Gazeti la Sauti Huru: CHADEMA Asili mbioni kusajiliwa!

Itoshe kusema mfa maji haachi kutapatapa, kwani huo ndo muendelezo wa mwisho wa magamba
 
Linamilikiwa na Subash Patel pale MM Integrated, Kijitonyama. Subash wa kashfa ya Chavda, rafiki na Jeetu Patel wa EPA. Jamaa anazo kwelikweli. Alitajwa na Mzee Mengi kuwa kati ya mapapa wa ufisadi.

Ni yule aliyeshirikiana na Lowassa wakauziana jengo la Umoja wa Vijana wa magamba Nape hakuona ngawira zilipitia wapi, ndo akaanza fujo UV magamba mpaka akakosana na rafiki wa marehemu baba yake Mzee Makamba! Kumbukeni msiba wa marehemu mzee Moses Nnauye ulikuwa kwa Makamba jijini.

Ndiye mwenye maghorofa yale mawili pale UV Magamba. Ana kampuni inaitwa Estim inapata tenda nyingi sana serikalini. Inamjengea nyumba mtu mmoja pale magogoni. Ni mwenyekiti wa Mfuko wa maendeleo ya Bagamoyo! nk..nk..nk..nk..kila palipo na pesa kwenye serikali ya magamba, Subash yupo.

Hilo gazeti lilianzishwa kupambana na Mengi, lilipomaliza kazi hiyo ya kumchafua Mengi, likaanza kazi ya kuwafurahisha magamba. Kila siku lina habari za CDM, ni la propaganda kuliko hata Uhuru na Mzalendo.

Mhariri wake aliwahi kukamatwa na rushwa mara kadhaa....
Duh!...amaaa kweli, ukistaajabu ya Musa......
 
Hivi mtu unatoaje pesa yako kununua takataka ya namna hiyo!!! Nadhani anataka auze copy ili apate japo pesa ya kununulia dagaa manake maisha magumu sana kwa kweli. Baraza la Habari wako wapi kwenye hilo? Eti nalo liko kwenye orodha ya mkuu wa posta..Kweli nchi tunayo. Utasikia Tanzania tuna media company nyingi sana kwa idadi na huku SAUTI HURU nalo linahesabika!! How....
 
hahaha, magamba acheni na na hao , hawa watu noma, wanaweza kweli kuleta chma chenye jina kama hilo kuchanganya tu watu...
 
HIVI HABARI KAMA HII WAHUSIKA WALIOTAJWA HAPO HAWAWEZI KUSHTAKI MAHAKAMANI?

Nauliza kwasababu hii habari inaweza kuwa na negative impacts kwa baadhi ya wananchi na kuleta shida kwenye jitihada za ukombozi. Naamini waliotajwa hapo juu wana sababu zote la kulishtaki hili gazeti.
 
Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuamini ujinga kama huu. CCM mtakukuruka sana lakini hamtoki watanganyika wamewachoka mno.
 
Kuweni makini wana CDM. Nyinyiemu hawana njia nyingine mbali na kuwafitinisha viongozi wa juu wa CDM. Walifanya hivyo NCCR, kazi hiyo wakampa akiyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Mzalendo, Marehemu Yahya Buzaragi, mgogoro ukaanza hadi NCCR ikafa. Hawa akina Sauti Huru ni walewale.

Hebu kama mna kumbukumbu wiki iliyopita Uhuru lilikuwa na habari ati Dr Slaa nusra aihame CDM. Hatujakaa sawa,Sauti Huru wana habari kuwa itaundwa CDM Asilia. Lengo ni kurudia uongo mara nyingi ili baadaye uonekane ukweli na CDM waanze kutafutana, na ndo mwisho wa CDM.

Naomba viongozi wa CDM kuwa makini sana kipindi hiki ni nyeti sana!
 
magazeti kama haya huwa hayadumu kwenye mzunguko yanakuwa yamefunguliwa kwa madhumuni maalum pindi malengo yakifeli yanapotea ,gharama zinakuwa ni kubwa kuliko faida ingawaje mara nyingi hawaangalii faida bali ujumbe umefika umepokeleweje .nk
 
Waliingia madarakani kwa mbinu kama hizi.. Na wanataka kuendelea kung'ang'ania madaraka kwa mbinu kama hizi.. Wamesahau kwamba madaraka ni uongozi.. kuhakikisha wale unaowaongoza wanapata neema na maisha yao.. Wameshindwa kubadilisha maisha ya watanzania na kuamua kujinufaisha wenyewe..

Kimbunga kinawang'oa sasa.. Hakuna pa kushikia wala kujificha.. Tufani itawakumba na hakika watalipa kwa mabaya yote waliowatendea wananchi kwa miaka yote hii...
 
