Gazeti la The East African: Katuni ya Kejeli kwa Tanzania, Olympic

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Mnakumbuka ile katuni iliyokuwa imechapwa kwenye gazeti la Kenya ikonesha wana habari wa Tanzania wakilamba viatu vya JK. Ililalamikiwa sana ingawa ilikuwa na ukweli fulani. Sasa imewekwa katuni kwenye gazeti la The East African kama ilivyo hapa chini. Sijui tena tukasirike au tukubali ukweli?
 
Attachments

  • Kenya catton of tanzania.JPG
    Kenya catton of tanzania.JPG
    416.6 KB · Views: 6,055
Hii hata JK itamchekesha. This time watapewa zawadi wachoraji wa katuni hii kwa kuitangaza vizuri Tz.
 
Katuni hii nimeipenda kwa vile inasema ukweli. Kuanzia viongozi hadi wana michezo wa kitanzania wamekuwa wakienda nje kutalii na kufanya ufuska. Hili si tusi wala kejeli. Katuni hii inafurahisha na kufundisha kwa sababu mchoraji hakuwa na haja ya kupindisha ukweli. Kwa watu wenye akili timamu na wanaofikiri sawa sawa hii katuni ilitosha kuwa suto na somo. Ila kwa walio wengi wanaopenda kusifiwa hata upuuzi ni maudhi.
 
Yaaani kwa maneno mdomo wa TZ umejaa medali!!!

Hivi nani alimpa madaraka Bayi??? Ana akili timamu mtu huyu?

Pia tuwaelewe wakenya kwamba siyo washirika wetu. ni wapinzani na washindani wetu. Tz hatujawachora kwa upuuzi wao wa kuingia Somalia kwa sababu ya wazungu wawili tu waliotekwa nyara. sasa hivi wanalizwa kila kona ya Nairobi.
 
Mkuu.. Huyo mchoraji katuni ni Mtanzania.. Na hayo anayoyachora ni mawazo yake na wala ci ya wakenya.. Ni sawa na kipanya anavyoweka hicia na mawazo yake kwenye katuni zake.. Muhimu ni ujumbe uliobebwa..

Sent from Tora Bora..
 
Kwani hatuwezi hata kupiga blah blah hadi Olympic wakaamua kuweka mchezo wa blah blah kwenye orodha ya michezo yake? Na kama ikiwekwa, tutashinda?
 
Mnakumbuka ile katuni iliyokuwa imechapwa kwenye gazeti la Kenya ikonesha wana habari wa Tanzania wakilamba viatu vya JK. Ililalamikiwa sana ingawa ilikuwa na ukweli fulani. Sasa imewekwa katuni kwenye gazeti la The East African kama ilivyo hapa chini. Sijui tena tukasirike au tukubali ukweli?

Ukweli ni ukweli; japo unaumma! Kwa kuwa tunatia aibu hawa wachoraji vibonzo wacha watuchane vizuri tuu!

Japo kwa uzoefu wetu wa kuboronga, naona hata kutaniwa, kushutumiwa na kushauriwa hakusaidii! Heri tuanze kutishia viongozi wa michezo kwa kichapo wakishindwa kutimiza malengo yao!
 
Yaaani kwa maneno mdomo wa TZ umejaa medali!!!

Hivi nani alimpa madaraka Bayi??? Ana akili timamu mtu huyu?

Pia tuwaelewe wakenya kwamba siyo washirika wetu. ni wapinzani na washindani wetu. Tz hatujawachora kwa upuuzi wao wa kuingia Somalia kwa sababu ya wazungu wawili tu waliotekwa nyara. sasa hivi wanalizwa kila kona ya Nairobi.

Mkuu hicho kibonzo kinatuonyesha tulivyo watu wa maneno mengi. Timu yetu ya Olimpiki imetia aibu kulinganisha na majirani zetu. Kuhusu Kenya kupigana vita Somalia,siku zote nasema Kenya walichelewa sana. Matatizo ya utekaji meli ktk bahari ya Hindi na maelfu ya vijana wanaokimbilia Afrika Kusini kupita hapa,kote huko ni kushindwa kuwajibika kwa majirani wa Somalia. Hata kujazana Wasomali hapa ambao wameanza kulalamikiwa na wazawa ktk miji ya Arusha na Dsm ni kwasababu majirani tulishindwa timiza wajibu!
 
Back
Top Bottom