Gazeti la The East African laomba radhi kwa Rais Kikwete, wakiri Katuni haikufaa kutumika

msemakweli

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
1,627
880
attachment.php

we don't joke!
 

Attachments

  • catoon.v05.jpg
    catoon.v05.jpg
    34.6 KB · Views: 13,918
Watu wa magazeti walivyo wahuni, huniacha mdomo wazi. Wanaboronga na kumuandika mtu kwa MAANDISHI MAKUUUUBWA SANA, halafu wakikosea wanaomba radhi kwa viji-maandishi vidogoooooo halafu katikati ya gazeti kurasa za ndani kabisa. Huu ni unafiki wa hali ya juu sana. Cc Pasco
 
Last edited by a moderator:
..i dont have a problem with that cartoon.

..i have a problem na miaka kadhaa ya makala za kuilaumu, kuichonganisha, na kuipakazia Tz.

..hapa nazungumzia makala zinazotoka rwanda new times na kuishia kwenye the East African.

..tatizo lingine ni kwamba waandishi wetu wa ikulu na wizara ya mambo ya nje hawajishughulishi kujibu upotoshaji huo.

cc Pasco, Manyerere Jackton, jMali, msemakweli, Kobello
 
Last edited by a moderator:
..i dont have a problem with that cartoon.

..i have a problem na miaka kadhaa ya makala za kuilaumu, kuichonganisha, na kuipakazia Tz.

..hapa nazungumzia makala zinazotoka rwanda new times na kuishia kwenye the East African.

..tatizo lingine ni kwamba waandishi wetu wa ikulu na wizara ya mambo ya nje hawajishughulishi kujibu upotoshaji huo.

cc Pasco, Manyerere Jackton, jMali, msemakweli, Kobello
Mkuu Joka Kuu,

  1. Kwanza nakubaliana na wewe kuhusu cartoon, haina problem kabisa, cartoon za namna hiyo ziko duniani kote na marais karibu wote wanafanywa caricature from time to time, ila most of the times ni wachoraji caricature wa nchi husika, wakitumia magazeti ya nchi husika, sasa inapotokea ni nchoraji wa nchi jirani amemchora rais wa nchi jirani, ndipo assence ya matukano inapoibuka, ila in the spirit of regional block, gazeti la The East African ni regional paper, hivyo liko right kumchora rais wa nchi yoyote, na ikawa kama ni rais wa ndani!, sasakwa vile wahusika ni Wakenya!, then its seems as a bigger problem. Ndipo serikali yatu ikaamua kulipiga marufuku, kwa sababu japo original layout na page making inafanyikia Nairobi, actual printing inafanyikia Dar es Salaam, kama The Herald Tribune liko produced in Paris, likini liko printes in Paris, London na New York at the same time, na hawa ndio wamiliki wa The New York Times, kama The Nation walivyo wamiliki wa Citizen Mwananchi, hivyo serikali haikujali kwa siku zote kuwa wana print nchini bila usajili, hivyo sasa itawabidi wa printie Nairobi na kuleta magazeti yao humu physically.
  2. Ni kweli wana makala nyingi za kuilaumu, kuichonganisha na kuipakazia Tanzania, hicho ni kitu cha kawaida kwa magazeti ya nchi fulani yana take side na nchi yao kwenye some of the issues, mfano Kenya, Uganda na Rwanda walipounda "the coalition of the willing" na kuiside line Tanzania. Huu ndio unaitwa nationalism na patriotism to ones nationalistic interests.
  3. Hili la waandishi wetu na Ikulu, hawajishughulishi katika kupotosha hayo, pia nakubaliana na wewe kiasi, ila pia pia naunga mkono kiasi, uwongo ukiachwa kurudiwa rudiwa bila kukanushwa hugeuka kuwa ndio ukweli, ila kuna uongo wa kitoto na kijinga kabisa, ukiandikwa kwa kiingereza, ni bora uoachwe hivyo hivyo kwa kuwa ignored na kuishia kusomwa na wale wachache tuu, wanaojua Kiingereza, kuukanusa ndio kuutangaza zaidi!. Amini nakuambia, wengi wameitafuta cartoon ile baada ya East Africa kufungiwa!.
  4. Ila pia lazima tukiri wazi udhaifu wetu sisi kama Watanzania, hatuna waandishi wenye uwezo na level ya kukanusha baadhi ya mada za The East African!, nasikitika kukujulisha Ikulu yetu, hawana uwezo huo, wala MFA!. Kwa maoni yangu, nadhani kazi kubwa ya ile diroctorate ya mawasiliano Ikulu ni kutoa tuu press release kesho rais atafanya nini, na kama ni safari za nje, kurejea kutupa feed back rais amefanya nini na amelkutana na nani!, sina kumbukumbu ni lini wanahabari wa ikulu wanajitokeza kukanusa concrete things!.
  5. Mfano rais wetu "aliposingiziwa kuhongwa suti", ikulu yetu ilinyamaza kimya kabisa as if nothing happened!. Lakini JF iliporusha humu kuwa "rais wetu kahongwa suti!", ndipo ikulu ikaamka kukanusha, ila kilichokuwa kinakanushwa sio tuhuma za source, bali tuhuma za jf!. Kwa kanusho lile, wenye akili zao walishabaini ni kwa nini Ikulu haikukanusha the source!.
  6. Sasa tupaoelekea kwenye mtangamano wa Africa Mashariki, (EA Regional Integration), ili tunafania na kwenda sambamba na wenzetu, lazima sisi pia tuwe na vibrant media!, mpaka hii leo, sio tuu Watanzania knows very little kuhusu opportunities za EA, but our media people hawajui, our media houses have no capacity hivyo kujikuta we deprive our people with very vital informations wakati media za wenzetu ni driving force kwa watu wao kuchangamkia fursa za mtangamano!.
Japo tumetoka mbali, we still have a long way to go, vinginevyo tutaendelea kuburuzwa with mis information, and lack of information.

Pasco
 
Kumchora JK ilikuwa ji hitimisho tu. Lakini makala za gazeti hili zilikuwa bias sana. Na zilikuwa na negative impact kwa TZ kama nchi nw kama mwanachama wa EA. Hakuna kulifungulia.
 
Tukubali tu challenge katika utoaji habari. Tusifurahie kuambiwa mazuri tu hata mabaya nayo ni kwaajili ya kujirekebisha...
 
Hawa jama wakafie mbali na gazeti lao. mimi sitaki hata kuliona. Aisee binafsi sinaga imani kabisa na watu wa kenya, nilishawahi kutembea kenya kama mara tatu hivi. Aisee hawaaminiki hata kidogo. Kifupi roho zao zina sura mbili
 
Hawa jama wakafie mbali na gazeti lao. mimi sitaki hata kuliona. Aisee binafsi sinaga imani kabisa na watu wa kenya, nilishawahi kutembea kenya kama mara tatu hivi. Aisee hawaaminiki hata kidogo. Kifupi roho zao zina sura mbili
A good kenyan is a dead one!
 
Haya! Wale waliokuwa wanaipondea serikali kwa kuwafungia hawa, waje tena kuwatetea.
 
Mkuu Joka Kuu,
  1. Ni kweli wana makala nyingi za kuilaumu, kuichonganisha na kuipakazia Tanzania, hicho ni kitu cha kawaida kwa magazeti ya nchi fulani yana take side na nchi yao kwenye some of the issues, mfano Kenya, Uganda na Rwanda walipounda "the coalition of the willing" na kuiside line Tanzania. Huu ndio unaitwa nationalism na patriotism to ones nationalistic interests.
  2. Hili la waandishi wetu na Ikulu, hawajishughulishi katika kupotosha hayo, pia nakubaliana na wewe kiasi, ila pia pia naunga mkono kiasi, uwongo ukiachwa kurudiwa rudiwa bila kukanushwa hugeuka kuwa ndio ukweli, ila kuna uongo wa kitoto na kijinga kabisa, ukiandikwa kwa kiingereza, ni bora uoachwe hivyo hivyo kwa kuwa ignored na kuishia kusomwa na wale wachache tuu, wanaojua Kiingereza, kuukanusa ndio kuutangaza zaidi!. Amini nakuambia, wengi wameitafuta cartoon ile baada ya East Africa kufungiwa!.
  3. Ila pia lazima tukiri wazi udhaifu wetu sisi kama Watanzania, hatuna waandishi wenye uwezo na level ya kukanusha baadhi ya mada za The East African!, nasikitika kukujulisha Ikulu yetu, hawana uwezo huo, wala MFA!. Kwa maoni yangu, nadhani kazi kubwa ya ile diroctorate ya mawasiliano Ikulu ni kutoa tuu press release kesho rais atafanya nini, na kama ni safari za nje, kurejea kutupa feed back rais amefanya nini na amelkutana na nani!, sina kumbukumbu ni lini wanahabari wa ikulu wanajitokeza kukanusa concrete things!.
Pasco,

..kila wizara ina Afisa Habari.

..kwa hiyo hata kama waandishi wa habari wa Tz hawawezi kwenda "pound-for-pound" na waandishi wa the East African bado naamini maafisa wa habari walioko Foreign, Wizara ya Afrika Mashariki, na Wizara ya Utalii, mmoja mmoja au kwa pamoja wanaweza kupangua propaganda za the East African Magazine.

..tatizo letu ni kwamba tuna-react pale anaposhambuliwa Raisi tu. Ikishambuliwa nchi na wa-Tz wahusika wanakaa kimya.

..the East African has done a lot of damage kwa Tanzania. Imewaathiri wasomaji wake wa Uganda na Kenya kiasi kwamba wanaamini kwamba Tanzania haina mchango wowote ule ktk EAC.

cc Mwawado, Kichuguu, Jasusi, Nguruvi3, Kibona, EMT, jMali, Tetty
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom