi kodi? Na kama ndio hilo wao TRA wanawajibikaje kwa kutokusanya kodi tangia mwaka 1992 kwene chama ambacho kina usajili na kinafanya kazi kila siku? Na je hali ikoje vyama vingine vya siasa?
PAYE inalipwa na mwajiri ila anakata kwenye mshahara wa mtumishi wake
Dr. mpaka mwaka karibu mwishoni mwa 2010 alikuwa mbunge kama hakalipa sio kosa lake ni kosa la utendaji mbovu wa Serikali
Mimi ninapiki piki yangu inafanyakazi ya boda boda mpaka mwishoni mwa Machi inabidi uwe umelipa mapato fail to do that Aprili piki piki itakamatwa utalipa TZS 65,000 ( 35,000 mapato, 20,000 fine na 10,000 gharama za kukushika) kwa ninin hawakufanya hinyo kwa CDM? waanze wao kuwajibishwa kabla ya CDM.
 
Wakubwa,
gazeti la leo la Magamba-Mzalendo, limeandika hyo habari!

Tena mshahara wa Dr. Slaa ni sh.1,700,000 na wamesema hauna kodi.

Wamesema chadema haijalipa kodi tangu 1992. Na wamedai walipe haraka sana pamoja na adhabu.

My take: TRA WALIKUWA WAPI hadi wakurupuke leo kutoa hyo taarfa? Majungu hayaish yaan hadi TRA yaingia katka siasa!

Jana Man Yuu hawakucheza mpira kabisa. Ingekuwa bongo, wangeweka mpira kwapani.

jamani mi napita tu
 
Wakubwa,
gazeti la leo la Magamba-Mzalendo, limeandika hyo habari!

Tena mshahara wa Dr. Slaa ni sh.1,700,000 na wamesema hauna kodi.

Wamesema chadema haijalipa kodi tangu 1992. Na wamedai walipe haraka sana pamoja na adhabu.

My take: TRA WALIKUWA WAPI hadi wakurupuke leo kutoa hyo taarfa? Majungu hayaish yaan hadi TRA yaingia katka siasa!

Tia Ra Ari (TRA) wafukuzwe wameshindwa kazi. Kodi gani toka 1992 wanastuka hivi sasa? Wasikurupuke, they should be sacked frm office, they are only pompous brats.
 
Sasa nani alaumiwe hapo? Au kazi ya TRA ni nini? Unapoongea hadharani unahitaji kutumia akili sana, yawezekana anayekusifu ni mkeo peke yake, wengine wote wanakudharau!!
Kama TRA imeshindwa kukusanya kodi toka 1992 basi hiyo ni kashfa kubwa kwa TRA sio kwa CDM!

Sio tu kashfa bali wameamua kujionesha ni jinsi gani hawatambui mamlaka yao kama baba yao mzee wa kaya, kiufupi wengi walio katika ofisi za umma hawajui wajibu wao ndomana ni vigumu kuendelea.

wamemtaja Dr. slaa kwa sababu ya kujipendekeza kwa mzee wa kaya, na bila shaka atafurahi kwa kuzani Dr. Slaa kachafuliwa kumbe kwa kiongozi mwenye akili angewafukuza wote ofisini maana hamna wanachofanya zaidi ya kupokea mishahara ya bure.
 
Sioni sababu ya kulipa kodi yoyote ile ktk utawala huu wa kuwazia vimshahara,pombe,sigara,mafuta!huku wakiachia magogo,samaki,wanyama pori,madini,vipusa wakifaidi wachina,wahindi na wazungu!
 
Sioni sababu ya kulipa kodi yoyote ile ktk utawala huu wa kuwazia vimshahara,pombe,sigara,mafuta!huku wakiachia magogo,samaki,wanyama pori,madini,vipusa wakifaidi wachina,wahindi na wazungu!
wakuu slaa lazima alipe kodi anayodaiwa kwa maendeleo ya taifa na si vinginevyo
 
Suala muhimu hapa ni Slaa na wakwepa kodi wenzake kulipa fasta pesa yetu waliyokuwa wakiiba.

Suala la muda kupita kabla hajagundulika si hoja, hata nchi zilizoendelea wakwepa kodi hugundulika baada ya miaka kibao kupita na kulazimishwa kulipa pamoja na faini au interest.

Wahalifu wakwepa kodi wana mbinu nyingi chafu za kuficha matendo yao maovu, ninaamini hata DR Slaa alifanya hivyo hivyo.

Maadam tumembaini, tuhakikishe analipa pesa yetu yote, tena haraka sana kabla hasira hazijapanda.

Pia achukuliwe hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa viongozi wanaofanana naye, wapuuzi wasiotaka kulipa kodi.

Wanaomtetea hawajui kuwa wanabariki hujuma kwa uchumi wetu, ni wasaliti na wanaorudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu.

Hatumtetei Dr Slaa hata kidogo wala CDM ila tunataka evidence na sio mambo ya siasa kwenye chombo kikubwa kama TRA.

Tumesikia tuhuma mara nyingi na hata kuwepo kwa ushahidi lakini TRA walinyamazia. Mfano wakati chama cha magamba walipoingiza magari aina ya toyota Landcruiser Hardtop na Mahendra yakalipiwa undervalue pamoja na taarifa kuvuja lakini TRA walijifanya viziwi mpaka leo hakuna kilichofanyika.
 
Hii nadhani si hoja hapa mzalendo na Jambo leo mnavalia njuga . Kama kuna hoja walete madai na wadaiwa watajibu . Slaa mshahara wake bado umekuwa ukijadiliwa hadi juzi .Leo TRA wanasema halipi kodi ? Haya ni maajabu sana lakini wajue kuna mwisho wa kila ujinga .
 
imefika wakati sasa TRA kuachaa kutumikia mafisadi wa ccm na kuacha kufanya siasa.Ni mabilioni mangapi yanayopotea kupitia makampuni ya simu na madini, huku tra wakila rushwa tuu?.tra wanadhalilisha watanzania kwa kuanza kufanya siasa badala ya jukumu lao la kimsingi.
 
kariakoo kule wahindi na risiti books mbili mbili.ukinunua mzigo wa 5Mil unapewa risiti ya elfu 20.nilienda na jamaa mmoja rafiki yangu anafanya tra shopping, wahindi wakawa wanamchangamkia kama vile rais wa nchi.anachukua bidhaa kama zake. Wizi mtupu.hakuna ofisa wa tra anaweza kumnyoshea kidole mtakatifu dr slaa.
 
Huyu Slaa PhD ya kanoni isiyoukuwa na digrii hata maja si ndio anajidai kutetea umma? Kumbe mwenyewe mbabaishaji halipi kodi? Looooo! Yatamshinda.

Hizo posho mnazolipwa kwa kushinda JF mnalipa kodi?:dance:
 
Upumbavu huu toka 1992 mpaka sasa hivi hao tra walikuwa wapi!? Waache siasa za kinafiki au kwa sababu dr.slaa aliwalipua? Waende wakamkamate kama wanaume kweli!
 
kariakoo kule wahindi na risiti books mbili mbili.ukinunua mzigo wa 5Mil unapewa risiti ya elfu 20.nilienda na jamaa mmoja rafiki yangu anafanya tra shopping, wahindi wakawa wanamchangamkia kama vile rais wa nchi.anachukua bidhaa kama zake. Wizi mtupu.hakuna ofisa wa tra anaweza kumnyoshea kidole mtakatifu dr slaa.

Wizi wa namna hiyo haukomeshwi na tra, unakomeshwa na wananchi wenyewe kujipa nidhamu sawia. Kwa hili la Slaa kutokulipa ushuru na chadema kutolipa ushuru toka 1992 ni uzembe wa tra wao ndo wanatakiwa kushughurikiwa kikamlifu.

mwajiri yoyote lazima afikishe ripoti ya kodi ya mwajiriwa sehemu husika kila mwezi, sasa wao sijui wanafanya je kazi
 
Kodi hizi tunalipa ndiyo askari wanalipwa mshahara wanaishia kuwaua walipa kodi kwa risasi za moto sasa sijui inakuwaje .
 