Kuondoka CCM ni kama mvua kunyesha, huwezi kuzuia, ila unaweza kujikinga usilowane, wanachofanya wanaCCM wanaohamia CDM ni kuzuia wasilowane na ndo akili nzuri.
 
Linamilikiwa na Subash Patel pale MM Integrated, Kijitonyama. Subash wa kashfa ya Chavda, rafiki na Jeetu Patel wa EPA. Jamaa anazo kwelikweli. Alitajwa na Mzee Mengi kuwa kati ya mapapa wa ufisadi.

Ni yule aliyeshirikiana na Lowassa wakauziana jengo la Umoja wa Vijana wa magamba

Ndiye mwenye maghorofa yale mawili pale UV Magamba. Ana kampuni inaitwa Estim inapata tenda nyingi sana serikalini. Inamjengea nyumba mtu mmoja pale magogoni. Ni mwenyekiti wa Mfuko wa maendeleo ya Bagamoyo! nk..nk..nk..nk..kila palipo na pesa kwenye serikali ya magamba, Subash yupo.

Kila siku lina habari za CDM, ni la propaganda kuliko hata Uhuru na Mzalendo.

Mhariri wake aliwahi kukamatwa na rushwa mara kadhaa....

Kama sikosei ni JUMA PINTO. Aksante kwa kunikumbusha huyu mwanaizaya fisadi papa nilikuwa nimesahau kuwa ndiye mmiliki wa SAUTI HURU
 
Magazeti bila Tittle yenye kuisifia Chadema huuzi kabisaaaaaaa! au ukitaka kuuza lazima uiponde CCM hiyo ndio siri ya biashara ya magazeti kwa sasa
 
Linamilikiwa na Subash Patel pale MM Integrated, Kijitonyama. Subash wa kashfa ya Chavda, rafiki na Jeetu Patel wa EPA. Jamaa anazo kwelikweli. Alitajwa na Mzee Mengi kuwa kati ya mapapa wa ufisadi.

Ni yule aliyeshirikiana na Lowassa wakauziana jengo la Umoja wa Vijana wa magamba Nape hakuona ngawira zilipitia wapi, ndo akaanza fujo UV magamba mpaka akakosana na rafiki wa marehemu baba yake Mzee Makamba! Kumbukeni msiba wa marehemu mzee Moses Nnauye ulikuwa kwa Makamba jijini.

Ndiye mwenye maghorofa yale mawili pale UV Magamba. Ana kampuni inaitwa Estim inapata tenda nyingi sana serikalini. Inamjengea nyumba mtu mmoja pale magogoni. Ni mwenyekiti wa Mfuko wa maendeleo ya Bagamoyo! nk..nk..nk..nk..kila palipo na pesa kwenye serikali ya magamba, Subash yupo.

Hilo gazeti lilianzishwa kupambana na Mengi, lilipomaliza kazi hiyo ya kumchafua Mengi, likaanza kazi ya kuwafurahisha magamba. Kila siku lina habari za CDM, ni la propaganda kuliko hata Uhuru na Mzalendo.

Mhariri wake aliwahi kukamatwa na rushwa mara kadhaa....

Ok ndiyo mwenye KIBOKO PAINTS, MM STILL, ULTMATE SECURTY ILIYOPATA TENDA YA KUTOA HUDMA YA DHARURA AMBULANCE MSAFARA WA JK.
 
Mafisadi maji ya shingo kila kukicha wanafikiria tu CDM... Hatuwaachi wapumue Muda unakaribia... Wametudanganya tangu miaka 50 iliyopita, hatuwapi nafasi tena...

Watanzania wa DINI zote, Makabila Yote, Sehemu zote Bara au Visiwani tusiwape hawa mchwa nafasi maana wametutia sisi vilema, sasa wanataka watoto wetu je hadi wajukuu wawe vilema? Namaanisha vilema vya kutokuwa na elimu Bora, Afya Bora, Na Maisha Bora kwa ujumla..

Tuipe Chadema hasa mwenyekiti akiwa Mbowe kwa angalau miaka mitano tu halafu tutaweza kufanya comparison nafuu ni wapi...

Nimesikia kauli nyingi sana za watu wetu wa Usalama wakituhadaa eti vyama vya upinzani vyote sawa. Na mimi nasema inawezeka vikawa sawa lakini si CCM.. Kwa CCM watu weupe I mea wahindi, waarabu, Wachina, wazunngu etc na Wakenya, wasomali na wote wasio waTZ ni bora kuliko watanzania ukitaka kulihakikisha hilo nenda kwenye makampuni yaliyobinafsishwa utajua....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom