Gazeti la Uhuru Vipi Tena?

Mutua i think this post is irrelevant. Labda kama ungekua na swali dogo kama hili ungem PM mmojawetu tungekujibu.
Hamna ubaya wowote..ama wee unaonaje? maana kama ni wananchi kuchoswa na mabomu i dont think that stands. Labda useme wanawatishia wananchi ili waichague Chi Chi Em hapo maybe..
 
Dilunga,

Unajuaje kama wana ridhaa ya mgonjwa na mgonjwa anataka kuonekana hivyo...

Ninajuaje kama wana ridhaa ya mgonjwa? Sijui kama wana ridhaa ya mgonjwa, na sijasema najua.

Nasema, hii kawaida ya kupiga piga picha wagonjwa wamegalagala sakafuni na nusu khanga ni udhalilishaji na uvunjwaji wa maadili ya usitiri wa nyeti za mgonjwa unless wana idhini.
 
Labda huyumwanajamii anashangaa kuona Gazeti la uhuru limekuwa wazi hawamu hii kuliko siku zote kwani siku zingine ilikuwa haionyeshi matukio makubwa ,hasa ajali iliyotokana na uzembe wa serikali.Mimi nimemuelewa kwamba kwa kawaida hao jamaa hawapendi kuripoti ukweli wa mambo badala ya wanafichaficha.
 
hata mimi nimeshangaa leo. Nimepita kwenye mbao za wauza magazeti mipicha kibaaao sijui hata mantiki yake nini. Wangeweka picha hata za Makamba akiwa busanda

Gazeti hili limetoa picha za majeruhi wa mabomu Mbagala ukurasa wa mbele wakiwa wamelazwa chini wawili wawili kwenye godoro moja.

Binafsi sijafurahishwa na picha hizo likiwa ni gazeti la chama tawala lisingeonyesha picha hizo.

Wengine mnasemaje?

Siyo kwamba ukweli ufichwe kwani nani hajui kuwa watu wengi wamedhurika, na si lazima utangazie watu wote hata wapita njia , zingewekwa basi hata ndani siyo front page!!!!!!!!

Mimi wa kwanza nilikuwa sijui mpaka niliposoma kwenye gazeti la UHURU, SIONI TATIZO LOLOTE HAPO, mambo ya kuficha ficha mtaficha na visivyofichika.......
 
Siyo kwamba ukweli ufichwe kwani nani hajui kuwa watu wengi wamedhurika, na si lazima utangazie watu wote hata wapita njia , zingewekwa basi hata ndani siyo front page!!!!!!!!



Nahisi tatizo lako ni kutofahamu maana ya chombo cha habari !!!!
 
Back
Top Bottom