Inabidi Dr. Slaa na CHADEMA wajibu shutuma, na TRA nao wajibu shutuma za kwamba wanatumia hili suala kisiasa kwa kutueleza kigezo kipi kilitumika kumtaja Dr. Slaa kati ya wasiolipa kodi wote.

This country is a curse!

Nijuavyo mimi TRA workers are the highly paid people in this country na the most corrupt!

Nashindwa kuwaelewa TRA kwa kuanza kufuatilia mshahara wa Dr. Slaa wa Tshs.1,700,000/=ilhali kuna vigogo wa Serikali wenye mishahara minono zaidi kuliko Slaa na hawakatwi KODI.

Sheria ya Kodi inataka mapato yote yakatwe kodI, hii ni pamoja na mshahara,posho ya safari,nauli ya likizo, n.k.
  1. Tukianza na mawaziri na wabunge nataka TRA watuambie wanalipa kodi kiasi gani kutokana na mishahara yao na posho wanazolipwa wakiwa Bungeni na safari zingine za kikazi ndani na nje ya nchi?
  2. Pili TRA watuambie misamaha ya KODI(TAX HOLIDAYS) kwa wawekezaji wanaokuja nchini ni kiasi gani kimesamehewa tangu waanze ujinga huo wa misamaha ya KODI.
  3. Je,vigogo wa CCM wanalipa KODI ya mishahara yao na kwa kiasi gani? Je,CCM wanaponunua magari,mitambo ya Radio k.m.UHURU FM,wanalipa KODI?
  4. TRA watuambie na BILLIONS ngapi zinapotoe kutoka kwa haya Makampuni ya Wawekezaji yanayopewa misamaha ya KODI every other 5 years na baada ya 5 YEARS the same company changes its name in order to have another 5 years TAX holidays?
Haiingii akilini hata kidogo ATI MWEKEZAJI MWENYE MAMILIONI YA SHILLINGS AU DOLLARS ANAYEKUJA KUWEKEZA UNAMPA MSAMAHA WA KODI(TAX HOLIDAYS) KWA MIAKA 5 BILA KULIPA KODI KWA KISINGIZIO KUWA ANAKUWA HAPATI FAIDA LAKINI M-TZ anayepata mshahara kiduchu(Hand to Mouth) anakatwa KODI KILA MWEZI!!! This is NOT FARE AT ALL. It did no good to nobody.

Nawashauri TRA waachane na mshahara wa Dr. Slaa kwani utawatokea puani. Kinachoonekana hapa ni visasi vya TRA zidi ya Dr.Slaa simply because juzi aliwalipua kuwa WALIZUIA MAGARI YA MFANYA BIASHARA MMOJA HUKO ARUSHA NA KUIKOSESHA SERIKALI BILLIONS OF MONIE!
Dr.Slaa alikuwa mbunge wa Karatu kupitia CCM toka mwaka 1995 mpaka 2005, Je TRA wana maana gani kusema kuwa Chadema na Dr. Slaa hajawahi kulipa kodi tangu 1992?

TRA acheni kujiingiza kwenye SIASA, Kazi yenyu ni KUKUSANYA KODI,Full stop. Pambaf kabsa!
 
TRA msimwangalie doctor slaa peke yake,hayo makampuni yanayochimba madini mbona hamtuambii haya lipi kodi kiasi gani?kama wangelipa Tanzania isingekuwa nchi ya pili duniani kwa kutegemea misaada
 
'Serikari corrupt haikusanyi kodi, inabaki kufukuzana na ushuru mdogomdogo wa wamachinga', hayo ni maneno ya Julius Kambarage Nyerere,
Ndicho serikari yetu ya ccm na jk inafanya sasa.
 
'serikari corrupt haikusanyi kodi, inabaki kukimbizana na ushuru mdogomdogo wa wamachinga mabarabarani'. hayo ni maneno ya Julius Kambarage Nyerere.Sasa serikari yetu inayoongozwa na ccm na jk ndicho wanachofanya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom